Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 28, 2016

TUNAITAJI UKUMBI BORA WA MCHEZO WA MASUMBWI TANZANIA

Kocha wa Kimastaifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhaila 'Super D' kushoto akimnowa bondia bingwa wa Afrika wa U.B.O nA wpbf Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati akijiandaa na mpsmbano wake wa kimataifa
NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.

Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.

Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
Mchezo wa ngumi katika nchi yetu ya Tanzania unazidi kushika kasi kutokana na kuchipukia kwa mabondia wengi na mapromota ambao wanapigana katika kuwania mataji mbalimbali nje na ndani ya Tanzania na kuandaa mapambano . wapo mabondia wengi katika historia ya Tanzania ambao wamewahi kupigana nje ya nchi hukiwauliza kuhusu ubora wa mchezo wa ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo ndani ya nchi yetu ni imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami kuwa bado unahitaji vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo .
Kwa Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje ya Tanzania kama Stanley Mabesi 'Ninja' Joseph Marwa, Rashid Matumla, Rogers mtagwa ,Habibu Kinyogoli Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi na ni mwanaharakati wa mchezo uho kwa nyanja zote kwa sasa na Emanuel Mlundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo huo.
 jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa kumbi bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini nimeona nijaribu kulitilia mkazo .
Natoa mfano kama tulivyo weza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil Ivory Coast  na nyingine basi hata mchezo wa ngumi linawezekana ukitazama kama marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea kumbuka silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya kuboresha.
Kwa Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST,TPBC,TPBO,KBF bila kusahau kile cha taifa cha BFT lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo ya mazoezi na kumbi za kupigania vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa mchezo huo kwa Tanzania kwakuwa serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa mpira wa miguu ambao hata mchezo wa kufukuza upepo Riada wanafaidika nao halikadharika wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki bila shaka mchezo wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea mchezo huo kama ilivyo Las Vegas Nevada na MGM Grand au Madson square ni dhahiri inawezakana kwa Tanzania kuwa na kumbi bora ya kisasa na imani vyama vya mchezo wa ngumi vyote nchini vinaweza kukaa chini na kujadiliana na serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha tunapata kumbi bora ya kisasa ya kupigania ili kuongezea ujuzi na viwango vya mchezo wa ngumi kwa Tanzania.
Kama Ufilipino imeweza kutoa bingwa wa dunia hata Tanzania inaweza pia kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndio mchezo pekee ambao unakuja kwa kasi pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Nina maliza kwa kusema kuwa ni imani yangu kuwa kwa kujengwa uwanja huo kutawapa mabondia wa tanzania kujiaamini na kuupanua mchezo huo na unaweza pia kulitangaza jina la Tanzania katika Nyanja za utalii ndani na nje ya Tanzania kama inavyowezekana kuleta mastaa wakubwa wa muziki kutoka ulaya na amerika ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa Tanzania .
Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Floyd Mayweather, akifuatiwa na Manny Paquaio  mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.

Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya tano,
nina mengi ya kuongelea kuhusu mchezo wa masumbwi hila kwa leo naomba nishie hapo
Na: Super D Boxing Coach www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255713 406938
Po.Box. 15493

Dar es Salaam Tanzania

TUNAITAJI UKUMBI BORA WA MCHEZO WA MASUMBWI ANZANIA

MADA MAUGO APIGWA T.K.O YA RAUNDI YA TATU WENZAKE WOTE WAKITOKA DROO

Bondia Pus Kazaula kushoto akimrushia kunde la mkono wa kushoto mpinzani wake Seba Temba wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam mpambano uho walitoka droo Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA PIUS KAZAULA WA PILI KUSHOTO AKIWA NA MPINZANI WAKE SEBA TEMBA

