Monday, October 31, 2011

FRANSIC MIYAYUSHO AMTWANGA MBWANA MATUMLA KWA POINT



Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Mbwana Matumla wakati wa mpambano wao Dar es salaam jana
Jab Jab akuna kulala fransic akipiga jab jab kila wakati ndicho kilicho mfanya ashinde mpambano huo jana


Kamanda wa Polosi Kanda Maarumu, Suleimani Kova akimvisha mkanda wa Ubingwa Bondia Fransic Miyayusho baada ya kushinda kwa pointu kulia ni Diwani wa KInondoni Kata ya Hananasifu, Abasi Tarimba na kiongozi wa kambi ya ngumi ya kinondoni Lazima Ukae, meneja ambaye ni mkurugenzi wa Kisangani Genalar Trades ya Kariakoo,Bobani

Masumbwi mawe kwa kwenda mbele

Matukio Safari Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel Kuelekia Fainali Za Mrembo Wa Dunia



|
Miss Vodacom Tanzia 2011 Salha Israel aliye vaa Nguo za Njano katika Mazoezi ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi na wenzake .. katika safari ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia.
Na Fredy Njenje

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA JAJI WARIOBA



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Sinde Warioba kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 31,2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Sinde Warioba, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 31,2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NBC na mabenki sita ya biashara yaingia makubaliano na (NHC)leo



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu akisaini hati za makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Lawrence Mafuru kuhusu suala la mikopo ya nyumba jijini Da es Salaam leo, Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia Kesogukewele Msita.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna
Tibaijuka (kushoto) akishikana mikono na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru katika hafla ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilisaini hati za makubaliano kuhusu mikopo ya nyumba na benki saba nchini. Benki hizo ni NBC, NMB, BOA, EXIM, Azania, KCB na CBA. Wa pili kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT) Lila Mkila na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka (katikati, nguo nyekundu), Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa benki saba zilizosaini makubaliano ya ushirikiano na NHC.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Lawrence Mafuru (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano kuhusu suala la mikopo ya nyumba jijini Da es Salaam leo, Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia Kesogukewele Msita.

Blogu Ya 8020 Fashion Yatimiza Miaka 5 Ya Utendaji Wake




Shamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion akimlisha keki mgeni rami Mh Angela Kairuki wakati wa hafla ya blogu hiyo kutimiza miaka 5 ya utendaji wake wa kazi.
Mmiliki wa Blogu ya mavazi ya 8020 Fashions Shamimu Mwasha kushoto aka Shamimu Zeze pamoja na mgeni rasmi Mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam Agela Kairuki wakizundua nembo ya mavazi ya B2A itakayomilikiwa na Shamimu, wakati wa hafla ya kutimiza miaka 5 ya mtandao wa 8020 Fashions iliyofanyika kwenye ukumbi wa Daimond Jubilee jijini Dar es salaam leo mchana.
Tukio hilo limedhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa kusaidia wanawake MMWEI na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers kupitia kinywaji chake kikali cha Baileys
hamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion na mgeni rasmi Mh Angela Kairuki wakiangalia mavazi ya nguo zilizobuniwa kwa kutumia nembo ya mavazi ya B2A kama wanavyoonekana
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakijimwaga stejini kucheza muziki kama wanavyoonekana katika picha.
Joseline Kamuhanda kushoto na Grace Lyon kutoka Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania , Mwamvita Makamba kulia akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa MMWEI Vodacom Tanzania Mwamvua Mlangwa katika hafla hiyo.

