Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, April 22, 2016

BARIDI BAND YATOA KIBAO IPYA CHA MOLA NILINDE


Na Mwandishi Wetu

KATIKA Band zinazokuja kwa kasi apa nchini moja wapo ni Baridi Band yenye maskani yake Chanika Dar Es Salaam bendi hiyo inayokuja kwa kasi ya juu imekuwa gumzo kw sasa

Baada ya kutoa kibao chake kipya kabisa cha 'Mola Nilinde' inayotamba akizungumza wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi  wa Baridi Bandi  King Nayowe
Amesema bendi yao ilianza mwaka Desemba 2014 ikiwa na wanamuziki 13 imekuwa ikifanya maonesho mbalimbali Chanika na vitongoji vyake kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi hawo

pia imesha rekodi nyimbo mbili na video moja ambayo inatamba katika vituo vya radio na stesheni mbalimbali za luninga 

aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo kuwa ni Saby Ally Orrgan Mwanambeti,Robart Mwanabeti,Yusuph Othumani  Maki hawo ni baadhi yao katika bendi hiyo

mpaka sasa ina nyimbo mpya kazaa ikiwemo tumetoka mbali, Dunia na Mola nirinde

bendi hiyo imesajiliwa kwa usajili wake katika baraza la sanaa la Taifa kwa ajili ya kufanya shughuli za Sanaa na kutoa burudani mbalimbali za mziki wa Dansi

NYIMBO MPYA WALE WALE

Jina la wimbo - WALE WALE
jina la msanii- SPIZZY KWANZA FT RAN P
Producer - SPIZZY KWANZA
Studio - MP RECORD

BARIDI BAND YATOA KIBAO IPYA CHA MOLA NILINDE

Na Mwandishi Wetu

KATIKA Band zinazokuja kwa kasi apa nchini moja wapo ni Baridi Band yenye maskani yake Chanika Dar Es Salaam bendi hiyo inayokuja kwa kasi ya juu imekuwa gumzo kw sasa

Baada ya kutoa kibao chake kipya kabisa cha 'Mola Nilinde' inayotamba akizungumza wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi  wa Baridi Bandi  King Nayowe

Amesema bendi yao ilianza mwaka Desemba 2014 ikiwa na wanamuziki 13 imekuwa ikifanya maonesho mbalimbali Chanika na vitongoji vyake kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi hawo

pia imesha rekodi nyimbo mbili na video moja ambayo inatamba katika vituo vya radio na stesheni mbalimbali za luninga 

aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo kuwa ni Saby Ally Orrgan Mwanambeti,Robart Mwanabeti,Yusuph Othumani  Maki hawo ni baadhi yao katika bendi hiyo

mpaka sasa ina nyimbo mpya kazaa ikiwemo tumetoka mbali, Dunia na Mola nirinde

bendi hiyo imesajiliwa kwa usajili wake katika baraza la sanaa la Taifa kwa ajili ya kufanya shughuli za Sanaa na kutoa burudani mbalimbali za mziki wa Dansi










MABONDIA WA TANZANIA WATAMBA KUWASAMBALATISHA WAGENI


Mabondia watakaocheza katika mpambano wa kimataifa mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa kutoka kushoto ni  Abdallah Pazi  Fransic Miyeyusho, Thomas Mashali, Lulu Kayage na Swalehe Mkalekwa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia watakaocheza katika mpambano wa kimataifa mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa wakionesha mshikamano wao wakati wa kutambulisha mpmbano uho kutoka kushoto ni  Abdallah Pazi  Fransic Miyeyusho, Thomas Mashali, Lulu Kayage na Swalehe Mkalekwa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Antony Ruta akizungumza na wanahabari

BONDIA THOMAS MASHALI AKIZUNUMZIA MPAMBANO WAKE

LULU KAYAGE AKIONGEA KUHUSU MPAMBANO WAKE


Mabondia watakaocheza katika mpambano wa kimataifa mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa kutoka kushoto ni  Abdallah Pazi  Fransic Miyeyusho, Thomas Mashali, Lulu Kayage na Swalehe Mkalekwa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia watakaocheza katika mpambano wa kimataifa mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa kutoka kushoto ni  Abdallah Pazi  Fransic Miyeyusho, Thomas Mashali, Lulu Kayage na Swalehe Mkalekwa na mratibu Anton Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mratibu wa mpambano wa kimataifa Anton Rutta akizungumzia mpambano uho nyuma akiwa na mabondia watakaocheza Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mratibu wa mpambano wa kimataifa Anton Rutta akizungumzia mpambano uho nyuma akiwa na mabondia watakaocheza Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