REFARII WA MPAMBANO WA MASUMBWI SAID CHAKU AKIWAINUA MIKONO JUU MAONDIA PIUS KAZAULA KUSHOTO NA SEBA TEMBA BAADA YA MPAMBANO WAO KUMALIZIKA KWA DROO Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia mohamed Matumla kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano uho ulisha kwa droo  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Mada Maugo kioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdallah Pazi wakai wa mpambano wao Pazi alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu wakati wa mpambano wao uliofanyika uwanja wa ndani wa Taifa  
Mabondia Nassibu Ramadhani kushoto akionshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao wa raundi nane uliofanyika katika uwanja wa ndani wa taifa siku ya jumapili ya psaka mpambano uho ulisha kwa maamuzi ya droo Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano waouliofanyika uwanja wea ndani wa taifa Dar es salaam mpambano uho ulishaa kwa Droo  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Pus Kazaula kushoto akimrushia kunde la mkono wa kushoto mpinzani wake Seba Temba wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam mpambano uho walitoka droo Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Pus Kazaula kushoto akimrushia kunde la mkono wa kushoto mpinzani wake Seba Temba wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam mpambano uho walitoka droo Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MASHABIKI wapata burudani mashabiki waliofika uwanja wa ndani wa taifa kulikokuwa kunafanyika mchezo wa masumbwi wametoka na furaha tele baada ya kushudia mapambano waliyokuwa wakiyasubili kwa hamu kubwa hapa nchini

akizungumza baada ya kumalizika mpambano uho mratibu wa mapambano hayo Rajabu Mhamili 'Super D' amesema mashabiki wamefuraia mapambano ambayo karibia yote yalimalizika kwa droo

akitaja matokeo ya mapambano hayo amesema bondia Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' alimsambaratisha bondia Mada Maugo kwa T.K.O ya raundi ya tatu wakati Mohamedi Matumla na Cosmas Cheka waritoka droo
wakati Pius Kazaula alitoa Droo na Seba Temba

mpambano mwingine mkali uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi nchini 

kati ya bondia Nassibu Ramadhani na Fransci Miyeyusho nawo pia umemalizika kwa sale 

wakati uhu uhu mabondia Mfaume Mfaume na Ramadhani Shauri wanatarajia kusaini mkataba wa kuzipiga siku y mei mosi katika uwanja uho uho wa taifa

Saturday, March 26, 2016

MABONDIA DULA MBABE/MADA MAUGO/COSMAS CHEKA NA MATUMLA WAPIMA UZITO KUPIGANA J2 YA PASAKA TAIFA

Mabondia Abdalla Pazi 'Dulac Mbabe' kushoto akitambiana na Mada Maugo baada ya kumaliza kupima uzito kwaajili ya mpambano wao wa ubingwa wa UB.O Afrika utakaofanyika jumapili ya pasaka march 27 kesho katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Abdalla Pazi 'Dulac Mbabe' kushoto akitambiana na Mada Maugo baada ya kumaliza kupima uzito kwaajili ya mpambano wao wa ubingwa wa UB.O Afrika utakaofanyika jumapili ya pasaka march 27 kesho katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa katikat ni promota Kaike Siraju Picha na SUPER D BOXING NEWS

abdalla pazzi na mada maugo

ROJAS MASAM AKIPIMWA AFYA

Rojas Massam kushoto akitunishiana misuli na Mwinyi aMzengela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa march 27 uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rojas Massam kushoto akitunishiana misuli na Mwinyi aMzengela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa march 27 uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

SEBA TEMA KUSHOTO NA PIUS KAZAULA

Mabondia Seba Temba kushoto akitunishiana mkisuli na Pius Kazaula baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpasmbano wao kesho march 27 uwanja wa ndani wa taifa  katikati ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
 
MABONDIA wote wanaicheza siku ya jumapili ya pasaka March 27  uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam wamepima uzito wao kwa ajili ya mpambano uho

akizungumzia mpambano uho mratibu wa pambano hilo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayali kwa kuwa wapo na afya tele na wameshapia uzito pamoja na afya zao kwa ajili ya mpambano uho
 
ambapo mabondia mahasimu kg 54.9 Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ule wa mwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe

mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo kg 79 na Abdallah Pazi ambao wametafutana kwa mda mrefu na sasa wamaliza ubishi siku ya jumapili hii ya march 27 katika uwanja wa ndani wa taifa

Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote wamepima uzito pamoja na kuangaliwa afya zao katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni  na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka March 27 uwanja wa ndani wa Taifa

'Super D' aliongeza kwa kusema kuwa mipambano hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuki
 
 kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka mingine bondia  

 Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla
 
Katika mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu

DAWASCO YATOA RAI ONGEZEKO LA MAJI JIJINI

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwako na ongezeko la Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza kufanya majaribio ya uzalishaji wa Maji .