Saturday, October 29, 2011

MBWANA MATUMLA NA FRANSIC MIYAYUSHO WAPIMA UZITO KWA AJILI YA KUPIGANA KESHO

Francis Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla wakitunishiana misuri leo baada ya kupima
Mbwana Matumla akipima uzito leo

AUNT EZEKIEL AADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA PAMOJA NA WASANII WENZAKE LUKUKI


Aunt Ezekieli akikata keki yake ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaamwa leo.Pembeni ni watoto Yatima wa kituo cha Umra cha Jijini Dar es Salam
MSANII wa Luninga,Aunt Ezekiel aadhimisha siku yake ya kuzaliwa na Watoto Yatima pamoja na Wasanii wenzake lukuki katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salam jana.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili alisema ameamua kuiadhimisha kwa staili hii kwa kujumuika na badhi ya Watoto Yatima wa kituo cha Umri kilichopo Kawe Jijini Dar es Salam kwasababu yeye alitoka katika mazingira hayo mpaka kufikia hapo alipo, hivyo hujisikia furaha kujumuika na watoto yatima mahali popote anapokuwa haswa wakati wa furaha kama siku yake ya kuzaliwa, alisema Aunt Ezekiel.
Aunt Ezekiel katika sherehe hiyo alitimiza miaka 30 hivyo pia aliwahusisha wasanii wenzake mbalimbali kama JB,Dr.Cheni,Mboto,Wema,Cloud,Sinta,Chilele,na wengine wengi pamoja na marafiki zake ambao kila mmoja aliingia viwanja vya Leaders kwa staili yake haswa kwa kuonyesha umarufu wao kwa kumiliki gari la kifahari kila mmoja.
Aunt Ezekiel alizaliw JIJINI Mwanza na alilelewa katika mazingira ya watoto Yatima na katika sherehe yake aliwazawadia watoto Yatima vifaa vya Shule kwa kila mmoja na Chakula kwa Kituo chao.

MBWANA MATUMLA NA FRANCIS MIYAYUSHO WAPIMA UZITO LEO

Mabondia Mbwana Matumla 'Golden Boy' na Francis Miyayusho 'Chichi Mawe' leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam kesho jumapili OKCTOBA 30.

wakizungumza wachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima wamesema wapo tayari kuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha zisizo na kifani kwa sababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua tumejiandaa vya kutosha

Licha ya mabondia hawo kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali ususani Ukimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.

Mapambano hayo ya kati ya Juma Fundi na Fadshili Majia, Mohamed Matumla na Ramadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli wakati kwa upande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere) atazichapa na Salma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D;

Twiga Bank ilivyoshiriki katika maonesho ya Wizara ya Fedha


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo (kulia) akitoa maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha na Mpigapicha wetu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo akiwaonesha waandishi wa Habari Nishani ya Ulezi Bora wa Vikoba iliyotunukiwa Benki ya Twiga kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini. Mbululo alikuwa akiionesha wakati Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Twiga Bank, Adelbert Archard akitoa akiwagawia wanafunzi vipeperushi na kuwapa maelezo juu ya Akaunti maalum ya Akiba kwa watoto , walipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo akizungumza na waandishi wa Habari juu ya huduma zitolewazo na Benki hiyo wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kushirikisha taasisi zake zote. Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Wake wa viongozi wa Jumuia ya Madola washiriki mkutano wa CHOGM 2011


Na Anna Nkinda – Perth, Australia

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni mmoja wa wake wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuia ya madola waliohudhuria mkutano wa siku tatu wa jumuia hiyo unaofanyika mjini Perth nchini Australia.

Wake hao wa viongozi walishiriki ufunguzi wa mkutano huo uliofunguliwa na Malkia Elizabeth wa pili na baada ya ufunguzi waliweza kuendelea na ratiba yao ya kujifunza na kujadili mambo mbalimbali yanayaikabili jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na afya, elimu, utamaduni, mila na michezo.

Baada ya kumalizika kwa ufunguzi huo walianza ratiba yao kwa kusikiliza mada kuhusu afya ya binadamu ilitolewa na Kanali Dk. Robert Walters ambaye ni Balozi wa Serikali wa afya ya binadamu na Julian Krieg Afisa mtendaji na mwalimu wa jamii katika mpango wa mkoa wa Afya ya binadamu.

Mme wa Waziri Mkuu wa Australia Tim Mathieson aliweza kuwatembeza wake hao wa viongozi maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na makumbusho ya Australia’s Aboriginal and Torres Strait Islander ambako waliweza kujifunza historia ya nchi hiyo pamoja na utunzaji wa mila na utamaduni wao.