HOMA ya mpambano wa kimataifa umezidi kupamba mota baada ya leo kukutanishwa mabondia wote  wa Tanzania watakaocheza na wa nje kuongea na wahandishi wa habari

akizungumza katika mkutano na waandihi wa habari mlatibu wa mpambano uho Anton Rutta amesema mabondia wote wapo safi kwa ajili ya mpambano uho wa kimataifa ambapo bondia

Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' atakuwa anagombea ubingwa wa dunia mkanda wa U.B.O na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani'

Wakati mapambano mengine ya kimataifa yatawakutanisha mabondia 
 
 Mwanadada Lulu Kayage atakaezichapa na Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi  wengine ni Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda Abdalla Pazi 'Dula Mbabe' atavaana na  Chamunorwa Gonorenda kutoka Zimbabwe
mapambano mengini ya kitaifa yatawakutanisha  Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola


mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga

siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi



siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo

Thursday, April 21, 2016

BONDIA ABDALLAH PAZI KUENDELEZA UBABE KWA KUWAPIGA MABONDIA KWA K.O


Na Mwandishi Wetu

Bondia Abdalla Pazi 'Dula Mbabe' baada kumsambalatisha Mada Maugo kwa TKO ya raundi ya tatu mpambano uliopita uliofanyika jumapili ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa

sasa ameingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake mwingine wa kimataifa utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya mei 14

Akimkabili bondia Chamunorwa Gonorenda kutoka Zimbabwe bondia Pazi  amesema kuwa yeye ni tingatinga la kuchonga barabara hivyo achagui bondia wa kucheza nae aliongeza kwa kusema kuwa vichapo vyangu vinaeleweka kuwa mabondia wote ninaokutana nao awamalizi raundi  nilianza hivyo china nikampiga bondia raundi ya nne nikaja bongo nikampiga K,O mbaya sana bondia Baraka Mwakansope

 Baada ya hapo nikapambana na Mada Maugo ambaye kwa sasa ataki ata kuniona na akisikia jina la Dula Mbabe anakaa kimyaaa hivyo nataka niendeleze rekodi yangu hii na sito waangusha mashabiki zangu

katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mbalimbali ya kimataifa itawakaokutanisha na mabondia wa Tanzania na wa nchi nyingine mbalimbali

ambapo Thomas Mashali atakuwa akigombania ubingwa wa Dunia wa W.B.O akipambana na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani' 

mapambano mengine ya kimataifa yatawakuanisha bondia mwanadada Lulu Kayage na Chiedza Homakoma 'Nikita' Malawi mabondia wengine ni  Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi  wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya  na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda



mapambano mengini ni kati ya Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola



mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga




siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi



siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo
No comments:

BONDIA WA KIKE LULU KAYAGE AHAPA KUFIA URINGONI KATIKA MPAMBANO WAKE MEI 14 TAIFA


BONDIA CHIEDZA HOMAKOMA 'NIKITA' MALAWI  LULU KAYAGE TANZANIA

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Lulu Kayage yupo katika mazoezi mazito na makali kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake wa kimataifa na Chiedza Homakoma 'Nikita' Malawi mpambano utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani wa Taifa 

akizungumza wakati wa mazoezi yake anayofanya kinondoni msisiri amesema anajiandaa vizuri tu kwa ajili ya kumkabili mmalawi huyo atakaepigana nae 

aliongeza kwa kusema unajuarekodi yangu imearibika kidogo kwa kuwa nilipigwa kwa point mpambano wangu wa mwisho

hivyo sasa nimejipanga vizuri kuakikisha nafanya vema katika mpambano uho wa kimataifa nawa aidi mashabiki wagu kuwa siku hiyo nitakuwa radhi nifie uringoni ili ushindi ubaki Tanzania na siwezi kupigwa hapa nchini na nikatia aibu Taifa langu

siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi nchini

ambapobondia Thomas Mashali atakumbana na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani'  ubingwa wa Dunia mkanda wa U.B.O 

mapambano mengine ya kimataifa yatawakuanisha bondia Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi  wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya  na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya na Fransic Miyeyusho atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda

mapambano mengini ni kati ya Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola

mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga




siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba shiria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo

Tigo wakabidhi madawati 400 katika shule nane za Wilaya ya Mwanga







Inline image 2

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki(Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mwanga Theresia Msuya(katikati) Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.


