Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 30, 2014

SMILEON KUWEZESHA WATEJA WAKE KUWA HEWANI MTANDAONI PALE KIFURUSHI CHA INTANET KINAPOKWISHA


Baadhi ya mahofisa wa Smile wakiwa na furaha uku wameshikili vipeperushi vinavyo onesha kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intanet kinapoisha
Mkuu wa Masoko wa Kampuni Smile Bi, Linda Chiza kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya SimelON kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intaneti kinapokwisha kushoto ni Head of Operational Efficiency and Compliance Bw. Athumani Nzowa
Mkuu wa Masoko wa Kampuni Smile Bi, Linda Chiza kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya SimelON kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intaneti kinapokwisha kushoto ni Head of Operational Efficiency and Compliance Bw. Athumani Nzowa na kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Smile Edgar Mapunde



Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini  maofisa wa Smile

WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA WAAPISHWA LEO NA RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha   Mabrouk Jabu Makame   kuwa Mjumbe  wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ambapo anaendelea na kazi hiyo kwa kipindi chengine cha miaka mitatu,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Hamid Mohamoud  Hamid kuwa Mjumbe  wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ambapo anaendelea na kazi hiyo kwa kipindi chengine cha miaka mitatu,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Hamid Mohamoud  Hamid kuwa Mjumbe  wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo ambapo anaendelea na kazi hiyo kwa kipindi chengine cha miaka mitatu,
KWA MATUKIO ZAID BOFYA READ MORE

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA


      

PG4A0416Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba, Kapteni John Komba, Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A0440Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir kificho (kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi wakiteta, Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A0462Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Lazaro Nyarandu (kushoto) na Mwigulu Mchemba wakiteta, bungeni Mjini Dodoma Septemba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A0533Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza, Bungeni Mjini Dodoma Septembe 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A0633Mwenyekiti  wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta akifafanua kuhusu namna wajumbe wa Bunge hilo watakavyopiga kura, bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A0777Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Bernard Membe wakiteta kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 29, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAASISI YA VYOMBO VYA HABARI KUSINI MWA AFRIKA(MISA-TAN) YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA NA KUTOA MATOKEO YA UTAFITI WA UPATIKANAJI WA TAARIFA KWENYE OFISI ZA UMMA NCHINI TANZANIA‏‎



Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akiwakaribisha wageni waalikwa na waandishi wa habari waliofika kweye mkutano wao uliofanyika Jana kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam kulia ni  Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew.
Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Jana imekutana na waandishi wa habari na wadau tofauti katika kuadhimisha Siku ya haki ya kupata taarifa kimataifa amabayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.09.2014 katika ofisi zao zilizopo kinondoni Mkwajuni Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28 kwa kila mwaka.
 Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wagene waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa zinazoadhmishwa septemba 28 kwa kila mwaka. kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (kushoto) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini.
 Mkurugenzi  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kitabu cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma.

SMILEON KUWEZESHA WATEJA WAKE KUWA HEWANI MTANDAONI PALE KIFURUSHI CHA INTANET KINAPOKWISHA

Baadhi ya mahofisa wa Smile wakiwa na furaha uku wameshikili vipeperushi vinavyo onesha kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intanet kinapoisha
Mkuu wa Masoko wa Kampuni Smile Bi, Linda Chiza kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya SimelON kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intaneti kinapokwisha kushoto ni Head of Operational Efficiency and Compliance Bw. Athumani Nzowa
Mkuu wa Masoko wa Kampuni Smile Bi, Linda Chiza kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya SimelON kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intaneti kinapokwisha kushoto ni Head of Operational Efficiency and Compliance Bw. Athumani Nzowa na kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Smile Edgar Mapunde



Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini  maofisa wa Smile





Monday, September 29, 2014

Bondia wa Kike mwafrika Bintou Schmill Bingwa mpya wa ngumi Ulaya




 
,Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill,mkazi wa Ujerumani siku ya ijumaa 26.September 2014 alifanikiwa kuchukua taji la ubingwa wa ngumi za kulipwa unatambuliwa na IBF,Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake bondia Mirjana Vujic   kwa K.O katika raundi ya 3,. Pambano hilo lilionyeshwa Live katika TV channel ya euro sport na ktazamwa na maelfu ya watu wakishuhudia bondia wa kike mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radu.Bintou Schmill (30) aka The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,Katika pambano la Ijumaa 26.September 2014 liliofanyika kwenye ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied,lifanikiwa  kumpa wakati mgumu mpinzani wake kuanzia round ya kwanza hadi ilipofika raund 3 bondia Mirjana Vujickatika alipigwa kwa KO na Bintou Schmill aka "The Voice" kutangazwa ndie bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani ulaya na kuvikwa mkanda huo unatambuliwa na IBF.Bintou Schmill aka 'The Voice' anaye fananishwa na Simba Jike (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !
Mengi kuhusu bondia Bintou Schmill aka 'The Voice" usikose at For more information write to
http://www.facebook.com/schmillbintou but first all visit the lion queen

on http://www.bintouschmill.de/     also   http://www.twitter.com/schmillbintou
Vijimambo