Akiongea na waandishi wa habari kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na pia kumekuwepo na ongezeko la uvujaji wa Maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam, hasa katika maeneo ambayo yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji na baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo (Low pressure)

Kufuatia ongezeko hili la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na uvujaji wa Maji umeongezeka katika maeneo ambayo aidha yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji au maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo Alisema Bi. Lyaro

Aidha, ametoa wito kwa wateja na wananchi wote kutoa taarifa za uvujaji huo wa Maji pindi wanapobaini kuwapo na uvujaji wa Maji katika makazi yao na maeneo mbalimbali ya jiji kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 022194800 au 0800110064 (Bure).

“Namba hizi ziko wazi saa 24 kwa siku na mteja hatakatwa gharama yoyote akipiga simu hizi. Hivyo tunaomba wateja wetu waisaidie Dawasco kupunguza upotevu wa maji kwa kutupa taarifa za mivujo na kupasuka kwa mabomba” alisema bi Lyaro.

Kutokana na ongezeko hilo la Maji maeneo yaliyoanza kupata Maji baada ya majaribio ya mtambo huo kuwa ni Tandale,Manzese makunimula,Mwananyamala,Kinondoni mkwajuni, baadhi ya maeneo ya vingunguti,changombe,ubungo-mabibo na city centre.

Pia, DAWASCO imetumia nafasi hiyo kuwakumbusha wateja wote kulipia huduma ya Maji kwa wakati kwani watu wengi kwa sasa wameanza kupata huduma ya Majisafi na salama kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa Maji katika mtambo wa Maji wa Ruvu chini, hivyo hawana budi kuyalipia ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma ya Maji.

Kuongezeka kwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo  kumetokana na kukamilika upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini ulioanza mwaka 2011 hivyo kuongezeka kiasi cha uzalishaji wa Maji kutoka wastani wa lita milioni 182 hadi lita 270 kwa sasa.

WAGOMBEA USPIKA BUNGE LAWAWAKILISHI ZANZIBAR WAMKATAA KIFICHO

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

HEKAHEKA zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho.

Kificho ni Spika wa Bunge la Wawakilishi kwa muda wamiaka 25 sasa ambapo wanachama wa CCM Zanzibar tayari wameanza kutilia mashaka uamuazi wa spika huyo aliyechukua fomu za kugombea tena akitaka kuendelea na kuongoza kiti cha uspika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, jambo, inalozua maswali mengi yasiyo na majibu.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar, walitoa maoni yao juu ya sakata hilo na kusema kuwa Kificho hakustaili kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kijacho bali alitakiwa kuiga mfano wa baadhi ya viogozi kama Spika Pius Msekwa na wengine walioamua kuachia ngazi kwa kujiuzuru madaraka na kuwaachia vijana wenye hali ya kuongoza ili kupata radha mpya katika Bunge hilo la Wawakilishi.

Naye mgombea, Mahamud Muhamed Mussa, alisema kuwa amejitokeza kuchukua fomu ili kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo alionao na Zaidi akijiandaa kuongoza kisasa Zaidi na kuleta mabadiliko ili Bunge la Wawakilishi liwe lakisasa na kuendana na kaulimbiu ya Mhe Rais wa Jamhuri ya 'Hapa kazi tu', alisemaMussa. 

''Kiukweli Kificho sasa anaelekea kuwaudhi Vijana ambao nao sasa ni muda wao wa kuongoza ili waweze kuchangia mengi waliyonayo ili kuendana na Kasi ya Rais wa awamu ya tano Mhe Dkt. Magufuli, Kificho amekalia kiti cha Spika Bunge la Wawakilishi kwa muda wa miaka 25 sasa ni kwa nini asipumzike na kuwaachia vijana wafanye kazi, sidhani kama bado ana jipya'', alisema Mwanachama mmoja wa CCM aliyejitambulisha kwa jina la Kijeshi.

Aidha Wanachama hao walikwenda mbali Zaidi kwa kukumbushia wakati wa zoezi la Kura ya maoni kuhusu Serikali mbili,ambapo Mhe. Kificho alionekana kwenda kinyume na msimamo wa Chama chake wa Serikali mbili huku yeye akionyesha msimamo wake Zaidi wa kudai Serikali tatu akidai 'eti' ni msimamo wa Baraza la Wawakilishi.