Aprili 20 2016 Mwanga: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa shule nane za msingi katika manispaa ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi Reli Juu katika manispaa ya Mwanga, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Lugata.

Lugata amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro  na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Kilimanjaro. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Sadiki

Madawati hayo yametolewa kwa shule za msingi  nane kama ifuatavo, Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru,Kiboriloni, Lawate na Reli Juu

Saturday, April 16, 2016

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ASHINDA KWA POINT AKIWA NCHINI PANAMA


BONDIA IBRAHIMU CLASS AKIWA NA MIKANDA YAKE YA UBINGWA WA AFRIKA  WPBF JUU NA CHINI NI U.B.O AFRIKA
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na bondia Shane Mosley ambaye alishawai kucheza na Floyd Mayweather na kuonesha upinnzani mkubwa kushoto ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa hapa ni baada ya kushinda mpambano wake na Zapir Rasulov wa Russia kwa point
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na mpinzani wake Zapir Rasulov wa Russia baada ya kumshinda kwa point 

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Mtanzania Bingwa wa Afrika wa mikanda ya WPBF na U.B.O Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe' april 15 mwezi uhuu amefanya maajabu baada ya kumtwanga bila huruma

Bondia 

Zapir Rasulov wa Russia na kufanikiwa kumpiga kwa point katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya

Convenciones Vasco nchini

Panama City, Panama 

 Class anakuwa bondia wa kwanza kumpiga bondia huyo katika mapambano yake 30 aliyocheza ambapo kati ya hayo mapambano 27 ameshinda kwa K.O na matatu kashinda kwa point 

 bondia huyo arikuwa na rekodi ya kutopigwa ata mpambano mmoja ambao aliocheza katika michezo yake yote

Class ameweka dowa katika michezo yake na kuwa bondia wa kwanza kutoka afrika kumpiga bondia huyo anaesifika uku ugaibuni

 Bodia King Class Mawe baada ya kuibuka na ushindi uho amesema ushindi ni wa watanzania wote kwani yeye amekuwa mtumishi wao tangia mpambano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa ubingwa alipokwenda nchini Zambia na ufanikiwa kumdunda bondia Mwansa Kabinga  katika mpambano uliofanyika Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia hii ilikuwa june 8 ,2014  na kushinda kwa TKO ya raundi ya tisa na kufanikiwa kurudi na mkanda wa WPBF Afrika

hivyo natarajia kuendeleza kuitumikia Tanzania na watu wake kupitia mchezo wa masumbwi nchini

bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na kocha mkongwe kabisa Habibu Kinyogoli akisaidiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amekuwa akimshauli katika mapambano yake mblimbali nchini

bondia huyo anataraji kurudi nchini wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya mpambano mwingine wa asumbwi utakaomkabili hivi katibuni

Rais Magufuli afungua rasmi mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (flai ova) eneo la Tazara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua  jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua ramani ya mradi wa barabara ya juu eneo la Tazara kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi huo Tazara Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea maelekezo kuhusu mradi wa barabara za juu eneo la Tazara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale katika ufunguzi rasmi wa mradi huo Jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018.

Sherehe ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida.

Barabara hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.

Barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha upotevu wa shilingi Bilioni 411.55

Rais Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara  ya njia sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano, ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi hospitali ya Agha Khan.

Juhudi nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe.

Aidha, Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika.

Dkt. Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA CHINI YA KOCHA WAKE SUPER D


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu yhamila 'Super D ' Kushoto akimfundisha bondia Vicent Mbilinyi jins ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'Upcut' wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa basketi Shule ya Uhuru wasichana 'Uhuru GYM' Picha na SUPER D BOXING EWS

Bondia Aloyce Kakinda kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea Uhuru GYM kariakoo Dar es salaam
Picha na SUPER D BOXING EWS

VICENT MBILINYI

Bondia Aloyce Kakinda kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea Uhuru GYM kariakoo Dar es salaam
  1. Picha na SUPER D BOXING EWS
Bondia Aloyce Kakinda kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea Uhuru GYM kariakoo Dar es salaam
Picha na SUPER D BOXING EWS

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu yhamila 'Super D ' Kushoto akimfundisha bondia Vicent Mbilinyi jins ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'Upcut' wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa basketi Shule ya Uhuru wasichana 'Uhuru GYM' Picha na SUPER D BOXING EWS

SERIKALI YA KOREA YAGHARAMIA UJENZI WA HOSPITAL YA CHANIKA UTAKAO GHARIMU BILIONI 8.8 ZA KITANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8 za kitanzania.
.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mr Isaya (kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victriana Ludovic na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mr Kim wakiweka jiwe la msingi la Hospitali hiyo.
Meneja wa Mradi huo, Mr Kim akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na ujumbe wake ramani ya majengo ya Hospitali hiyo.Na Dotto Mwaibale
Hutuba na taarifa ya mradi huo zilisomwa.
Balozi wa Korea nchini Geum-young Song (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na balozi wa Korea nchini Geum-young Song wameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo itakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi 4000.

