Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, April 30, 2011

DVD YA SUPER D BOXING COACH KUPATIKANA KIURAISI KESHO PTA

Rajabu Mhamila Super D (kushoto) akisisitiza jambo wakati anaelekeza vitu vya msingi vilivyomo katika Video ya mafunzo ya mchezo wa ngumi kulia ni Said Chaku, Amri Massare na Antoni Ruta

Edson Joel na Zaituni Kibwana wakiangalia kava ya Super D Boxing Coach leo
Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D (kushoto) akitoa maelekezo yaliyomo katika DVD yake ya mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa wadau wa mchezo huo kutoka kulia ni Saidi Chaku, Amri Masare, Zainabu Kiliware, Edson Joer na Antoni Ruta Dar es salaam leo ambapo VIDEO CD hazo zitapatikana kwenye mapambano yote ya ngumi nchini

HAPPYBIRTHDAY PRINCESS ASIA MAHMOUD ZUBEIR

Pichani ni Mtoto Princess Asia 'Checha' leo anatimiza miaka minne ya kuzaliwa. Anawasalimu mama yake Dina Ismail mwendeshaji wa Blog ya Mamapipiro.blogspot.com, Baba yake Prince Mahmoud Zubeir.Pia anamsalimu Dada yake Precious na mdogo wake Prince Akbar wote wakiwa Kinondoni Dar es Salaam. Babu na Bibi Checha wanaoishi Tabata, mwisho awawasalimu Aunt Ankal Abbas,Aunt zake Amina na Miski.Mwendeshaji wa Blogu hii nakupongeza Baby Checha pia nakuombe kwa mungu akujaalie umri mkubwa na undelee kuwa mtoto mtiifu kwa wazazi wakubwa na wadogo pia endelea na moyo huohuo wa kupenda shule.

WAFANYAKAZI IDARA YA HABARI (MAELEZO) WAMUAGA RASMI MKURUGENZI CLEMENT MSHANA ALIYETEULIWA KUONGOZA TBC

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Clement Mshana (kushoto) akikabidhiwa zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara hiyo na Ofisa Habari Mwandamizi, Anna Itenda (kulia)wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Mshana ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .
Clement Mshana, akizungumza na wafanyakazi wa Idara hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na wafanyakazi hao.

Wafanyakazi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Clement Mshana (katikati) baada ya hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Idara hiyo jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha Zote na Aron Msigwa-MAELEZO

VIMWANA WA TWANGA KUONYESHA NYONGA ZAO LEO USIKU MANGO GARDEN 'TWANGA CITY'


Mratibu wa Shindano la Kimwana wa Twanga Maimatha.





Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” Jumamosi tarehe 30-04-2011 inataraji kutumia onyesho lake katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, kuwasugulisha kisigino washiriki wa shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011.
Sugua Kisigino ni mtindo unaotumiwa na Twanga Pepeta na ni moja ya staili zitakazotumika kwenye shindano hilo, hivyo washiriki watatumia fursa hiyo ili kufahamu jinsi ya kucheza staili hiyo.
Washiriki watatumia onyesho hilo ili kusalimu mashabiki wa Mango Garden ukumbi ambao una historia ndefu na Twanga Pepeta.
Onyesho rasmi la utambulisho wa Vimwana wa Twanga Pepeta 2011 unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 06-05-2011 ndani ya Club ya Sun Cirro iliyoko Sinza na Fainali itakuwa Ijumaa tarehe 03-06-2011.
Burudani ya Utambulisho wa Shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 itatolewa na Wakali wa Dansi Tanzania, African Stars Band “Twanga Pepeta” na Msanii Abbas Kinzasa maarufu kama 20 percent au asilimia ishirini, pamoja na shoo kali ya Nyonga teketeke ya Vimwana wa Twanga Pepeta.
MAIMARTHA JESSE
MRATIBU WA SHINDANO.
http://bongoweekend.blogspot.com/

SHINDANO LA MISS TANZANIA LAZINDULIWA RASMI KILIMANJARO KEMPINSKI DAR ES SALAAM




Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala akiwa katika picha ya paoja na warembo waliowahi kuvaa Crown ya Miss Tanzania anaye fuata baada ni Angela Damas, Nasreen Karim, Jacqueline Ntuyabaliwe, Hoyce Temu, Saida Kessy na Richa Adhia.

Wadau hawa wakifuatilia uzinduzi wa mashindano haya ya urembo ambayo yamezinduliwa rasmi.
Mratibu wa Miss Tabata Fred Ogot akiwa na Miss Tabata 2010 Consolata Lukosi.
Mbunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi nchini Ally Rhemtullah.