Bintou Schmill

BOXING FEATURE: KUELEKEA PAMBANO LA ALIBABA DHIDI YA THOAMS MASHALI OKTOBA 5



Allybaba Ramadhani

Masumbwi ni miongoni mwa michezo nchini Tanzania iliyowahi kuiletea nchi hii medali nyingi kutokana na umahiri wa watupa makonde kujituma vilivyo wawapo ulingoni katika mapambano yao.
Ninapozugumza hivi ninawakumbuka baadhi ya makocha na waliopo kwenye benchi kwenye mchezo wa soka wakati mwingine hutaka kurusha makonde pindi waonapo hali ni ngumu kwa timu zao.
Unamkumbuka kocha Jose Mourinho? kama sio sheria za FIFA kuwa kali angemtwanga kocha wa zamani wa Barcelona, marehemu Tito Vilanova aliyefariki mwaka huu kwa matatizo ya kansa akitoka kuachiwa mikoba na kocha wa sasa wa Bayern Munich, Pep Guardiola.
Mwingine ni German Burgos, kocha msaidizi wa Atletico Madrid akiwa na mtata mwenzake mwenye wenge la hatari, Diego Simeoni wote wakiwa waargentina waliotoka mbali lakini kwenye suala la kurusha ngumu hawajambo.
Unaweza kusema waache kufundisha soka waje, kipande hiki cha urushaji wa makonde, ha ha haaaa! Unacheka?
Hapa nchini tuna wanamasumbwi wengi ambao wamekuwa wakijitahidi kufanya mazoezi lakini hatma yao huwa ni kazi bure wafikapo katika medani ya kimataifa kutokana na mipango mibovu ya kuukuza mchezo huu.
Wapo mabondia wakali nchini wakitiwa moyo kama ilivyo katika soka wanaweza kuitangaza Tanzania kimataifa kwani hakuna kinachoshindikana.
Hata hivyo kuna madaraja ambayo mwanamasumbwi ni lazima apambane ili aweze kusonga hadi kujulikana kimataifa yakiwemo Superfeatherweight, Lightweight, Junior welterweight, welterweight, na Super welterweight.
Sijui kama watoto wetu wanajua haya!
Nchini Marekani miaka ya nyuma kabla ya mwaka 1950 kulitokea kizazi cha warusha mawe wa ukweli Willie Pep, Chalky Wright miaka ya 1944 na rekodi zinaonyesha mchezo huu ndio ulikuwa wa kwanza kurushwa moja kwa moja (live) katika luninga.
Walikuwepo George Foreman, Joe Frazier, na Muhammad Ali waliofanya vizuri katika medani hii na kulitangaza taifa la Marekani baada hapo kikaja kizazi cha kina Mike Tyson, Evander Holyfield na sasa ni kina Floyd  Mayweather.
Kimataifa zaidi wengineo ni Amir Khan, Manny Pacquiao, Marcos Maidana, Rocky Marciano na Oscar de la Hoya.
Leo, tutamwangazia bondia Alibaba Ramadhani wa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro anayetarajiwa kutifuana na bondia Thomas Mashali wa Dar es Salaam hapo Jumapili Oktoba 5 mwaka huu katika pambano litakalofanyika Mkwakwani Mkoani Tanga.
HISTORIA YA ALIBABA RAMADHANI
Jina kamili anaitwa Alibaba Ramadhani (37), alizaliwa katika Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi, mkoa Kilimanjaro t
arehe 23 Machi 1977.
Alianza elimu ya msingi mwaka 1984 na kuhitimu mwaka 1990 katika shule ya msingi Korongoni iliyopo Manispaa ya Moshi.
Mwaka 1991 aliingia kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Mlite iliyopo wilayani Rombo mkoni humu.
Hata hivyo hakufanikiwa kuhitimu elimu ya sekondari kwani mwaka 1992 alifukuzwa shuleni hapo kutokana na utovu wa nidhamu.
Baada ya hapo ajitupa katika shule ya ufundi na udereva mjini Moshi akisomea masuala ya ufundi makenika katika gereji moja ambako alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika fani hiyo.
Wakati akiendelea na mafunzo ya ufundi na udereva, Alibaba alijitumbukiza katika michezo mbalimbali ikiwemo utunishaji wa misuli kwa wanaume ambapo mwaka 1998 alishiriki shindano la kumtafuta Mr. Kilimanjaro na kumaliza nafasi ya 5.
Akiwa katika michezo mbalimbali ikiwemo kurusha tufe, mpira wa kikapu mwaka 1999 alikutana na Mwalimu Yasint ambaye alimshauri atinge CCP kwa ajili ya masumbwi.
Ndipo Oktoba 1999 alipoanza mazoezi makali, ilipofika Desemba 1999 alifuzu kushiriki michuano ya masumbwi kwa timu za majeshi yaliyofanyika CCP mjini Moshi na kuishia Nusu fainali.
Mpambano anaoukumbuka ni ule aliomchana sehemu ya jicho bondia Stanley Ernest katika raundi ya nne, hivyo kushinda kwa TKO hii ilikuwa mwaka 2000 na kutwaa mkanda wa mkoa.
Pia amewahi kupambana na Joshua Onyango mzaliwa wa Kenya anayeishi Marekani hii ilikuwa mwaka 2008, pambano hilo la kirafiki lilivunjika katika raundi ya tano.
Mwaka 2014 amepambana na Erick Mwenda katika ubingwa wa UBO-Africa raundi 10 na kumtwanga kwa pointi katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Alibaba amepambana mapambano 22 akitoka sare pambano moja tu mengine akifanya vizuri.
BONDIA WA KIMATAIFA KIVUTIO
Akizungumza Alibaba alisema bondia Floyd Mayweather (37) wa nchini Marekani ndiye anayemvutia zaidi na hujisikia vizuri akimwona akishinda mapambano yake, hasa ikizingatiwa kwamba majuma machache yaliyopita amemtusua Muargentina Marcos Maidana.
KUELEKEA PAMBANO DHIDI YA THOMAS MASHALI
Wakali hawa watakuwa wakiwania mkanda wa kimataifa wa UBO uzito wa kilogramu 72 “lightmiddleweight”.
Viunga vya mji wa Tanga vitarindima vigelegele na vifijo pale mabondia Ali Baba na Thomas Mashali watakapopanda ulingoni.
WITO KWA MABONDIA MAPROMOTA
Alibaba aliwataka mabondia wenzake  kufanya mazoezi na kuacha starehe na kujikita kufanya mazoezi kwa bidii zote ili kuurudisha mchezo huu kwenye zama zake.
Pia aliongeza kusema wanamasumbwi za zamani na wa kizazi cha sasa kuna utofauti mkubwa sana ikiwemo kupunguzwa kwa raundi kutoka 15 hadi kuwa chini ya 12 kutokana na wengi wao kukosa chakula cha kutosha na kujikita katika starehe badala ya mazoezi.
Hata hivyo Alibaba anayenolewa na Kocha Pascal Bruno kutoka Nairobi aliwataka mapromota wa mchezo kuacha tamaa ya fedha na badala yake wajikite kuwasaidia mabondia wao hali ambayo itaongeza hamasa kwa chipukizi.
WITO KWA SERIKALI
Aidha bondia huyo aliitaka serikali kuangazia mikoani na sio Dar es Salaam pekee kwani mikoani kuna wengi wenye uwezo wa kutosha hivyo mazingira yakiboreshwa yatasaidia kuinua mchezo huo kimataifa na kuachana na tabia ya kuwa wasindikizaji michuano mbalimbali.
Alibaba alihitimisha kwa kuwataka wakazi na wadau wa mkoa wa Kilimanjaro kuachana na dhana ya michezo hailipi na badala yake wawekeze katika m
chezo wa masumbwi badala ya kujikita katika masuala yasiyo ya kimichezo ili kuendeleza masumbwi.
Imetayarishwa na Jabir Johnson, barua pepe:jaizmela2010@gmail.com, cell: 0768 096 793

