Mkurugenzi
wa kikundi cha uigizaji cha The Original Comedy, Isaya Mwakilasa
'Wakuvanga' akielezea katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es
Salaam leo, jinsi walivyojiandaa kushiriki katika Bonanza la Tigo
litakalofanyika kesho na kesho kutwa kwenye ufukwe wa Coco, Oysterbay
jijini. Kushoto ni Mratibu wa Promosheni wa Tigo, Edward Shila na Alice
Maro ambaye ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo.(PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA)
Friday, June 29, 2012
TBL FAMILY DAY YAFANA DAR
Wanafamilia wa TBL wakimuangalia mcheza sarakasi wa kikundi cha Black Texas, wakati akitembea juu ya waya.
Mtoto wa moja ya familia ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambaye hakufahamika jina lake akitoa shoo ya bure katika bonanza la wafanyakazi hao kufurahi pamoja na familia zao, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mnasihi wa VVU wa AMREF, Peace Kayoza (kushoto), akimchukua kipimo cha damu Zaina Mohamed, mmoja wa wanafamilia ya TBL katika bonanza hilo.
Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akijadiliana jambo na viongozi wenzake wakati wa bonanza hilo.
Watoto wa familia ya TBL wakiogelea.
Wafanyakazi wa TBL wakiwa wameshika zawadi za fulana.
Ofisa wa TBL Salvatory Rweimamu (kulia) akimkabidhi zawadi mtoto wa wanafamilia ya TBL aliyeshinda mbio.
MSAFARA WA RAIS WAZUIWA KWA KUWEKWA MAWE BARABARANI TEGETA, WALINZI 42, WANANCHI 56 WASHIKILIWA POLISI
Baadhi ya akina mama wakiwa na vyombo vyao eneo la wazi baada ya nyumba zao kubolewa. |
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam, linawashikilia walinzi 42 wa Kampuni ya Nassy, wananchi 56 na mmiliki wa Kituo cha kuuza mafuta cha Gapco cha Namanga Tegeta, wakituhumiwa kubomoa nyumba 10 za wakazi wa eneo hilo.
Tukio la kubolewa nyumba hizo lilifanyika katika eneo hilo jana asubuhi na kuzua tafrani kubwa iliyosababisha watu kadhaa kujeruhuiwa na kuurushia mawe msafara wa Rais Jakaya Kikwete uliokuwa ukielekea Bagamoyo.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishina Msaidizi (ACP), Charles Kenyela alisema watu hao wanashikiliwa kwa ajili ya upelelezi kufuatia tukio hilo.
Alisema tukio hilo limetokana na mgogoro wa ardhi kati ya mmiliki wa kituo hicho Hemed Salum na wakazi wa eneo hilo ambapo jana alikwenda na walinzi hao na kuanza kubomoa nyumba hizo.
" Katika hali ambayo haikufahamika mara moja mmiliki wa eneo hilo licha ya kuwa jambo hilo lipo mahakamani alifika eneo hilo walinzi hao na kuanza kubomoa nyumba hizo'' alisema Kenyela.
Alisema watu hao wanashikiliwa kusaidia polisi na kuwa watu wawili waliojeruhiwa vibaya wapo Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Mmoja wa wananchi wa eneo hilo alisema hali hiyo imetokana na Polisi kushindwa kulifanyia kazi kwani mara kwa mara walikuwa wakipelekewa malalamiko lakini walikuwa wakipuuza.
"Haya ndio matokeo baada ya polisi kutupuuza na sasa yametokea madhara ndio wanakuwa wakwanza kufika tunaomba rais aingilie kati sula hili kwani naye amepata adha ya jambo hilo". alisema mkazi huyo.
Kufuatia tukio hilo familia zilizokuwa zikishi katika nyumba hizo hazina mahali pa kuishi hadi tunaondoka eneo la tukio walikuwa wakiwasiliana na ofisi ya Serikali ya Mtaa wa eneo hilo kuona n jinsi ya kuwasaidia.
KHITMA YANGA YAISHA SALAMA 'ALHAMDULILLAH'
Hitima
Yanga imekwishasomwa, iliongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum. Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani
Omar Madega, Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa
Julai 15, Clement Sanga walikuwapo. Sasa watu wanakula, BIN ZUBEIRY
anaondoka eneo la tukio.