Muandaaji wa Kituo cha Kurasini Miss Kurasini Bibie Zuhura naye alikuwepo.

Somoe Ng'itu kulia na Khadija Kalili
Mhariri wa Habari za Michezo na Burudani Suleiman Mbuguni na Khadija Khalili.

Mama wa Bongoweekendblog nikijiegesha nje mara baada ya hafla hiyo.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency pia Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Dar es Salaam.

Kampuni ya Viodacom usiku huu imezindua rasmi shindano lake la urembo la Miss Tanzania kwa kipindi cha maka 2011.Hapa Meneja udhamini wa Kampuni hiyo George Rwehumbiza amesema kuwa wao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo.Waliosimama nyuma yake ni baadhi ya warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.

Meneja Udhamini wa Kampuni hiyo ametoa wito kwa wazazi kuwapa ushirikiano vijana wao wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo na hivyo kuonyesha vipaji vyao ."Pia nachukua fursa hii kuwaomba wasichana kokote walipo hapa nchini wajitokeze kwa wingi kushiriki katika shindano hili na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika kuitumikia jamii yetu".

Hawa ni baadhi ya warembo Miss Tanzania ambao walikuwepo katika uzinduzi wa rasmi wa shindano na nembo mpya ya mdhamini wao Kampuni ya simu ya Vodacom waling'ara kwa miaka tofauti na kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya dunia .Kutoka kushoto ni Angela Damas Miss Tanzania (2001),Nasreen Karim (Miss Tanzania 2009),Jacqueline Ntuyabaliwe (Miss Tanzania 2000),Genevieve Mpamnaga (Miss Tanzania 2010) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997).

Hapa tukishangweka SHOSTITO Miss Tanzania 1999 pia alikuwa Miss Ilala kwa mwka huo Hoyce Temu asiyechuja , Dina, Khadija nyuma ya Hoyce na menye kivazi cha buluu ni Somoe.

Mbunifu wa mitindo ya mavazi nchini Ally Rhemtullah katika uzinduzi huo .

Kutoka kushoto ni Dina, Mambo na Suleiman wote kutoka gazeti la Majira na Khadija.

http://bongoweekend.blogspot.com/

MAPACHA WATATU NA WANAUME TMK KUTUMBUIZA IKWETA GRILL LEO


BENDI ya muziki wa Dansi ya Mapacha Watatu na Kundi la muziki wa kizazi kipya TMK Wanaume Family, leo watafanya onesho moja kwenye Ukumbi wa Ikweta Grill uliopo Mtoni kwa Azizi Ali, Temeke.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa onesho hilo, Zahor Said alisema kuwa maandalizi ya onesho hilo yamekamilika kama walivyopanga na wapenzi wote wa burudani katika sehemu za Temeke na maeneo ya jirani watarajie mambo makubwa.
Alisema katika onesho hilo litakaloanza saa 3 usiku, watoto wa Temeke, Wanaume Family watakuwa wa kwanza kufanya makamuzi yao juu ya jukwaa ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya onesho kwenye ukumbi huo.
Said alisema mapacha wao watatoa burudani yao ikiwa ni pamoja na kupeleka tuzo zao za Kili Music Awards ambazo walizitwaa kutokana na umahiri wao.

MTOTO WA MFALME, WILLIAM AFANYA KUFURU KWA KUFUNGA NDOA YA KIFAHARI ILIYOGHARIMU MABILIONI YA PESA


Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

MTOTO wa mfalme wa Uingereza, Prince William na Kate Middleton wamefunga ndoa katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.

Takriban wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa, na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao kwa njia ya televisheni.


Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.


Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981.


Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.


Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke".


Kuanzia sasa maharusi hao watajulikana kama Duke na Duchess wa Cambridge.


Friday, April 29, 2011

MBUNGE ESTER BULAYA AANDAA MICHUANO 'BUNDA ESTER CUP'





