Thursday, September 30, 2010

ZANA ZA KAMPUNI YA RELI ZAHUJUMIWA


VIFUNGASHIO vya reli VILIVYOIBWA


Muhandisi wa Kampuni ya reli Tanzania TRL Bw. Abdallah Hawai (katikati) akiwapatia mahelezo wahandishi wa habari Dar es salaam leo ya kitendo cha hujuma dhidi ya zana za Kampuni hiyo ikiwemo kutolewa kwa vifungashio vya reli

Wednesday, September 29, 2010

MISS TANZANIA KUONDOKA KESHO


MKUTANO Mkuu wa Tisa wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), umemchagua Easther Mkwizu akimkabidhi bendera ya taifa Vodacom Miss Tanzania Genevieve Emmanuel tayari kwa safari yake ya kwenda nchini China kushiriki mashindano ya dunia ya Urembo yatakayofanyika Oktoba 31,2010.

Mama mzazi wa Miss Tanzania Genevieve wakiwa na aliyekuwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Sekta Binafsi nchini Ester Mkwizu na baba yake Emmanuel Mpangala.
Vodacom Miss Tanzania 2010 Ginevieve Emmanuel ametakiwa kulinda heshima yake pamoja na nchi yake awapo katika mashindano ya Miss World kwa kuwa amepewa dhamana ya kuibeba nchi na Amani ya Tanzania.

Nasaha hizo zimetolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Sekta binafsi, Ester Mkwizu wakati akimkabidhi bendera ya Taifa mrembo huyo tayari kwa safari ya kuelekea China kwenye mashindano ya Dunia ya Urembo ya 'Miss World'.

Ginevieve anatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini China kwa ajili ya Mashindano ya Miss World yatakayofanyika Oktoba 31 mwaka huu, na kushirikisha zaidi ya warembo 120 kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo jana mrembo huyo aliagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Herman Mwansoko na MKurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Emmanuel Olenaiko pamoja na viongozi mbalimbali.

Ginevieve ametakiwa kuwa jasiri na kupita kifua mbele, mbele ya warembo wengine wote wanaoshiriki mashindano hayo kwa kuwa anavigezo vyote vya kuiwaklisha nchi yake katika mashindano hayo.

"Ginevieve unakwenda kubeba dhamana ya nchi, nenda kifua mbele ukiwa unatoka kwenye nchi ya amani na ulinde heshima yako pamoja na heshima ya nchi yako hapo utafanikiwa, na sisi wanzania tunakuombea dua uweze kutwaa taji la Dunia,"alisema Mkwizu.

Mwenyekiti huyo ameipongeza Kamati ya Miss Tanzania kwa kuendesha mashindano hayo kwa ufanisi mkubwa na kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono kutokana na Sekta hiyo ya Urermbo kuongeza pato la Taifa kupitia masuala ya utalii na kuenzi pia Utamaduni wa Tanzania.

Naye Ginevieve amewataka watanzania kuondoa hofu juu yake na kwamba hatotishika na wapinzani wake kutokana na maandalizi mazuri ya kisaikolojia aliyoyapata kutoka kwa walezi wake wa Kamati ya Miss Tanzania.

"Nawatoa hofu watanzania ingawa nitashindana na warembo zaidi ya 120 kamwe sitatishika nao, nimeandaliwa vizuri kisaikolojia,"alisema Ginevieve.

Alisema kutokana na fursa hiyo na dhamana aliyopewa na Taifa atahakikisha anatangaza vivutio vya Tanzania kupitia kwa warembo wenzie kutoka nchi mbalimbali pamoja na sekta zote zilizopo nchini.

"kupitia upande wa siasa nitaitangaza Tanzania hasa amani iliyopo na fursa hii nitaitumia bila uoga nawaomba tu watanzania waniombee dua kwani ninajiamini na ninaimani taji la Miss World litatua nchini,"alisema Ginevieve.

Mrembo huyo ataondoka leo na ndege ya Qatar air kwa ajili ya kambi ya Miss World itakayoanza Oktoba mosi mwaka huu na safari yake itapitia Mongolia ambapo atakaa kwa muda wa siku tatu na baada ya hapo atakwenda Shangai ambako pia atakaa kwa siku tatu kisha ataelekea China kabla ya kutua Kusini Sanya kwa mashindano hayo.