Waungwana baada ya kisomo wakisubiri sadaka |
Sheikh Mussa kulia, kushoto ni Katibu wake Almasi lailly Mussa na nyuma yao ni mwanachama wa Yanga, Mustafa Mohamed, Katibu wa Tawi la Kurasini |
Madega kulia, akiwa na Sanga kushoto kwake |
Waungwana wakisubiri sadaka baada ya dua |
Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa kulia, Madega na Sanga |
Sheikh Mussa katikati, kulia Juma Mnonji mwanachama wa Simba, na kushoto Katibu wake, Almasi |
Waungwana baada ya dua wakisubiri sadaka |
Maandalizi
ya hitima katika klabu ya Yanga, makao makuu wa klabu, makutano ya
mitaa ya twiga na Jangwani yanaendelea muda huu. Mboga zinakaribia
kuiva, mchele umekwishaanza kuoshwa. Ng’ombe wawili wako jikoni. Ibada
ya hitima yenyewe inakaribia kuanza kusomwa. Picha zote kwa msaada wa
Blog ya BIN ZUBEIRY
Akina mama wakichambua mchele |
Akina mama wakichambua mchelehttp://richard-mwaikenda.blogspot.com/ |
Tunawatambulisha Kwenu Blog maalum ya Miss Utalii Tanzania/Miss tourism Organisation.
Miss Utalii Tanzania, tofauti na mashndano mengine
ya urembo, ni zaidi ya shindano la urembo, kwani linalenga katika
kutangaza na kuhamasisha Utalii,Utamaduni, Mianya ya
Uwekezaji,Elimu,Afya ya Jamii,Utalii wa ndani,Utalii wa
kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikitano Kitaifa na kimataifa.
Shindano hili pia linahamasisha vita dhidi ya Umasikini,Iharibifu wa
mazingira,uwindaji haramu,Uvuvi Haramu,Ujinga,Maradhi, Tamaduni kongwe
na Potofu. Miss Utalii Tanzania pamoja na uchanga wake, tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2005, ni shindano lenye mafanikio makubwa kuliko shindano
jingine lolote nchini kitaifa na kimataifa kwani pamoja na kuipa heshima
Tanzania ya kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la Miss Tourism World
2006, shindano hili ndilo lililo andika historia ya Tanzania kutwaa taji
la kwanza la Dunia kabla na baada ya uhuru, pale tulipo twaa taji la
Miss Tourism World 2006, pia shindano hili ndilo pekee nchini
linashikilia rekodi ya kutwaa mataji ya dunia katika kila shindano
tulilo shiriki,tumetwaa mataji 6 ya dunia tangu 2005. Kutokana na
mafanikio haya , Tumepewa heshima ya kuaandaa shindano la Dunia la Miss
Umoja wa Mataifa mwaka 2013 hapa Tanzania. Ni shindano pekee nchini
ambalo washiriki wake hawavai mavazi ya kuogelea, bali mavazi ya heshima
yasiyo mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yaliyo buniwa na kushonwa
kwa malighafi za tanzania tu.
Link yetu ni : http://www. misstourismorganisation. blogspot.com
Facebook Page: https://www.facebook.com/ MissUtaliiTanzania
E-Mail: missutaliitanzania@gmail.com
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM KATIKA MAONYESHO YA VIFAA VYA USAFI MANISPAA YA ILALA
Moja ya
gari maalum kwa ajili ya kufagia barabara (Road sweeper) gari hilo linafagia
barabara na kumwaga uchafu mbali zaidi.maonyesho hayo yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Said Meck Sadick akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na Operesheni ya usafi inayoendelea katika Manispaa ya Ilala ambapo
aliwataka wananchi wa ilala kuwa na Ushirikiano kwa kutoegesha magari ovyo
pasipo utaritibu ili waweze kupisha magari ya kufanyia usafi.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Rachel Charles
MKURUGENZI Mtendaji wa Ear promotion Bw.Brian Kikoti amewaomba wafanyabishara ndogondogo wa soko la wamachinga complex kupeleka bidhaa zao na sio kuliacha mpaka lichangamke.
Ameyasema hayo leo alipokuwa anaongea na wafanyabiashara katika
soko la wamachinga jijini Dar es salaam, alisema wafanyabiashara
ndogondogo hawapaswi kulikimbia soko hilo kwa madai kuwa hakuna wateja.
Bw.Kikoti alisema wamachinga wote wanapaswa kushirikiana na ear
promotion ili kulitangaza soko hilo ndani na nje ya nchi ili kukuza
uchumi kwa wafanyabiashara waweze kujikimu kimaisha na ata kukuza uchumi
wa Taifa.
Pia alisema ili kulifanya soko hilo litambulike kimataifa watakuwa
na maonyesho ya gulio litakalofanyika kila mwaka mwezi wa tisa kwa muda
wa siku 14 ili kuwasaidia wafanyabiashara hao kutangaza bidhaa zao kwa
uraisi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ear Promotion Bw. Frank Miti alisema
kila sikukuu wataleta makampuni mbalimbali ili kuunga mkono mawazo na
kuwawezesha wafanyabiashara hao kupata faida kubwa.
