Thursday, May 31, 2012

SAFARI LAGER YATANGAZA TAREHE NA ZAWADI ZITAZOKABIDHIWA KWA WAJASILIAMALI WASHINDI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.


  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika grogramu ya ruzuku ya “Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam jana.Vifaa hivyo vitakabidhiwa mwishoni mwa wiki katika viwanja  vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya.
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa  kwa wajasiliamali  ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali walioshinda katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali. Bwana Oscar alisema, “Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. Aliendelea, “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09 June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye viwanja vya leaders Club.”
Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea .
Akionyesha baadhi ya ruzuku zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda bwana Oscar alisema, “wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano .
Bwana Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
Bwana Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano la Wezeshwa na Safari Lager, alisema “Shukrani nyingi ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha haya na aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lagerbaadae mwaka huu
 .
Meneja akizungumza na waandishi wa habari

DOGO ASLAY, ORIJINO KOMEDY WAPAMBA UZINDUZI WA KAMPENI YA 'TUKO WANGAPI?TULIZANA!


Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Fatma Mrisho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kimataifa ijulikanayo kama ‘Tuko Wangapi?, Tulizana’.
 Dk.Mrisho ambayea likuwa mgezi rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Golden Tulip amesema kwamba kampeni hiyo imelenga kuongeza idadi ya Watanzania wanaojua maana ya mtandao wa ngono, hatari ya kuambukizwa VVU kutokana na kuwa mmoja ya wanamtandao wa kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja.
 Dogo Aslay jukwaani
 Original Komedy wakiwa kazini




Bondia wa kike,Lulu Kayege ajifua kwa ajili ya kuwakabiri wapinzani wake

 Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Kondo Nassoro akimfundisha bondia chipkizi wa kike,Lulu Kayege Dar es salaam leo kwa ajili ya kujiandaa  na mashindano ya kumi bora yatakayofanyika june 15 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni Dar es salaam

Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo  anaenolewa katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchini


Wednesday, May 30, 2012

AMOSI MAKALA AKABIDHI BENDERA KWA WACHEZAJI WA GOFU


Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala ameitaka timu ya Taifa ya Wanawake ya gofu kuhakikisha inapeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano ya All Africa Challenge yanayotarajia kuanza Juni 5, Botswana.

Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kesho kutwa huku ikiwa na Wachezaji watatu sambamba na mkuu wa msafara ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Maendeleo na watoto ya bunge Mary Chitanda.

Timu hiyo inaondoka nchini ikiwa tayari imeisha wahi kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka 2010 ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo Makala alisema watumie matoke hayo ya awali kwa kufanya vyema zaidi na kuweza kupeperusha vyema bendera ya nchi.

"Kama katika taarifa yenu ionavyosema mashindano ya mwisho mlishika nafasi ya pili sasa tunaimani mashindano haya mtakuwa wa kwanza na kuweza kututangaza vyema katika bara hili la Afrika, hivyo nendeni makaipiganie nchi yenu na kwa manufaa ya michezo," alisema.

Naye kwa upande wake Kepteni wa timu hiyo Madina Idd alisema kama waliweza kushika nafasi hiyo ya pili na wakati huo walikuwa katika maandalizi mabovu hivyo kwa sasa wanawahakikishia Watanzania wataibuka na ushindi.

"Mwaka 2010 tulishiriki na hata kufanikiwa kushika nafasi hiyo na huku tulikua katika maandalizi ya kusuasua lakini kwa sasa naimani tutafanya vyema zaidi," alisema.

Sambamba na hilo Shirika la ndege la Precion Air leo limekabidhi tiketi saba kwa timu  hiyo zikiwa ni za kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na tisheti na kofia vyote vikiwa na jumla ya sh. milion 7.3.

WAZIRI AMOS MAKALA AIKABIDHI BENDERA TIMU YA (TAIFA TAIFA STARS)


Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala akizungumza na waandishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi bendera kwa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inayokwenda Nchini Ivory coast kucheza na timu ya taifa ya nchi hiyo  jumamosi ya wiki hii ambapo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuipa raha Tanzania kwa kishindo kizito na kuwatangazia kuwa wasiogope wachezaji wa Ivory coast makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA PHILEMONI SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Rais wa shirikisho la Mpira Tanzania TFF Bw, Leodger Tenga akiwatakia wachezaji hhao kila la heri katika safari yao na kuwatakia ushindi mwema.
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Paulsen akiwahakikishia watanzania kuwa watakwenda kule Ivory Coast  kushinda kwani amewafundisha wachezaji wake namna ya kujiamini wenyewe na pia kuwa na nidhamu mchezoni ili waweze kupata ushindi.
Wachezaji wa timu ya Taifa waliohudhuria katika Tafrija hiyo ya kukabidhiwa Bendera.
Naibu waziri wa Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala (kushoto) akimkabidhi bendera ya taifa kapteni wa timu hiyo Mlinda mlango Juma Kaseja.