Akizungumza katika hafla ya kuweka jiwe hilo la msingi Chanika jijini Dar es Salaam jana, Makonda aliishukuru serikali ya Korea kwa msaada wa ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo itawasaidia wananchi wa Chanika na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Amana.

"Tunawashukuru hawa ndugu zetu wa Korea Kusini kwa msaada wa kutujengea Hospitali hii nawaombeni wananchi kuitunza ili kila mtakapokuwa mnafika kutibiwa tuwakumbuke wakorea" alisema Makonda.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victorina Ludovic alisema ujenzi wa Hospitali hiyo utasaidia kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi wapatao 398,882 kutoka maeneo ya Chanika, Msongola, Zingiziwa na Majohe hivyo kupunguza muda na gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitumia kufuata huduma hizo umbali wa kilometa 30 kwenda hospitali ya Amana ya Rufaa.

Ludovic alisema ujenzi wa mradi huo hadi utakapokamilika utagharimu dola la milioni 4 sawa na sh.bilioni 8.8 za kitanzania.Balozi wa Korea nchini , Geum-young Song amesema wakorea hawafurahishwi wanapoona mama na mtoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua nchini Tanzania.

"Nchi yetu kupitia shirika la Koica imeamua kujitolea kujenga hospitali hii ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania kupata huduma bora ya afya ya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwani hatupendi kuona wanapoteza maisha wakati wa kujifungua" alisema Young Song.

Balozi huyo aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi ya Korea katika shughuli mbalimbali jambo linaloimarisha uhusiano baina ya wananchi wa nchi hizo.

DART YAHIMIZWA KUELIMISHA WAKAZI WA DAR

ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya mradi wa mabasi yaendayo kasi kuanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
“Katika kipindi hiki cha majaribio, ambacho madereva wameanza kutumia barabara za BRT, hakikisheni mnatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu namna ya kuvuka barabara, kuzuia wenye bodaboda kutumia barabara hizo kuelezea na matumizi ya taa za barabarani kwa madereva wote,” amesema.
Ametoa agizo hilo jana usiku (Ijumaa, Aprili 15, 2016) wakati akizungumza na wakuu wa taaasisi, watendaji wakuu na wadau wa mradi huo kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu aliwataka watendaji wa wakuu wa taasisi wahakikishe wanapanua wigo na kutumia vyombo vya habari vingi kadri iwezekanavyo pamoja na mitandao ya kijamii katika kuelimisha raia juu ya zoezi hilo.
Akifafanua kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale alisema miundombinu kwa ajili ya mradi huo imekamilika na usafiri huo utaanza hivi karibuni.
Mhandisi huyo ametumia fursa huyo kutoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya barabara hizo kwa sababu imeigharimu Serikali fedha nyingi.
Naye Mrakibu wa Polisi (SP), John Shawa kutoka Makao Mkuu ya Trafiki alisema kuanzia kesho zoezi la majaribio kwa mabasi yaendayo haraka litaanza hivyo amewaomba wananchi kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
"Kuanzia kesho linapoanza zoezi la majaribio kwa mabasi yaendayo haraka ni vema watu wakatumia vizuri barabara hasa madereva wa bodaboda na madereva wengine watambue kuwa hawaruhusiwi kupita katika barabara hizo," alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAMOSI, APRILI 16, 2016.

HAKUNA MUDA WA KULALA, WAZIRI MKUU AIAMBIA DART

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaambia watendaji na wadau wa mradi Mabasi Yaendayo Haraka wa jijini Dar es Salaam (BRT) kuwa hawana muda wa kulala wa kupumzika na akawataka wakamilisha haraka vipengele vichache vilivyobakia ili mradi huo uweze kuanza kazi mapema iwezekanavyo. 

Ametoa agizo hilo jana usiku (Ijumaa, Aprili 15, 2016) wakati akizungumza na wakuu wa taaasisi, watendaji wakuu na wadau wa mradi huo kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. 