Mrembo huyo ni wa 17 kushiriki mashindano ya Miss World tangu kuanzishwa kwa mashindano ya Miss Tanzania 1994 ambapo watanzania wanategemea makubwa kutoka kwake kwa kua ameandaliwa vizuri na walezi wake Kamati ya Miss Tanzania.

MSONDO KUVAMIA KUSINI







BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma imeondoka Dar es Salaam leo kwa ziara ya maonesho matano katika mikoa ya kusini kuanzia Sept 29 mwaka huu baada ya kukaa muda mrefu bila kutembelea kanda hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' (PICHANI) alisema ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuitamulisha albamu yao mpya ya Huna Shukrani.

"Tukiwa huko tutafanya kazi ya kuwapa burudan wapenzi wetu watapata nafasi ya kuona mambo mengi yanayohusu bendi yao kama hayo niliyoyasema.," alisema SUPER D

Alisema wataanza ukumbi wa Bwalo la Maendeleo, Kilwa na Hoteli ya Lindi Oktoba mosi ambapo oktoba 2 watakuwa Brantare Hall na oktoba 3 watakuwa katika ukumbi wa Madeko Masasi, Oktoba 4 Nachingwea na 5 watakuwa Nyongoro Hall, Ruangwa.

SUPER D alisema mbali na utambulisho wa albamu hiyo bendi hiyo pia itatoa fursa kwa wapenzi wake wa mikao hiyo kusikia vibao vipya vya Dawa ya deni kulipa na Lipi Jema vilivyoibwa na wasanii mahiri akiwamo Edo Sanga.

MASHINDANO YA MITUBWI 2010 YAZINDULIWA RASMI



Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa mwaka 2010.

Mashindano hayo ya kupiga kasia, ambayo yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah alisema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika. Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa.

Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyikia Jijini Mwanza tarehe 4 Decemba. Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Kigoma tarehe 9 Octoba, Kagera 23 Octoba, Mwanza 13 Novemba, Mara na Ukerewe 27 Octoba.

Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu mbili za wanaume na moja ya wanawake zitakazoshika nafasi za juu katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Msaidizi wa Bia ya Balimi Edith Bebwa alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo:

Ngazi ya Mikoa Fainali Kuu
Wanaume Wanawake Wanaume Wanawake
Mshindi wa kwanza 700,000 500,000 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 550,000 400,000 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 350,000 250,000 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 300,000 200,000 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 200,000 100,000 400,000 200,000

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki. Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ya aina yake.

RIDHIWANI KIKWETE AWAPATANISHA WANA CCM IRINGA


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa
Viajana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani
Kikwete (katikati), akiwatambulisha Monica Mbega (kulia) na
Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi
katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.Monica
ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela
alienguliwa kuwania nafasi hiyo.
Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Monica Mbega (kulia),
akikumbatiana kwa furaha na David Mwakalebela baada ya
kuahidi kuvunja makundi mbele ya Mjumbe wa Kamati ya
Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Viajana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete (kushoto) katika
kikao cha Baraza la UVCCM, Iringa mjini jana. (PICHA NARICHARD MWAIKENDA)

Kila Ijumaa na Jumamosi ni pale Sanaa Pub, usikose mdau....!


Every Fridays and Saturdays at Sanaa Pub Movenpick.
Times Fm Djz...

Dj Spesso,Dj Kobbo & Lil Ommy.
Naija,Kwaito,Ragger,Bongo,Hip&Rnb,Pop,Old School and More.
Entry-5000/=

Come One Come All Yaa!

Deo: Nitatimiza ndoto na kuleta matumaini



VYAMA mbalimbali vya siasa nchini na wagombea wa nafasi za uongozi kwa tiketi ya vyama hivyo, wapo katika kampeni ya kunadi sera na ilani ya vyama vyao kwa wiki ya sita sasa.

Wapiga kura katika maeneo mengi, wamekuwa wakilishwa ahadi za matumaini ya maendeleo na wagombea ili jamii kubwa iweze kuondokana na umaskini walionao.

Lengo la wagombea wengi ni kuhakikisha majimbo yao yanakuwa mfano wa kuigwa dhidi ya mengine. Kazi kubwa inayofanywa na wagombea kwa sasa ni kuwashawishi wapiga kura wachague viongozi bora wenye dhamira ya kuharakisha maendeleo.