Na Mwandishi Wetu

MICHUANO ya Ester Cup inayofadhiliwa na mbunge wa viti maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo wilayani Bunda mkoani Mara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jijini Dar es Salaam, mbunge huyo alisema lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji, kutoa burudani pamoja na kuwakutanisha vijana pamoja ili kukuza umoja na mshikamano baina yao.Alisema mashindano hayo yatazishirikisha timu 10 zitakazopepetana katika viwanja vya Sabasaba na Shule ya Msingi Bunda ambapo kilele chake kitakuwa Mei 4 mwaka huu.Aidha Bulaya alibainisha kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia seti ya jezi, kombe na mipira miwili, mshindi wa pili atajitwalia seti ya jezi na mpira mmoja huku mshindi wa tatu atakabidhiwa seti ya jezi.Timu yenye nidhamu itakabidhiwa seti ya jezi huku mfungaji na golikipa bora kila mmoja atajinyakulia mpira mmoja.
“Nimedhamiria kuwaunganisha vijana pamoja kwa kuwa ubunge wangu niliupata kwa tiketi ya vijana, nina mpango wa kugawa jezi, mipira na viatu katika Kata zote za mkoa wa Mara,” alisema Bulaya.Alisema anaamini kuwa michezo ni ajira hivyo wataitumia michuano hiyo kuonyesha vipaji vyao vitakavyowawezesha kuonekana kwa wadau ili wasajiliwe katika klabu mbalimbali.http://bongoweekend.blogspot.com/

AMPLIFAYA ya BIG BROTHER kulindima Mei Mosi, BHOKE kuiwakilisha TANZANIA.......!


Bhoke, presenter wa TV nchini anatarajiwa kuingia kwenye Jumba la BigBrother kuiwakilisha BONGO ktk mchezo huo unaotarajiwa kuanza Jumapili hii ya tarehe 1 may na kuishi humo ndani kwa siku 91 akiwa na washiriki wengine kutoka nchi 13.

We wish u all the best sista

Big Brother Africa
Six seasons on, and the incredibly popular Big Brother Africa has been Amplified. Running 91 days and 24/7 with a dream grand prize of USD 200 000, this season of Africa’s biggest reality show will include more of the drama, the emotion, the excitement and the suspense that have made the series a firm fan favourite.




M-Net Africa Managing Director Biola Alabi, breaks it down:
“By definition amplified means to increase the volume, to make louder, to make more powerful. And that’s exactly what we want to do with season six.”

Looking at the Eye
With a dramatic new eye, etched in a carbon fibre background with an edgy, futuristic feeling and a sophisticated, polished, reflective finish, the newly unveiled show logo sets the scene for a bold new season!

The Housemates
Big Brother Amplified will showcase Housemates from 14 countries this year: Angola, Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Mozambique, Namibia, Nigeria, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.

Big Brother has enjoyed a growing popularity across the continent and M-Net is pleased that it draws support from Africans across borders and outside of the nationalities represented. This serves to highlight that Africans support other Africans regardless of where they live or what their nationality is.

Big Brother is Watching, Big Time
Big Brother Amplified is produced for M-Net by Endemol and will be filmed on location in a brand new House in Johannesburg, South Africa.

The series will once again be hosted by charismatic IK Osakioduwa. The fabulous host has been at the heart of the action since he joined the show two seasons ago.

BSS 2011 kukopi style ya Big Brother All stars...!


Mariam

Shindano la Bongo Star Search BSS kwa mwaka huu linatazamiwa kushirikisha washindi wa sessions za miaka minne iliyopita ambao ni kwa mshindi wa kwanza na wa pili kwa madai ya kupewa 'Second chance' ili kuinua upya vipaji vyao kutokana na kufifia ktk soko la muziki la bongo.Tofauti na wadau wengi waliotegemea kuona vipaji vipya vilivyozagaa mitaani vikikosa msaada

J4

James

Rogers Lucas

Leah Moudy

Mara nyingi washindi na washiriki Ma-star wa bongo kutoka BSS huwa hawaonekani ktk game ya muziki baada ya mashindano yao kumalizika, wakati wanapokuwa wanaimba copy za miziki ya wasanii wengine husifiwa na kuaminika watakuja kuwa wasanii wakali saaaaana!

Bench Mark Production imeonelea kuwainua mastar hao kwa mara ya pili huku wakitumia mtindo uliotumiwa na lile shindano la Big Brother Africa 2010 ambapo walishirikisha washiriki wa mashindano yaliyopita lakini wao hawakutumia washindi na kuiita Big brother All stars'

Paschal Cassian

Nawatakia kila Lakheri mastar wa BSS labda safari hii wataweza kuonyesha kazi zao nzuri kiasi cha ku-shine kama wenzao wa Tusker project fame