TUMBAKU HUUA WATU MILIONI 6 KWA MWAKA DUNIANI KOTE



NA MWANDISHI WETU
WAKATI Watanzania wakitarajia kudhimisha Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani kesho, imebainika kuwa tumbaku huua watu takribani milioni sita (6), kila mwaka.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Kumbana na Matumizi ya Tumbaku, Lutgard Kagaruki wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani.
Alisema maradhi yabayosababishwa na tumbaku huathiri nchi zite duniani, na ndiyo maana jumuiya ya kimataifa ikaungana na Mkataba wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alisema  Mkataba huo umebeba misingi muhimu ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku, itakayoweza kuokoa maisha ya watu milioni 200 ifikapo mwaka 2050, kama itatekeleza ipasavyo.
Alisema muingiliano wa kampuni za tumbaku umekuwa tishio kubwa kuliko yote kwa mikakati ya kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alibainisha kuwa mkataba huo unavipengele muhimu kwenye Kanuni namba  5.3 ambacho kinaeleza bayana mgongano mkubwa wa maslahi uliopo kati ya kampuni za tumbaku na afya ya jamii.

THABEET KUFUNDISHA KIKAPU WATOTO 200



NYOTA wa NBA, Hasheem Thabeet anategemea kutoa mafunzo ya siku mbili ya kucheza mpira wa kikapu kwa watoto 200 walio chini ya miaka umri wa miaka 17 kwenye  Uwanja wa Don Bosco kuanzia Juni 2 hadi Juni 3.

Thabeet anayechezea timu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ataongoza kliniki hiyo yenye lengo la kuibua vipaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Thabeet alisema  mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ni tofauti kidogo na yale ya mwaka jana.

“Ninaimani kliniki hii itakuwa tofauti na ile iliyopita kwa sababu watoto wengi wamepata mwamko wa kucheza mpira wa kikapu baada ya kuona mafanikio ya wenzao,”anasema Thabeet.

Naye Meneja wa Sprite nchini Warda Kimaro wanadhamini wa mashindano hayo alisema baada ya mafunzo hayo vijana hao watakuwa kwenye mpango maalum wa kuendelezwa na kampuni yake.


Habari - Jackson Odoyo
Picha - globalpublishers.info

JK AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IVORY COAST JIJINI ARUSHA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo Mei 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea  kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.PICHA NA IKULU

Wakiwa katika picha ya pamoja.

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE


Baada ya  kufanya  show ya Big Brother  Afrika Kusini MSANII Abdul Naasib ‘Diamond’ni mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kamambe kulipamba  shindano la Redd’s Miss Chang’ombe 2012 shindano litakalofanyika Juni 9 mwaka huu  katika ukumbi wa Quality Centre barabara ya Nyerere Jijini Dar es Slaam.
Wengine watakaopamba shindano hilo la aina yake ni  kundi la Original Commedy akina Joti na bendi ya mapacha watatu ambayo kwa sasa imekuwa moja ya bendi zinayokonga  nyoyo za mashabiki wengi wa muziki hapa nchini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam msemaji wa Kampuni ya King Promoters  ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo Martin Mauya ameaema kuwa kwa sasa warembo hao wameendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya klabu ya TCC Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo linatarajia kushirikisha warembo bomba 14 watakaopanda jukwaani kuchuana vikali kumpata mrembo wa mkoa huo wa kimashindano wa Chang’ombe huku baadhi ya wadau wa fani hiyo ya urembo nchini wakitabiri kuwa mrembo wa Tanzania mara hii atatokea katika mkoa huo wa kimashindano.
Mauya  amewataja warembo wanaotarajia kupanda jukwaani ni Elizabeth Mushi, Restituta Faustine, Miriam Ntakisivya, Flora Kazungu, Flora Robert,  Like Abraham, Clara Diu, Margareth Gerald, Jesca Haule, Deborah Nyakisinda, Suzan Paul, Wensley Matius, Zulfa Bundara na Catherine Masumbigana.
‘Kwa sasa warembo hao wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani lakini Juni 3 warembo hao wataingia rasmi kambini katika Hoteli moja kubwa Jijini kabla ya kuapnda hiyo Juni 9’ alisema Mauya.
Shindano hilo limedhaminiwa na REDD’S ORIGINAL, NEXUS CONSULTING AGENCY, DODOMA WINE, CXC AFRIKA, PAPAZII INTERTAINMENT, KITWE GENERAL TRADERS,CHERISH, BEN EXPEDITION, SCREEN MASTERS, ARDHI PLAN LIMITED.