“Asili ya wenyeji wa nchi hii ni watu weusi ambao kwa sasa kizazi chao kinatishia kumalizika kutokana na uchache wao lakini miaka ya nyuma Waingereza walihamia hapa na kuzaliana na hivyo idadi yao kuwa kubwa kuliko wenyeji hivi sasa asilimia kubwa ya waustralia ni watu weupe.

Nchi hii inaongozwa na waziri mkuu Julia Gillard’s huku mtalawala wa nchi akiwa ni Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili”, alisema Mathieson.

Katika makumbusho hayo pia walijifunza mila za watu wa Magharibi ya Australia ambao wanaishi kandokando ya Bahari ya Hindi hivyo walifahamu utawala wao, faida wanazozipata hususani za kibiashara na utalii kutokana na matumizi ya bahari na bandari ambayo ni lango kuu la meli.

Waliweza kutembelea bahari ya Hindi na kujionea shughuli za biashara na utalii zinavyofanyika katika ukanda wa pwani, meli kubwa za mizigo zinavyotia nanga, kupakua na kupakia mizigo na kuona jinsi maaandalizi ya mashindano ya kimataifa ya mchezo wa mashua (Sailing World Championships) yanayotarajia kufanyika katika mji huo mwishoni mwa mwaka huu yanavyoendelea.

Wake hao wa viongozi walishukuru kwa ziara na mafunzo waliyoyapata na kusema kuwa yatawasaidia katika kazi zao wanazozifanya kila siku ikiwa ni pamoja na kuboresha afya ya mama na mtoto na elimu ya mtoto wa kike.

Thursday, October 27, 2011

VIPAJI MCHEZO WA NGUMI VINAINULIWA HIVI


Kocha mkongwe wa mchezo wa ngumi Habibu Kinyogoli akimwelekeza mtoto Salim Mponda (5) jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi ya klabu ya ngumi ya Amana Dar es salaam




Wednesday, October 26, 2011

FRANCIS MIYAYUSHO NA MBWANA MATUMLA WATAMBIANA MPAMBANO JUMAPILI

Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla wakitunishiana misuri mbele ya waandishi wa habari katikati ni Mohamedi Bawaziri mratibu wa mpambano huo.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Mratibu wa mpambano wa ngumi Mohamedi Bawaziri katikati akiwa na mkanda wa ubingwa utakaogombaniwa na mabondia Fadhili Majia (kushoto) na Juma Fundi siku ya jumapili.(Picha na Linkwww.superdboxingcoach.blogspot.com)

Tuesday, October 25, 2011

STAR TIMES YATOA MSAADA WA VYAKULA SHULE YA MSINGI UHURU MCHANGANYIKO LEO

Meneja Masoko wa Star Times Zuhura Hanifu (kushoto) akikabidhi baadhi ya vyakula walivyotoa kama msaada kwa Mwalimu mkuu wa SHule ya Msingi UHuru Mchanganyiko, Bi, Anna Mang'enya leo wanaoshuudia wa pili kushoto ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Bw. Fidelis Charles na Ofisa Masoko na Ufundi Bw.Erick Cyprian



Saturday, October 22, 2011

DEO NJIKU NA JONAS SEGU WATAMBIANA BAADA YA KUPIMA UZITO

Bondia deo Njiku akimtambia mpinzani wake Jonas Segu kwa kumonesha vidole vitatu na kusema atamtwanga katika raundi hiyo katikati ni Kocha wa Mchezo wa Ngumi Mhamila Rajabu 'Super D Boxing Choach'
kocha wa mchezo wa ngumi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D Boxing Coach' katikat akiwainua mikono juu mabondia Deo Njiku wa Morogoro kushoto na Jonas Segu wa Dar es salaam baada ya kupima uzito katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro LEO kwa ajili ya mpambano wa kuwania ubingwa wa taifa wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) utakaofanyika KESHO.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)