Bw. Mushi Deo (40) ni mgombea udiwani Kata ya Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye anasema, dhamira yake ya kuwania nafasi hiyo ni kutimiza ndoto ya matumaini kwa wananchi wa kata hiyo ili kuwa ya mfano.

Katika mahojiano na Majira, Bw. Deo anasema kata hiyo inahitaji kiongozi makini anayeweza kumaliza kero za wananchi zilizodumu muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

“Mwaka 2005 niliwania ubunge wa jimbo lakini kura zangu hazikutosha, mwaka huu nimeamua kushuka ngazi ya chini kwa sababu wananchi wanahitaji mchango wangu ili waweze kutimiza ndoto yao ya kuwa na maisha bora,” alisema.

Anasema jambo ambalo limemsukuma kuwania nafasi hiyo ni kuonesha uwezo wake katika kuwatumikia wananchi kama kijana, kutatua kero zao kwa wakati na kuondoa umaskini uliopo kwa jamii kubwa akitumia elimu aliyonayo, maarifa pamoja na ubunifu kuboresha maisha yao.

Bw. Deo ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Sayansi na Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema pamoja na kata hiyo kukabiliwa na matatizo lukuki, zipo kero sita ambazo atazipa kipaumbele cha kwanza ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Anasema kero hizo zimetokana na uongozi mbaya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo wananchi kukosa huduma muhimu kama maji, barabara, elimu na afya.

Hali hiyo imechangia vijana wengi kujihusisha na vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu ya kukosa ajira za uhakika.

“Kama wananchi watanipa ridhaa ya kuwa diwani wao, nitahakikisha ilani ya chama changu inatekelezwa kwa vitendo ambapo katika sekta ya afya, nitajenga zahanati ya kata ndani ya miaka miwili na kutoa matibabu bure.

“Zahanati hii, itakuwa ikilaza wagonjwa wa kawaida, wanawake wajawazito, watoto, wazee pamoja na kuajiri wataalamu waliobobea katika fani ya huduma za afya,” anasema Bw. Deo na kuongeza kuwa, atahakikisha mapato katika kata yanasimamiwa vizuri ili kuharakisha maendeleo na kukuza uchumi.

Anaongeza kuwa, tatizo la ukosefu wa zahanati ya kata limekuwa likichangia wanawake wengi kufuata huduma Hospitali ya Mwanyamala ambayo haitoi huduma za afya kwa kiwango kinachokidhi mahitaji ya mgonjwa.

Akizungumzia sekta ya maji, Bw. Deo anasema inashangaza kata hiyo kukabiliwa na tatizo sugu la maji safi na salama wakati Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), ina ofisi katika kata hiyo.

Anasema asilimia kubwa ya Watanzania hawapati maji safi na salama lakini pamoja na kilio hicho, watawala ambao wametangulia hawakulipa kipaumbele suala hilo badala yake, wamelipa kisogo na kuwaacha wananchi wakiteseka kwa kukosa huduma hiyo muhimu.

“Ni jambo lisilowezekana kwa DAWASCO, kuwa na ofisi katika kata yetu lakini wakazi wa kata hii wasinufaike na huduma wanazotoa, hakika inashangaza,” anasema.

Anaongeza kuwa, kama atapata ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo, atahakikisha katika kipindi cha miaka mitano, kila mwananchi atakunywa maji safi na salama.

Anasema kero nyingine inayowakabili wananchi ni barabara. Kero hiyo ni kilio cha muda mrefu lakini bado imefumbiwa macho na viongozi waliotangulia wakati maeneo wanayoishi viongozi wa Serikali zimewekwa miundombinu mizuri ya kuvutia.

Bw. Deo anasema, ujenzi wa miundombinu ya barabara haupaswi kubagua maeneo kwani kila mwananchi anawajibika kulipa kodi hivyo ameahidi kusimamia ujenzi wa barabara katika kata hiyo ili wananchi wake waweze kunufaika na ujenzi huo.

"Ndani ya Manispaa kuna fungu linalotolewa kwa ajili ya matengenezo ya barabara, fungu hili litakuwa halitumiki ipasavyo ndio sababu inayochangia barabara hizi kutofanyiwa ukarabati unaostahili,” anasema.