Meneja mkuu wa kampuni ya tigo atembelea kampuni ya Clouds Media Group leo jijini Dar


Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez akizungumza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pichani kulia,mara baada ya kumaliza ziara ndani ya kampuni hiyo  na kujionea mambo mbalimbali,shoto ni Ofisa Mahusiano wa Tigo Alice Maro.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo akifanya mahojiano mafupi na mtangazaji wa Choice FM,aitwaye Thandi Kathembe mapema leo jioni.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga (pili kutoka kulia),akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez alieambatana na Ofisa Mahusiano wake, Alice Maro,kulia ni Dj Fetty.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez (pichani kati),Kulia ni mmoja wa watangazaji wa Clouds FM,Ruben Ndege.
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez akiperuzi moja ya jarida la Burudani hapa nchini la KITANGOMA,linalochapishwa na kampuni ya Prime Time Promotions LTD. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikiwa tayari kwa kurushwa hewani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikitayarishwa kabla ya kwenda kurushwa hewani.

WANASHERIA WA KIMATAIFA WASAIDIA KUWAJENGEA UWEZO WANASHERIA WA KITANZANIA


 Mkuu wa Chuo cha Sheria cha Tanzania Dr. Gerald Ndiku akiongea katika ufunguzi wa mafunzo kwa ajili ya wanasheria wa hapa nchini kuwajengea uwezo na mbinu za uandika maandiko ya kisheria, namna ya kutengeneza vipengele vya upatanishi wa mizozo, mwenendo wa kesi mahakamani, mikataba ya kuuza na kununua, mikataba ya mikopo pamoja na mbinu na taratibu zake na maandishi mengine ya kisheria kwa ujumla.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki akisoma risala yake kuashiria ufunguzi wa mafunzo ya sheria kupitia Chuo Cha Taifa Cha Sheria kupitia shirika la kujitolea lijulikanalo kwa jina la New Perimeter lililoanzishwa na DLA Piper kwa muda wa wiki 2 kwa wanafunzi wapatao 240 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Bw. Simon Boon kutoka DLA Piper- London Kitengo Maalum cha Restructuring ambaye pia ni kiongozi wa mradi akiongea machache.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Sheria cha Tanzania Dr. Gerald Ndiku, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki  wakiwa pamja na Bw. Lawrence Masha kutoka IMMMA Advocates.
 Wageni waalikwa wakiwa na wanafunzi.
Mshereheshaji wa sherehe hiyo, Bw. Sebo akiongea machache kabla ya kumaliza ufunguzi.
 Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baaya ya kufungua mafunzo hayo.

WEMA SEPETU AVARISHWA PETE NYINGINE YA UCHUMBA NA BWANA WA 4 ASEMA MWENYE BAHATI HABAHATISHI


Mwimbaji wa bendi ya Machozi, Mwinyi akimvalisha pete ya uchumba mwigizaji wa bongomovie Wema Sepetu ambapo sherehe hiyo ilifanyika ndani ya Maisha Club jijini Dar es Salaam jana na kusema kuwa mwenye bahati habatishi sasa amefika na hayawi hayawi sasa yatakuwa.
 Hapa akiwa amepiga magoti.
 ...Furaha na nderemo zikiwa zimetawala.
....Kwa Raha zao wakifurahia. Picha/Dj Choka Blog.

Mwimbaji wa bendi ya Machozi, Mwinyi akimvalisha pete ya uchumba mwigizaji wa bongomovie Wema Sepetu ambapo sherehe hiyo ilifanyika ndani ya Maisha Club jijini Dar es Salaam jana na kusema kuwa mwenye bahati habatishi sasa amefika na hayawi hayawi sasa yatakuwa.
 Hapa akiwa amepiga magoti.
 ...Furaha na nderemo zikiwa zimetawala.
....Kwa Raha zao wakifurahia. Picha/Dj Choka Blog.

Mwimbaji wa bendi ya Machozi, Mwinyi akimvalisha pete ya uchumba mwigizaji wa bongomovie Wema Sepetu ambapo sherehe hiyo ilifanyika ndani ya Maisha Club jijini Dar es Salaam jana na kusema kuwa mwenye bahati habatishi sasa amefika na hayawi hayawi sasa yatakuwa.

 Hapa akiwa amepiga magoti.

 ...Furaha na nderemo zikiwa zimetawala.
....Kwa Raha zao wakifurahia. Picha/Dj Choka Blog.

WAZIRI AMOS MAKALA NA MATUKIO JIJINI DAR ES SALAAM


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi bendera kwa Timu  ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa kusafiri kwenda  Gaborone Botwsana kwa ajili ya mashindano ya chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake.Wapili kushoto ni  Mh. Mery Chatanda (Mbunge).(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia. (Picha na Benjamn Sawe wa WHVUM)