Thursday, April 28, 2011

CREDO MWAIPOPO AJINADI BONGO




KIUNGO wa zamani wa timu ya soka ya Yanga, Credo Duncan Mwaipopo (pichani kushoto), kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam akisaka timu ya kujiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Credo aliyekuwa akicheza soka ya kulipwa nchini Sweden alisema kuwa mkataba wake wa kucheza soka nchini humo umeshamalizika, hivyo yupo tayari kujiunga na timu yoyote itakayomhitaji.
“Nina miezi minne tangu nitue hapa nchini, nipo katika kusaka timu yoyote ya kuichezea hapa nchini na hadi sasa sijapata timu yoyote, hivyo nipo tayari kujiunga na timu yoyote itakayonihitaji,” alisema Credo.
Credo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio miaka ya nyuma kabla ya kutimkia nchini Sweden, alieleza kuwa alishindwa kuendelea na klabu yake ya Pannelinois IF inayoshiriki ligi daraja la pili kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimwandama.
Alisema kuwa anaendelea na mazoezi katika viwanja mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuonyesha uwezo wake endapo atapata timu itakayomsajili kwa msimu ujao wa ligi.
http://mamapipiro.blogspot.com/

BENKI YA EXIM YAAHIDI KUINUA UCHUMI WA NCHI





Na Mwandishi


WetuBenki ya Exim imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika mikakatimbalimabli ya kuinua uchumi wa nchi.

Hayo yalisemwa jijini jana na Meneja Mkuu wa benki hiyo, Bwana Dinesh Arora.

Alikuwa akizungumzia ufadhili wa benki hiyo kwenye mkutano wa uwekezaji Afrikauliofanyika jijini katikati ya mwezi huu na kuhudhuriwa na maraisi watano kutokanchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki na wajumbe zaidi ya 900 kutoka sehemumbalimbali duniani.Alisema kuwa sekta binafsi inao wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuinuauchuni na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania.

“Exim Benki iliona fahari kubwa kufadhili mkutano huu ambao ulikuwa una lengo la kuonyesha utajiri wa rasilimali za nchi na pia kufungua fursa za kibiashara”,alisema.Bwana Arora alisema kuwa Benki ya Exim itaendelea kusaidia fursa kama hizo ilikuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuweza kupata nafasi ya kukutana nawafanyabiashara kutoka sehemu nyingine za dunia.Alisema kuwa benki yake ina wajibu mkubwa wa kuendelea kuisaidia uchumi wan chikukua.Alisema kuwa ili wajasiriamali wa Kitanzaniia waweze kukua kibiashara na kutoamchango mkubwa zaidi kwenye uchumi,lazima ziwepo juhudi za makusudi zakuwakutanisha na wawekezaji kutoka Afrika na duniani kote. “Tunaamini kuwa maendeleo ya benki yetu yanategemea sana mafanikio ya jamiiyetu tunakofanyia kazi”alisema. Alisema pamoja na biashara benki hiyo ina jukumu la kuchangia shughulimbalimbali za kijamii na kwamba Ujasiriamali ni miongoni mwa sektazinazochangiwa kwa nguvu na benki husika.“Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini pia tumekuwana majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini wetu katika TEYA nimiongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo na kwamba Ujasiriamali tunauangaliakwa namna ya kipekee,” alisemaAliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa sekta ya hiyo,hivi karibuni wamefunguaakaunti mpya ya Tumaini maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali wanawake.Alifafanua kuwa pamoja na wengine wanawake ni mhimili mkuu wa shughuli zakijamii katika familia nyingi za kitanzania hivyo benki hiyo imeona ipo haja yakipekee kuwawezesha ili nao waweze kumudu majukumu yao kwa ufanisi.Kuhusu tuzo hiyo alisema ni changamoto ya kutosha kwa Wajasiriamali nchinikatika kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinakuwa na tija kwao binafsi na taifakwa ujumla.“Akaunti ya Tumaini ni maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali Wanawake na hiiinaonyesha jinsi tunavyoijali sekta hii lakini pia tuzo hii ni changamoto kubwakwa wahusika kwani itawasukuma kufanya shughuli zenye tija,” alisema Bwana Arora.TEYA imelenga kutambua kazi za Wajasiriamali katika nyanja mbalimbali kutokanana mchango wao katika pato la taifa na ukuaji wa uchumi lakini pia kutoachangamoto ya ushindani kwa wahusika na sekta ya kibiashara kwa ujumla.