Anasema fedha za ujenzi huo hazitatoka mfukoni kwake bali kwa kushirikiana na viongozi ambao watakuwepo madarakani pamoja na marafiki zake wa ndani na nje ya nchi, atahakikisha wanatafuta wafadhili ambao watatoa fedha ili kufanikisha ujenzi huo.

Mbali na wafadhili hao, ilani ya chama hicho pia itafanikisha ujenzi huo kwani dhamira ya viongozi wa juu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wake Bw. Freeman Mbowe, ni kuhakikisha sekta mbalimbali, zinapiga hatua kubwa ya maendeleo.

Akizungumzia suala la elimu, Bw. Deo anasema kwa muda mrefu sasa, kata hiyo inakabiliwa na tatizo la vijana na watoto kukosa elimu kutokana na upungufu wa shule.

Mkakati wake ni kuhakikisha kila mtoto ndani ya kata hiyo, anapata elimu bora ambayo itatolewa bure kuanzia shule ya awali, sekondari hadi vyuo vikuu.

Ili suala hilo liweze kufanikiwa, atashirikiana na Serikali iliyopo madarakani na wadau wa elimu kuhakikisha zinajengwa shule kuanzia chekechea hadi sekondari.

“Siwezi kuwashau yatima na waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI, nitahakikisha wanapata fursa ya kusoma na kusaidiwa ili waweze kujipatia kipato cha uhakika, kukuza mitaji yao na kujikomboa kiuchumi,” anasema Bw. Deo na kuongeza kuwa, kupitia utaratibu huo, yatima wote watapata elimu bure na waliopo sekondari watatafutiwa wafadhili.


Anasema mpango huo utakuwa umekamilika ndani ya mwaka mmoja ili kupunguza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Anaongeza kuwa, Manispaa imekuwa na kawaida ya kutenga fedha hivyo kinachohitajika ni ufuatiliaji ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Bw. Deo anasema, lipo tatizo la waathirika wa dawa za kulevya katika kata hiyo kutokana na Serikali kutowajengea vijana mazingira mazuri ya kuwanusuru na janga hilo.

Vituo vingi vya polisi vimekuwa vijiwe kwa kurundika vijana badala ya kutafutiwa njia mbadala ambazo zitawafanya waachane na matumizi ya dawa hizo. Kama atakuwa diwani wa kata hiyo, atashirikiana na watendaji wa kituo cha kudhibiti dawa za kulevya ili kuwasaidia vijana hao waachane na matumizi ya dawa hizo.

“Ili niweze kufanikisha lengo hili, nitaunda Serikali ya Kata ambayo itakuwa ikishirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa ili kutafuta mbinu mbadala za kuwaletea wananchi maendeleo, katika Serikali ambayo itaundwa, itahusisha wanawake na viongozi wa siasa bila kujali itikadi zao,” anasema.

Anasema ili kuhakikisha kata hiyo inakuza pato lake, ataboresha soko la Sekenke ambalo kwa miaka 30 sasa, halijawahi kufanyiwa ukarabati hivyo linakabiliwa na hali mbaya ya uchafu na hakuna kiongozi anayejali.

Anaongeza kuwa, tatizo hilo limesababishwa na CCM ambayo imejibinafsisha ardhi ndani ya soko hilo hivyo kusababisha kukosekana mwekezaji wa kuliboresha ili lisaidie kuongeza pato la kata hiyo.

Tuesday, September 28, 2010

MWANAMKE APOKEA KIPIGO TOKA KWA MUMEWE BAADA YA KUPOKEA SIMU KWA NAMBA NGENI


Pamoja na wanaharakati mbali mbali kuendelea kupiga vita vitendo vya unyanyasaji kijinsia vinavyoendelea kuota mizizi hapa nchini,bado baadhi ya wanaume wameendelea kuendekeza mfumo dume kwa wake zao pamoja na kuonyesha ukati wa kutisha.

Katika tukio hililotokea usiku wa kuamkia septemba 28 mwaka huu mwanamke mkazi wa Ilala mtaa wa Mwanayanga mjini Iringa Bi.Faraja amenusurika kifo baada ya kupokea kipigo cha kutisha kutoka kwa mwanaume ambaye amekuwa akiishinaye kwa kile alichodai kuwa ni kupigiwa simu usiku na mtu ayesimtambua ambaye alimtaka kutoka nje ya nyumba hiyo ili wakutane nje.