Mh. Lowassa amkaribisha Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh.  Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo jana Jumapili Septemba  28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya  kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.
Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha  Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni  kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli,Bw. Twalib  Mbasha.
Balozi wa Japan nchini,Mh. Masaki Okada (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha (kulia) na Meneja wa  Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema alikofikia balozi huyo na 
ujumbe wake katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo.

Mke wa Waziri Mkuu achangisha Milioni 128 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jijini Dar


Mke wa Waziri Mkuu,MamaTunu Pinda akipokea kiasi cha dola elfu moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko utafiti na huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB,Tully Esther Mwampamba kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la kiinjili Moroviani Tanzania (KKMT) Mburahati jijini Dar es salaam.kulia ni Askofu David Martin Mwalyambile wa kanisa hilo Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.Picha na Chris Mfinanga
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akimshukuru mtoto Cecylia Mashaka Mwaisaka mwenye umri wa miaka mitatu kwakuchangia shilingi elfu ishirini kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Moroviani mburahati jijini Dar es salaam.Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.
Kwaya ya kanisa la Moroviani Mburahati ikitumbuiza katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa lao.
Picha ya pamoja.

Sunday, September 28, 2014

NASSIBU RAMADHANI ADROO NA MOHAMED MATUMLA





Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana point Picha na SUPER D BLOG

Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana point Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fatuma Yazidu wakati wa mpambano wao Yazidu alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Lulu Kayage akilalamikia matokeo ya kupigwa na Fatuma Yazidu kulia ni bondia Ibrahimi Class 'King Class Mawe' Picha na SUPER D BLOG
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo pamoja na mashabiki mbalimbali
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo
 
Mabondia Juma Bigilee kushoto,Ibrahimu Class ; King Class Mawe' na Rashidi Mhamila wakiwa katika pozi baada ya mchezo kwumalizika

SIMBA YATOSHANA NGUVU YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA POLISI MOROGORO


Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ramadhani Singano 'Messi'
Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. 
 Okwi akiipangua ngome ya Polisi Moro.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Polisi Morogoro, Lulanga Mapunda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


 Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe akiwa katikati ya wachezaji wa Polisi Morogoro,  Lulanga Mapunda (kushoto) na golikipa wa timu hiyo, Abdul Ibad  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe akiwa katikati ya wachezaji wa Polisi Morogoro,  Lulanga Mapunda (kushoto) na golikipa wa timu hiyo, Abdul Ibad  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kipa wa Polisi Moro akipata matibabu baada ya kuuimia.Picha na Francis Dande,Globu ya Jamii.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...