Waliojitokeza kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa, Zuberi Ali Maulid, Muhamde Ali Amhed, Jajh Janeth, Sadifa Juma, David Mwakanjuki, Perera Silmg na Abdallah Wazisi, ambapo mchuano mkali unaonekana kuwa kwa ni kati ya Spika aliyemaliza muda wake akijaribu kutetea kiti chake, Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa na Jaji Janeth Sekihola.

Wagombea wote walifika kuchukua fomu jana Machi 23,2016  na kurejesha jana hiyo hiyo, zoezi la kupitiamajina na kufanya mchujo na kupata majina matatu lilifanyika jana na kuwapata hao wanaochuana.

Monday, March 21, 2016

SUPER D AENDELEA KUWANOWA VIJANA KATIKA MCHEZO WA MASUMBWI

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwafundisha jinsi ya kutupa makonde mabondia Isihaka Lusinde  wa pili kushoto, Castory Manjulungu na Miraji Issa wakati wa mazoezi yao yanayofanyika katika GYM ya Uhuru iliyopo kariakoo Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbi ncgini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwafundisha jinsi ya kutupa makonde mabondia Isihaka Lusinde  kushoto, Castory Manjulungu na  naMiraji Issa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia chipkizi Castory ManjulunguPicha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini akiwasimamia kwa makini mabondia Mohamed Muhuzi kushoto na Yusufu Bahati wakati wakiwa mazoezini Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA KUPIMA UZITO MANGO GARDENI JUMAMOSI KWA AJILI YA KUCHEZA MARCH 27 JUMAPILI YA PASAKA

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA waendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Pasaka march 27 uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam 

akizungumzia mpambano uho mratibu wa pambano hilo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayali kwa kuwa wapo na afya tele na wanaendelea na mazoezi yao ya mwisho mwisho kila mmoja akijitamba kumsambalatisha mwenzake 

ambapo mabondia mahasimu Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ule wa mwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe

mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi ambao wametafutana kwa mda mrefu na sasa wamaliza ubishi siku ya jumapili hii ya march 27 katika uwanja wa ndani wa taifa

Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote watapima uzito siku ya jumamosi pale katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni  na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka Matrch 27 uwanja wa ndani wa Taifa

'Super D' aliongeza kwa kusema kuwa mipambano hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuki
 
 kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka mingine bondia  

 Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla
 
Katika mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu

Sunday, March 13, 2016

NGUMI ZILIVYOPIGWA VIGAE CLASSIC MBAGALA ZAKHEM

Bondia Selemani Galile kulia akimshambulia kwa makonde bondia Ambokile Chusa wakati wa mpambano wao uliofanyika jana jumamosi katika ukumbi wa vigae Classic Mbagala Zakhem mpambano uhuo wa raundi sita ulimalizika kwa droo Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Mwinyi Muhina kulia akipambana na Godfre Sadiq wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa vigae classic mbagala zakhem Sadiq alishinda kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Karage Suba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Pius Kazaula wa Morogoro mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Vigae Classic mbagaa zakhem Kazaula alishinda kwa T.K.O ya raundi ya pili baada ya Suba kusalimu amri kwa kunyoosha mikono juu Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Joseph Sinkala wa Mbeya wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa vigae Classic Mbagala Zakhem Maokola alishinda kwa point mpambano uho  Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Joseph Sinkala wa Mbeya akipokea kipondo kutoka kwa Ibrahimu Maokola wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Vigae Classic Mbagala Zakhem  Maokola alishinda kwa pointPicha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Joseph Sinkala wa Mbeya wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa vigae Classic Mbagala Zakhem Maokola alishinda kwa point mpambano uho  Picha na SUPER D BOXING NEWS

SUPER D KATIKA HARAKATI ZA KUKUZA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KATKA MOJA YA POZI

 RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
SUPER D KATIKA UBORA WAKE

 RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKIWA KATIKA MITAA YAKE YA KUJIDAI UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO DAR ES SALAAM

 RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO AKIWA NA CHAUREMBO PALASA WALIPOKUTANA KATIKA MOJA YA MAPAMBANO YA NGUMI
RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO AKIWA NA CHAUREMBO PALASA WALIPOKUTANA KATIKA MOJA YA MAPAMBANO YA NGUMI

 RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKIWA TAYARI KWA AJILI YA KUREFARII MPAMBANI

RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AKIWA TAYARI KWA AJILI YA KUREFARII MPAMBANI
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...