Akizungumza huku akibubujika damu baada ya kupigwa na kitu kizito katika paji lake la uso na mwanaume huyo ambaye katili ,Faraja alisema kuwa akiwa amekaa ndani ya mumewe huyo ilpigwa simu kutoka kwa mtu asiyefahamika akimtaka wakutane nje na bila huruma mwanaume huyo alianza kutoa kipigo huku akidai kuwa mwanamke huyo ni malaya wa mkubwa pamoja na kutokuwa na uhakika wa namba hiyo.


Hata hivyo baada ya kumpiga na kumuumiza vibaya mtu huyo ambaye alikuwa amepiga simu alirudia tena kupiga simu na kuomba radhi kuwa amepotea namba na kuwa yeye yupo Arusha alikuwa anamka Faraja ambaye ni mtoto wake hivyo inaonyesha namba imekosewa

NA.http://www.francisgodwin.blogspot.com/

DK. BILAL AENDELEA KUUNGURUMA MJINI MBEYA


Wananchi wa Kata ya Nsalaga Kibondenyasi, wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kukinadi chama cha Mapionduzi, wakati wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa kampeni eneo hilo Mkoani Mbeya leo

OIKO CREDIT YATOA MSAADA KCMC


Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyenye akisisitiza jambo kwa Mhasibu wa YWCA Moshi, Haidan Shayo na Dk Henry Nyamubi ambao ni wanachama wa chama cha watu wenye ulemavu kutokana na uti wa mgongo mara baada ya hafla ya kukabidhi hundi kwa zenye thamani ya bilioni 2.1/- kwa YWCA Moshi na Saccos ya Wazalendo zote za mjini humo.

Meneja wa Oiko Credit Tanzania Deus Manyenye (Kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya milioni 500/- Mwenyekiti wa YWCA Moshi, Valentine Mwinga fedha ambazo zimetolewa kwa mkopo kwa ajili ya ukarabati wa jengo la chama hicho lililokaa muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo. Wakati wa hafla hiyo taasisi hiyo pia ilikabidhi hundi yenye thamani ya bilioni 1.6/- kwa Saccos ya Wazalendo ili kusaidia kuwawezesha watu wa hali ya chini. Katikati ni Katibu wa chama hicho, Frida Mbowe.

MWISHO MWAMPAMBA AMVALISHA PETE MERY NDANI YA NYUMBA YA BIG BROTHER


Mtanzania Mwisho Mwampamba akikumbatiana na mchumba wake, Mnamibia Meryl wakati wa sherehe ya kuvalishana pete ya uchumba iliyofanyika kwenye Jumba la Big Brother Africa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki.

Monday, September 27, 2010

MASHINDANO YA ‘Rock City Marathon 2010’ YAFANA


Na Mwandishi Wetu
MWANARIADHA Daudi Joseph na Polnes Chacha wameibuka vinara katika mashindano ya
riadha kilometa 21 yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2010’ yaliyofanyika
Jijini Mwanza Jumapili.
Joseph alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume baada ya kuchukua saa 1:03:40
huku mwanadada Chacha akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa
1:13:10.Zaidi ya wanariadha 200 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.

Wanaume walionekana kuwa na mchuano mkali kutokana na kutopishana sana kumaliza
mbio hizo ambapo Eliya Sidame alishika nafasi ya pili baada ya kupishana na
mshindi kwa sekunde 10 ambapo yeye alitumia saa 1:03:50.
Nafasi ya tatu kwa wanaume ilikwenda kwa Ezekiel Japhet aliyetumia saa 1:04:05
ikiwa ni tofauti ya sekunde 15 na aliyeshika nafasi ya pili na sekunde 25 na
Joseph aliyekuwa kinara wakati kwa wanawake Jacquline Juma alishika nafasi ya
pili kwa kutumia saa 1:18:09 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Rebeka Chacha
aliyetumia saa 1:19:05.
Katika mbio za kilometa 5, Mzungu Ndorobo alishinda na kufuatiwa na Victor
Daniel aliyekuwa wa pili na Dotto Ikangaa akishika nafasi ya tatu wakati katika
mbio za kilometa 3 ambazo zilikuwa maalumu kwa wazee, Jonas Mwangole alishika
nafasi ya kwanza akifuatiwa na Ramadhani Kinye aliyeshika nafasi ya pili.
Kwa upande wa wanawake kilometa 5 mshindi alikuwa Fazina Rashid akifuatiwa na
Saida Romanus aliyeshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa Godriver