“Watu wa DART, UDA-RT hakuna muda wa kulala tena. Nanyi wa eGA, MAXCOM, POLISI NA SUMATRA inabidi mfanye kazi kama timu moja na wenzenu ili maeneo yaliyobakia yaweze kukamilika katika muda mfupi na kikubwa ni kuhakikisha mnatoa elimu ya kutosha,” alisisitiza. 

Akielezea utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare amesema miundombinu ya mradi huo imekamilika na utoaji huduma unatarajiwa kuanza hivi karibuni kwani hivi sasa wanamalizia ufungaji wa mfumo wa ukusanyaji nauli na uendeshaji wa mabasi hayo. Pia aliwatka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo na kuwa makini na matumizi ya barabara wakati mradi huo ukiwa kwenye majaribio na hatimaye kuanza kazi rasmi. 

Alisema watakuwa na karakana itakayotumika kwa ajili ya hayo mabasi ambayo itakuwepo eneo la Jangwani na kwamba ofisi za mradi pia zitakuwa eneo hilo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UDA Rapid Transit (UDA-RT), Bw. Robert Kisena amesema mpango wa kuanza kwa mradi huo umekamilila na tayari mabasi yote yamelipiwa kodi pamoja na bima. UDA-RT ni kampuni ya muunganiko wa UDA na wamiliki wa daladala ya kutoa huduma ya usafiri katika miundombinu ya mabasi yaendayo haraka. 

Bw. Kisena amesema kesho wataanza majaribio ya mradi huo kwa kutumia mabasi 10 na watakuwa wanaongeza mabasi 10 kila siku hadi yafikie 50 hivyo amewataka wananchi kuondoa shaka juu ya mradi huo. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom Africa, Bw. Juma Rajab amesema mabasi hayo yatakuwa yanatumia kadi za kielektroniki zitakazokuwa zinalipiwa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu za mkononi. 

Bw. Rajab amesema Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba fedha za mteja zitakuwa salama na hata kama atakapopoteza kadi yake. “Mtu akinunua kadi yake anapaswa atunze namba ya usajili iliyoko kwenye kadi hiyo kwani itatumika kurudishia fedha zake kupitia namba yake ya simu ya mkononi,” alisema. 

Amesema Maxcom Africa ndio wakusanyaji wa nauli kwa kushirikiana na UDA-RT ambapo watatumia mawakala wa MaxMalipo hivyo kila mwananchi atapata fursa ya kununua kadi yake kwa urahisi. Alisema taarifa za kila mtumiaji zitaunganishwa na simu yake ya mkononi ambapo mhusika ataweza kujua kwa urahisi salio la fedha lililomo kwenye kadi yake. 


IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU 
2 MTAA WA MAGOGONI, 
S. L. P. 3021, 
11410 DAR ES SALAAM 
JUMAMOSI, APRILI 16, 2016.

Viongozi wa ndondi 'mwisho wa ubaya aibu'


