Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi.
Stella Vuzo akiwa katika moja ya darasa na baadhi ya wanafunzi wa shule
hiyo ambao mpaka leo wana uhaba wa madawati hivyo kulazimika kukaa chini
wakati wa kusoma.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Tandale wakibanana katika dawati moja mithili ya
abiria ndani ya Dalala huku tukitegemea kuboreka kwa kiwango cha elimu
nchini.
Masoud Ramadhani wa Ubalozi wa Afrika Kusini akiosha moja ya Vyoo vya shule hiyo.
Balozi
wa Afrika Kusini nchini Mh. Henry Chiliza akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo katika shule ya Msingi ya Tandale ambapo
amesisitiza siku hii ya Kimataifa ya Mandela inaadhimishwa kwa kufanya
shughuli za kijamii kwa kuwa Mzee Mandela mwenyewe alikuwa akijitolea
muda wake mwingi kusaidia watoto, kufanya shughuli za kijamii, kutetea
haki za watoto na wanyonge.
Pichani
Juu na Chini Balozi wa Afrika Kusini nchini Mh. Henry Chiliza
akikabidhi msaada wa uliotolewa na UN kwa Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule
hiyo Lucy Mwakibete huku wakishuhudiwa na wafanyakazi wa UN, Ubalozi,
Walimu na wanafunzi.
Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy Mwakibete (katikati)
akitoa shukrani kwa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini ambapo
ameelezea changamoto mbalimbali zinazoikabili shule zikiwemo Uhaba wa
Madawati, Vyoo, Ubovu wa Sakafu za Vyumba vya Madarasa na kuwaomba wadau
kujitokeza kuwasaidia ili kuboresha mazingira mazuri kwa wanafunzi wa
shule hiyo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kutoka
kushoto ni Kansela wa Masuala ya Siasa Bw. Terry Govender na Joymery
Von De Merwe kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini wakiwa kwenye picha ya
pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy
Mwakibete.
No comments:
Post a Comment