HOSPITAL YA Agakhan KUFANYA KAMPENI MAALUMU YA SALATANI 2010







Mkurugenzi wa Hospital ya Agakhan Dkt. Jaffer Dharsee (kushoto) akizungumza nawaandishiwa habari Dar essalaam jana kuhusu Kampeni Maalumu ya Saratani ya Matiti itakayofanyika katika hospital hiyo jumamosi hii kulia ni Ofisa Mawasiliano mwandamizi toka Mfuko wa Taifa wa Bima yaAfya Bw. Luhende Andrew

MSONDO YAWAAGA MASHABIKI WAKE MAX BAR

shabiki maarufu wa msondo ngoma Masoud Nassoro Mzee wa Magorofani akicheza rumba
mafundi mitambo wa bendi hiyo kushoto momba na kilinda wakiwajibika
husein Jumbe na Romani Mng'ande Romario kushoto wakiimba
Super Maliki kushoto na Dokta Mabela
Hamisi Mnyupe akiwea na Romani Mng'ande
Mama Nzawisa akiwajibika
kilinda

Muthungu atwaa blackberry ya Zain




Mwandishi wetu

David Muthungu ameibuka bingwa wa mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya gofu vya Lugalo vya jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 38 na kumzidi mchezaji mkongwe wa mchezo huo Gidion Sayore kwa tofauti ya pointi 3 Sayore alipata pointi 35.

Mashindano hayo yalikuwa na msisimko mkubwa kutokana na wachezaji wengi walioshiliki kucheza kwa makini, ongezeko la wachezaji kila wiki liliwapelekea wadhamini wa mashindano hayo kampuni ya simu za mkononi ya Zain kuboresha zawadi za michuano hiyo.

Muthungu aliyekuwa akipambana vikali na wachezaji wenzie aliibuka mshindi kwa kishindo na kujinyakulia simu ya mkononi ya blackberry kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Zain.

“Kwanza na mshukulu mungu kuniwezesha kushinda simu kwani siku nyingi nimekuwa nikiwaza lini nitashinda na mimi simu, nimezoea kushinda zawadi za kawaida lakini leo mawazo yangu yamekamilika, pia nawapongeza Zain kwakujaribu kuboresha zawadi za mchezo huu pia na kuufanya mchezo huu upendwe na watu wa rika zote,” Alisema Muthungu.

Mbali na Muthungu washindi wengine walikuwa ni Peter Muchiri,Alex Kobia, Stephani Sayore wote walijipatia zawadi mbalimbali kutoka Zain vikiwemo vyombo vya nyumbani, begi za kisasa miamvuli.

HASHIMU WA DAR MORDEN TAARABU AKIPOZI KATIKA KAMERA YA BURUDAN BLOGSPOT

HASHIMU SAID MZEE WA MA LOVE DAV AKIWA KATIKA POZI



MZEE WA MA LOVE DAV HASHIMU SAIDI AKIWA NA SHABANI MADOBE WA SEGERE

Superbrands yaingia rasmi Tanzania



Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi, Meneja wa Tanzania Distilleries Limited KONYAGI Bw. David Mgwassa

Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Ajay Mehta.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mtahaba.

Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinazotambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi. Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kampuni ya Azam Bw. Yusuph Kamau katikati ni Meneja Biashara wa kampuni hiyo ya Azam Bw. Daniel Hill aliyembatana nae.


Dar ES Salaam Taasisi ya Superbrands, ambayo ni taasisi kubwa kuliko zote duniani inayoratibu ubora na thamani ya nembo za bidhaa, hatimaye imeingia rasmi nchini Tanzania, bwana Jawad Jaffer, Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands ametamka hivi majuzi. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na taasisi hiyo, Superbrands inathaminisha nembo ambazo zinatambulika kuwa zenye viwango vya ubora wa juu zaidi kupitia mipango yake mbali mbali. Taasisi hii pia inachapisha vitabu na majarida yanayoelezea shughuli za uimarishwaji na uthaminishwaji wa nembo mbali mbali duniani kote. Superbrands ilizindua miradi yake kwenye masoko makuu mengi duniani kote na inatoa machapisho mbali mbali kwenye takriban nchi 82. Taasisi hii iliingia rasmi Afrika Mashariki mwaka 2007.

