Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 13, 2012

MZEE MWINYI MGENI RASMI TUZO ZA WANAMICHEZO BORA TZ KESHO



Mwenyekiti wa TASWA, Juma Abbas Pinto katikati akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, kulia Katibu wake Amir Ally Mhando na kushoto ni Meneja Mawasiliano wa SBL, Imani Lwinga.

RAIS mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za utoaji wa tuzo za wanamichezo bora Tanzania kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Abbas Pinto amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu, ukumbi wa City Sports Lounge, Mtaa wa Samora, Dar es Salaam kwamba, wamemchangua Mwinyi kwa sababu alikuwa ana mchango mkubwa katika sekta ya michezo enzi zake, akiwa Ikulu tangu 1985 hadi 1995 alipomuachia Benjamin William Mkapa.
Pinto amesema kwamba maandalizi ya sherehe hizo yamekamilika na anawashukuru sana wadhamini wa tuzo hizo, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa mchango wao mkubwa.
Katika tuzo hizo, kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima wa Yanga, atachuana na Kipre Tchetche wa Ivory Coast anayechezea Azam FC na Mganda Emmanuel Okwi wa Simba kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka wa kigeni.
Kwa upande wa wanasoka wazalendo, tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka inawaniwa na John Bocco, Aggrey Morris, wote wa Azam na Juma Kaseja wa Simba, wakati kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza nje wanaoshindana ni Henry Joseph wa Kongsvinger ya Norway na Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC.
Kwa upande wa wanawake, Sophia Mwasikili anayecheza Uturuki, anashindana na Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamisi Omary wote wa Mburahati Queens, Fatuma Mustapha wa Sayari na Eto’o Mlenzi wa JKT.
ORODHA KAMILI YA WANAOWANIA TUZO:
KIKAPU:
WANAWAKE
DORITHA  MBUNDA :-JKT QUEENS
EVODIA  KAZINJA:-JKT QUEENS
FARAJA MALAKI:-JESHI STARS
WANAUME
ALPHA KISUSI-Vijana
FILBERT MWAIPUNGU:-ABC
GILBERT BATUNGI:-ABC
NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION
 DORITHA MBUNDA
 GOFU
WANAWAKE:
Madina Iddi (Umri miaka 27)
Hawa Wanyeche (Umri miaka 26)
Ayne Magombe (Umri miaka 24)
WANAUME:
Frank Roman
Nuru Mollel
Issac Anania
GOFU WA KULIPWA:
FADHILI  SAIDI NKYA.
YASINI SALEHE
HASSANI KADIO
OLIMPIKI MAALUM
Ahmada Bakar
Amina Daud Simba-kisahani na tufe
Othman Ally Othman-mkuki, kisahani na tufe.
Cio..
PARALIMPIKI
WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI
JOSEPH NZIKU
YOHANA MWILA
WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE
SIWEMA KILYENYI
JANETH MADISE
NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA
VICTOR NJAITI
ABDALAH KASSIM
CIO…
WAOGELEAJI
(WANAWAKE)
MAGDALENA MOSHI
GOURI KOTECHA
MARIAM FOUM
WANAUME
AMMAAR GHADIYALI
OMARI ABDALLAH
JUDO...
 MBAROUK SELEMANI MBAROUK
UNDER 81KG MEN JUDO PLAYER
 MOHAMED KHAMIS JUMA
OVER 90KG MEN JUDO PLAYER
 AZZAN HUSSEIN KHAMIS
UNDER 60KG Judo player
CIO…
WAVU…
WANAWAKE
ZUHURA HASSAN-JESHI STARS
THERESIA Ojode -JESHI STARS DAR
EVERLYNE ALBERT- MAGEREZA
WANAUME
MBWANA ALLY- MZINGA CORPORATION  - MOROGORO
KEVIN PETER -MAGEREZA – DAR
FARHAN ABUBAKAR- MAFUNZO ZNZ
CIO…
NGUMI ZA KULIPWA
Benson Mwakyembe
Nasibu Ramadhan
Francis Cheka
Nassib Ramadhan
Fadhil Majia
TENISI:
WANAUME
WAZIRI SALUMU
 OMARY ABDALAH
HASSANI KASSIMU
WANAWAKE
REHEMA ATHUMANI
 MKUNDE IDDY
VIOLET PETER
Cio…
BAISKELI
Wanawake
Sophia Hussein
Sophia Anderson
WANAUME:
Richard Laizer
Hamisi Hussein
WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE
Henry Joseph-Soka
Mbwana Samatta-Soka
Sophia Mwasikili-Soka
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI
Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars)
SHOMARI KAPOMBE- (soka) SIMBA
Salum Abubakari-Azam (soka)
MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Haruna Niyonzima-Yanga (soka)
Kipre Tchetche-Azam (soka)
Emmanuel Okwi-Simba (soka).
SOKA (WANAWAKE)
Asha Rashid-Mburahati Queens
Mwanahamisi Omary-Mburahati Queens
Fatuma Mustapha-Sayari
Ito Mlenzi-JKT
WANAUME
John Bocco-Azam
Aggrey Morris-Azam
Juma Kaseja-Simba
RIADHA
WANAWAKE
Zakia Mrisho
Mary Naali
Jaqueline Sakila
WANAUME
Dickson Marwa
Alphonce Felix
MIKONO
WANAWAKE
Abinery Kusencha-JKT Ruvu
Kazad Mtong-Magereza Kiwira
Faraji Shaibu  Khamis-Nyuki Zbar
WANAUME:
Doris Mangara-Magereza Kiwira
Zakia Seif-Ngome Dar
Mary Kimiti-Magereza Kiwira.
Cio…
KRIKETI
WANAWAKE
MoniCa Pascal
Asha Daudi
Esther Wallace
WANAUME
Kassimu Nassoro
Benson Mwita
Riziki Kiseto
TUZO YA HESHIMA-ITATANGAZWA SIKU HIYO
MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA 2011-ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO.

2 comments:

  1. You would back test the system for a long period using numerous currency crosses.
    It is preferable when these trades were done over many accounts,
    many a broker and currency pairs. For the past two years, there have been continuous efforts to publicize and promote the foreign
    exchange market.

    Also visit my blog - forex automated robot

    ReplyDelete
  2. Another program for iPhonw unlocking is
    Redsn0w.

    Have a look at my web-site: Cydia apps ()

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...