Mwandishi wetu
KILA mwanadamu anapoamua kufanya kazi ya aina fulani lengo na
hitaji lake ni kuhakikisha anapata mafanikio yatakayomuwezesha
kuendesha maisha yake kama watu wengine.
Hivyo ili kufikia mafanikio hayo nidhamu, upendo, elimu na
kujitabua ni mambo ambayo yanahitajika kuhakikisha malengo
yanafikiwa kwa asilimia mia moja.
Kwa maana nidhamu ikizingatiwa kuanzia katika mazoezi hadi
kwenye ulingo hakika kila kitu kitakwenda sawa na hakika hiyo ndio
mwanzo wa kufanikiwa katika mchezo huo.
Ndio maana kwa mabondia walioanzia katika hatua za awali
'Amature' mara zote wanakuwa na nidhamu kubwa katika maisha yao
katika mchezo huo na kuwa mfano kwa wengine.
Kitendo cha kufanya vema katika nidhamu ndio inayofanya viongozi
wa mchezo huo kuhamasisha vijana wanaotaka kuingia katika
masumbwi kuanzia kwenye hatua hiyo.
Pindi bondia atakuwa na nidhamu ya kutosha itafanya kuhamasisha
upendo katika familia ya wanamasumbwi nchi na upo uwezekano
mabondia wakawa wamoja katika kufuatilia  mambo yao.
Katika kipindi cha hivi karibuni mchezo wa masumbwi unaonekana
kupoteza radha yake kutokana na kuonekana kuwa kuingiliwa na
baadhi ya wajanja ambao wanaonekana kutaka kuwagawa
wanamasumbwi.
Wajanja hao wamekuja na vyama vyao na kujipa majina ya kila aina
likiwemo la urais wa chombo husika huku wakionekana wazi
kutafuta maslahi yao zaidi kuliko wanamasumbwi ambao wamekuwa
wakiharibu akili zao kwa ajili ya mchezo huo huku mafanikio yakiwa
kiduchu.
Kibaya zaidi hakuna chombo makini cha kuangalia na kufuatilia haki
za wanamasumbwi, kingine wanamasumbwi wengi elimu na ufahamu
wa kudai haki yao imekuwa ni tatizo hali ambayo inasababisha
mabondia kugonganishwa vichwa na wanaojihita marais wa vyombo
hivyo.
karibuni  mwaka huu wakati nikiwa katika daladala nikitokea nyumbani
kwenda ofisini, kituo kimoja cha redio kilikuwa kikifanya mahojiano
na bondia Japhet Kaseba majiahano ambao yalionekana kurekodiwa
siku chache zilizopita.
Hakika Kaseba alisikika akizungumza kwa uchungu namna baadhi ya
mabondia wanavyotumiwa vibaya na baadhi ya viongozi huku
akisema wengi wamekuwa wakipandikizwa chuki dhidi ya mabondia
wengine.
Pia wako tayari kufanya hila ili kutengenezewa rekodi ya mapambano
pindi wanapopanda ulingo hali ambayo mwisho wa siku wanafanya
vibaya katika mapambano yao ya kimataifa na ndipo msemo wa
kiswahili unaosema mwisho wa ubaya ni aibu unapotimia.
Nikinukuu katika mazungumzo hayo, Kaseba anasema kuwa baadhi
ya mabondia wanatumika vibaya kwa kujazwa chuki na wakati
mwingine kwa kupanga matokeo kutokana na shida walizonazo.
Pia hata wale ambao haki zao zinaminywa wanashindwa kujitetea
kutokana na elimu yao kuwa ndogo ingawa hakuweza kutoa
suluhisho ya nini kifanyike ili kuondokana na changamoto hiyo.
Kwa akili ya haraka ni dhahiri kuwa kinachotakiwa ni kwamba kwa
sasa ni kila bondia kutambua ameingia katika mchezo huo kwa ajili
gani hali ambayo itasaidia kupunguza changamoto kwa baadhi yao
kuwa mamluki wa viongozi wa baadhi ya vyama.
Pia itasaidia mabondia kuwa kitu kimoja katika kusaka mafanikio yao
kupitia mchezo huo unaonekana kuwa na changamoto lukuki hali
ambayo inaonekana kupoteza radha na mafanikio yaliyokuwa
yakipatikana miaka kadhaa iliyopita.
Kinachotakiwa kwa sasa ni mabondia kujitahidi kuwa kitu kimoja hali
ambayo itasaidia kuwa na nguvu moja ya kudai haki zao pindi
zinapopindishwa kwa maslahi ya wengine

Wednesday, April 6, 2016

SALIM MPONDA AIBUKA BINGWA WA NGUMI ZA WATOTO ILALA


Kocha wa mchezo wa ngumi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kushoto akimkabidhi tunzo bondia bingwa wa watoto Salim Mponda baada ya kumtwanga  Hemed Mrema wengine wa pili kushto ni bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kocha  Juma Mwalimu na Dickson  Tembo Picha na SUPER D BOXING NEWS



 Bondia Salim Mponda kushoto akioneshana umwamba wa kuitupiana makonde na Hemed Mrema wakati wapambano wao uliofanyika juzi katika uwanja wa club ya bar ya wazee ilala Dar es salaam Mponda alishinda kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
MPONDA NA MREMA WAKISALIMIANA KABLA YA KUMALIZA MPAMBANO WAO


MABONDIA SALIM MPONDA NA HEMED MREMA BAADA YA KUPOKEA ZAWADI ZAO
HEMED MREMA AKIZUNGUMZA BAADA YA KUCHUKUA NAFASI A PILI
Mabondia said Ligila na Fadhili Boika wkati wa mpambano wao uliofasnyika katika uwanja wa club ya bar ya wazee ilala bungoni
MABONDIA WA ZANZIBAR

fadhili boika kushoto akioneshana umwamba na said ligila
KIONGOZI WA MCHEZO WA MASUMBWI ZANZIBAR AKIMPATIA ZAADI BONDIA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...