Bwana Jawad amesema kwamba taasisi yake itafungua rasmi milango yake kwa makampuni ya Tanzania siku ya Jumatatu, Septemba 27, 2010, siku ambayo itakuwa na matukio mbali mbali muhimu, kama vile hotuba zitakazotolewa na wawakilishi wa Superbrands na Maofisa Watendaji Wakuu wa kampuni za Kitanzania. Hafla hiyo itaambatana pia na hafla ya utoaji wa tuzo za ubora za Superbrands kwa baadhi ya kampuni za Kitanzania ambazo tayari zimethaminishwa kuwa na kiwango cha juu cha ubora wa huduma na bidhaa zao.

Akiongea na waandishi wa habari, bwana Jawad amesema kwamba alikuwa mmojawapo wa watendaji wakuu wa kamati iliyoundwa kuendeleza Nembo ya Kenya, amesema kwamba kwa sasa anaweka mkazo zaidi katika utashi wake wa kuendeleza nembo za kampuni zilizopo Afrika Mashariki ili kuziwezesha kutambulika duniani kote. Amesema kwamba ameichagua Tanzania kuwa kambi kuu ya mkakati wake huo.

Akizungumzia jinsi Superbrands inavyofanya kazi yake, Jawad ameeleza kwamba jambo la kwanza linalofanyika ni kuandaliwa kwa orodha ya nembo za kampuni zinazoongoza na kufanya mchujo hadi kupatikana zile zilizo bora zaidi. Akaongeza kwamba, kinachofuata, baraza maalum la wataalam kutoka kwenye sekta za habari, masoko, utangazaji na mahusiano ya umma, hukutana na kuzipigia kura kila nembo itakayotauliwa, na kuziweka kwenye kiwango cha alama kuanzia namba 1 hadi 10. “Baraza huangalia vipengele vingi kama vile uaminifu wa wateja, kukubalika kwa jumla kwa nembo kwenye soko, muda wake kwenye soko na uimara wake,” Jawad alisema. Alisema, nembo zitakazopata alama za juu kabisa ndizo zinazochaguliwa na kuteuliwa kupata Hati ya Ubora ya Superbrands. Baada ya hapo, walaji (watumiaji) wanaombwa kuzipigia kura nembo hizo kwa vigezo vya umahiri wa nembo, ubora na uzatiti wake.

“Tunapopata maoni ya walaji na ya baraza la wataalam, tunapata mitazamo miwili tofauti ambayo tunaijumuisha ili kupata mtazamo wa jumla wa nembo husika,” alisema bwana Jawad. “Kwa mwendendo huu, tunaweza kupata nembo zenye ubora wa ziada kutoka kwenye kundi la nembo zenye ubora wa kawaiday,” aliongeza.

Kwenye utafiti uliofanyika kwenye kipindi cha mwaka 2007-2008, jumla ya watu 900 walihojiwa nchini Kenya, watu 700 walihojiwa nchini Uganda, na watu 900 walihojiwa nchini Tanzania. Utafiti huu ulifanyika kwenye miji mikuu ya nchi hizi, na ulijumuisha nembo 64 zilizo maarufu zaidi Afrika Mashariki, zilizoonekana kwenye toleo la kwanza la jarida la Superbrands, linalotambua nembo mahiri zaidi kwenye ukanda huu. Kitabu hicho kinajumuisha maelezo juu ya nembo mahiri tofauti, kama vile historia, masoko, mafanikio, bidhaa, matukio mapya, uhamasishaji na thamani ya nembo. Kwa mujibu wa utafiti huo, nchini Tanzania, nembo zilizopata nafasi kumi za juu zilikuwa Azam (1), Nokia (2), Blue Band (3), Tigo (4), VodaCom TZ (5), Kilimanjaro Pure Drinking Water (6), Whitedent (7), University of Dar es Salaam (8), Chai Bora – TATEPA (9), na Omo (10).