TEYA 2011 ilizinduliwa rasmi Machi 15 mwaka huu na inatarajiwa kutolewa baadayeNovemba ambapo Raisi Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mawazo WaziriMedia Relations ManagerCapital Plus International (CPI)Phone:

Wednesday, April 27, 2011

MBWANA MATUMLA ANOGESHA NGUMI ILALA

Bondia Mbwana Matumla (kulia) akioneshana umwamba wa kutupa makonde na Omari Bayi wakati wa tamasha la kuamasisha mchezo wa ngumi uliofanyika, Dar es Salaam jana mabondia wote wanajiandaa na mapambano yao yatakayofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam
Baadhi ya wadau wa Mchezo wa ngumi wakibadilishana mawazo
BABY IKOTA SUPER D MNYAMWEZI AKISALIMIANA NA HABIBU KINYOGOLI

KANUMBA ATOKA NA Ramsey WA NIGERIA

Msanii wa filam kutoka Nigeria, Ramsey Tokumbo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana baada ya kufanya kazi na msanii Stevin Kanumba kushoto ambapo alieleza mafanikio aliyoyapata na kuondoka

Hadija Khalili akipiga picha na Kanumba wa Bongo mover

Tuesday, April 26, 2011

POMBE SI CHAI MNENGUAJI AKUDO IMPACT AZIMIKA


Katika nderemo za Pasaka, ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar, mrembo mpya wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ katika safu ya unenguaji, Mariam Sagwa alijikuta akidondoka stejini na kuzimika kwa dakika kadhaa baada ya kupandwa na ‘mzungu’ wakati akinengua.



Hata hivyo, wanenguaji wenzake walimpiga ‘tafu’ ya kusimama lakini alionekana akiyumbayumba hadi alipotolewa stejini.

Monday, April 25, 2011

NGUMI KUPIGWA PANANDIPANANDI ILALA BUNGONI KESHO




MABONDIA wa ngumi za ridhaa wa mkoa wa Ilala wanatarajia kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Dar es Salaam. ambapo kutakuwa na ngumi kutoka kwa mabondia mbalimbali toka pande zote za mkoa wa DAr es Salaam

Tamasha hilo litakalokuwa likitimua vumbi kila wiki inatarajia kuwakutanisha mabondia wa Ilala na wa sehemu nyingine za Dar es Salaam ili kuweza kujipima nguvu katika kuinua mchezo huo katika mkoa huo.

Katika Tamasha hilo kesho bondia Mbwana Matumla anayejiaandaa kwa ajili ya kushiriki katika kuwania ubingwa wa UBO pambano linalotarajia kufanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa PTA dhidi ya Mkenya Gabriel Ochieng atachuana na mabonmdia Yohana Robert na Issa Sewa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Tamasha hilo kupitia Taasisi ya Kinyogoli foundation, Habibu Kinyogoli alisema mapambano yote yatakuwa katika raundi nne huku pambano la Mbwana likiwa katika uzito wa Kg 55 likiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano lake hilo.

Alisema, mkakati huo wa kuanzisha Tamasha akishirikiana na kocha msaidizi wa timu ya mkoa huo Rajabu Mhamila 'Super D' utasaidia kuinua vipaji vipya vya mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani kutawajenga wachezaji kujikita katika mchezo huo na kuufanya kama ndio ajira yao.

Alisema, katika kulifanikisha hilo anawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kuwadhamini ili waweze kufikia malengo yao katika kuinua vipaji hivyo.pia alisema kutakuwa na wageni waalikwa ambao watatoa mada mbalimbali kuhusu kuinua mchezo wa ngumi Tanzania akiwemo mdau wa ngumi.Innocente Melleck na mwingine Benedictor Hulilo ambao watakuwa wageni waalikwa

MASHINDANO YA SAFARI LAGER DARTS AFRIKA MASHARIKI YAMALIZIKA

Mratibu wa michezo ya DARTS Innocente Melleck akipanga zawadi mbalimbali za vikombe vilivyotolewa kwa washiriki
Mratibu wa michezo ya DARTS Innocente Melleck akipanga zawadi mbalimbali za vikombe vilivyotolewa kwa washiriki
Wachezaji kutoka Kenya wakishangilia baada ya kuimba wimbo wao wa Taifa
Wachezaji wa Kenya wakiimba wimbo wa Taifa

Wachezaji wa Uganda wakimba wimbo wa Taifa wakati wa Fainali
Mchezaji wa mchezo wa vishare, Julieth Kantumbare kutoka, Uganda akirusha wakati wa mashindano ya Afrika Mashariki yaliyomalizika Dar es salaam mwishoni mwa wiki ambayo yalizaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari
Mchezaji wa mchezo wa vishare, Dinah Amoding kutoka, Uganda akirusha wakati wa mashindano ya Afrika Mashariki yaliyomalizika Dar es salaam mwishoni mwa wiki ambayo yalizaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...