Japokuwa utafiti huo unaofanyika Afrika Mashariki sio wa muda mrefu sana, Superbrands inaendesha mkakati wake huu kwa mara ya pili hapa Afrika Mashariki, ikitarajia kwamba toleo la pili la jarida la Superbrands kuchapishwa mwaka huu wa 2010.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Jawad alisema kwamba changamoto kubwa analokutana nalo wakati wa utendaji wake wa kazi ni uelewa mdogo wa masuala ya nembo za kibiashara miongoni mwa wadau mbali mbali. Ili kukabiliana na changamoto hii, amesema kwamba Superbrands Afrika Mashariki ina mpango wa kuendesha kampeni ya uhamasishaji kwenye uwanda huu, ambapo vitabu vitasambazwa kwenye makampuni na taasisi mbali mbali, hususan vyuo vinavyotoa mafunzo ya kibiashara ili kuongeza uelewa na ufahamu na maarifa kuhusu masuala ya nembo na uendelezaji wa nembo. Amesema mkakati huu utawavutia, hususan, wamiliki wa viwanda ambao tayari wameziona jitihada hizi kama mojawapo ya njia ya kuzitambulisha shughuli zao kwa wanafunzi na hivyo kuimarisha uingizwaji wao kwenye mfumo wa utendaji kazi, ikilinganishwa na mikakati mbali mbali ya mafunzo yanayoendeshwa kwa ajili hiyo kila mwaka. Jawad amesema kwamba tayari kuna mifano hai ya utafiti juu ya nembo zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ambayo inatumika kama sehemu mojawapo ya mafunzo kwenye vitivo vya biashara kwenye vyo vikuu nchini Kenya.

Akiendelea na maongezi, Jawad amesema kwamba hivi sasa kuna mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa kwenye uendezwaji wa harakati za uimarishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jambo ambalo linahitaji kampuni kujenga uelewa na ufahamu wa nembo zao nje ya mipaka ya nchi zao. Alisema kwamba baada ya miaka miwili suala la nembo litakuwa ni jambo muhimu sana.

“Tunachotaka kufanya ni kuziendeleza nembo zaidi ya kile unachokiona kila siku. Tunaitaka serikali kusaidia kusogeza mbele nembo zinazoheshimika ili kuwasaidia watu kuzielewa,” alisema. Jawad alisema pia kwamba anataka nembo za Afika Mashariki kutambulika katika ngazi ya kimataifa. “Kwa kuhamasisha utambuzi na uelewa wa nembo tutakuwa tumechangia jambo hilo kufanikiwa,” alisema. Alisema anasikitika kwamba nembo za Afrika Mashariki hazijafikia hatua ya kuweka alama ya kijiografia, wakati kuna nembo ambazo ni vichocheo muhimu vya uchumi wa nchi zilizoendelea.

Akielezea juu ya faida ambazo Superbrands inazipatia kampuni, Jawad amesema kwamba Superbrands inachangia kwa kiwango kikubwa kuwapo kwa utambuzi na uelewa wa nembo, ambapo kupitia machapisho yake, maelezo juu ya kampuni za Afrika Mashariki yanasambazwa ndani ya Afrika Mashariki na nje yake. Maelezo yanayopatikana kwenye machapisho ya Superbrands zinaweza kuwa chanzo cha taarifa kwa watu binafsi au taasisi ambazo zinataka kuwekeza kwenye kampuni, alisema.

Bwana Jawad alisisitiza kwamba Superbrands pia ni kichocheo cha mauzo, kwani kampuni zinaweza kutumia maelezo yanayochapishwa juu yake kuimarisha mahala pake na kujijengea mkakati wa upanuzi wa soko lake. Alionesha mfano wa utafiti uliofanyika muda si mrefu uliopita nchini Uingereza, ambao ulibainisha kwamba wateja wanakuwa wepesi zaidi kununua bidhaa au huduma yenye nembo rasmi ya Superbrands, kuliko zile ambazo hazina chapa hiyo. Mtazamo kwamba baadhi ya nembo za Kenya zinatambulika sana nchini Uganda na Tanzania unaweza kuisaidia nembo kufikiriwa kupenyeza kwenye masoko ambayo mafanikio mazuri yanatarajiwa.

Akihitimisha, bwana Jawad alisema kwamba Superbrands inachangia utoaji wa maamuzi wa watendaji wakuu wa makampuni, akibainisha kwamba Superbrands inaipa nembo hadhi kubwa ambayo ni ujumbe wenye nguvu kubwa kwa wateja wa kibiashara, waajiriwa na wanahisa.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na bwana Jawad wa Superbrands Afrika Mashariki ___________________________________.