Aidha Wafanyabiashara ndogondogo wamelipongeza jambo hilo kwa kuwa
litawapa fursa ya kuingia kwenye ushindani na kubadilishana biashara
na Nchi nyingine hivyo kupata misaada kutoka kwa wafadhili.
KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR LEO
Baadhi ya maofisa mbalimbali na wananchi wakiwa katika Baraza la
Wawakilishi wakisikiliza Hotuba na Michango mbalimbali inayotolewa na
Wajumbe wa Baraza hilo.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu mwenye kitabu
akibadilishana mawazo na mwananchi ambae alienda kumuona huko katika
Baraza la Wawakilishi nje ya mji wa Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
RATIBA YA MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME 2012
KAGAME CUP 2012 FIXTURE
Sat. 14th July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm
2 YANGA vs ATLETICO Uwanja wa Taifa 4pm
Sun. 15th July 3 AZAM vs MAFUNZO Chamazi 4pm
Mon. 16th July 4 VITA CLUB vs PORTS Uwanja wa Taifa 2pm
5 SIMBA vs URA Uwanja wa Taifa 4pm
Tue. 17th July 6 ATLETICO vs APR Uwanja wa Taifa 2pm
7 WAU SALAAM vs YANGA Uwanja wa Taifa 4pm
Wed. 18th July 8 VITA CLUB vs URA Uwanja wa Taifa 2pm
9 PORTS vs SIMBA Uwanja wa Taifa 4pm
Thu. 19th July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm
11 MAFUNZO vs TUSKER Uwanja wa Taifa 4pm
Fri. 20th July 12 PORTS vs URA Uwanja wa Taifa 2pm
13 YANGA vs APR Uwanja wa Taifa 4pm
Sat. 21st July 14 AZAM vs TUSKER Uwanja wa Taifa 2pm
15 SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa Taifa 4pm
Sun. 22nd July REST DAY
QUARTER FINALS
Mon. 23rd July 16 B2 vs C2
17 A1 vs C3
Tue. 24th July 18 C1 vs A2
19 B1 vs A3
Wed. 25th July REST DAY
SEMI FINALS
Thu. 26th July 20 Winner 16 vs Winner 17
Thu. 26th July 21 Winner 18 vs Winner 19
Fri. 27th July REST DAY
FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
Sat. 28th July 22 Loser 20 vs Loser 21
23 Winner 20 vs Winner 21
|
WEMA SEPETU AAGANA NA OMOTOLA.
Hapa Wema Sepetu akimvalisha kanga msanii huyo. |
BIG RIGHT KUWAZAWADIA MABONDIA WAKE ENDAPO WATASHINDA
Kocha
wa ngumi wa Kambi ya mazoezi ya Big Right, Ibrahim (katikati) akiwa na
mabondia wake wakati akiwasimamia katika Kambi yao ya mazozi ya pamoja
kama timu kujiandaa na mapambano yao yanayotarajia kufanyika Julai 15
katika Ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es Salaam, mwaka huu.
********************************************
KATIBU
wa Vijana wa CCM Kata ya Kinondoni, Rehema Mbegu, ameahidi kutoa zawadi
ya Baiskeli kwa Mabondo wa Klabu ya Mazoezi ya Big Right ya
Mwananyamala jijini Dar es Salaam, iwapo watashinda katika mapambano yao
yanayotarajia kufanyika hivi karibuni, ili kuwa moyo zaidi vijana
kuupenda mchezo wa Masumbwi.
Rehema mbegu, mara kadhaa amekuwa akishirikiana na vijana wa Kata yake katika masuala mbalimbali ya Kijamii na ya kuendeleza michezo, ambapo amekuwa karibu zaidi na vijana wa rika zote na kuwapa sapoti kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri kujishughulisha na michezo zaidi ili kuepuka kutojiingiza katika mkumbo wa matumizi ya madawa ya kulevya.
Mabondia hao baada ya kuhakikishiwa zawadi nono ya kila atakayeshinda kuibuka na Baiskeli, wamezidi kuwa na morali zaidi na kutoa ahadi zao kwa Katibu huyo kuwa watafia ulingoni hadi kieleweke kwa kutupa mawe ya ukweli kwa wapinzani wao watakaokutana nao siku hiyo ya pambano.
Vijana hi wamekwishaanza kambi yao ya pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja kama timu chini ya Kocha wao, Ibrahim Bigright na kuongeza muda wa mazoezi ambapo kwa sasa wanafanya mara tatu hadi kwa siku.
Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele, kutoka Kambi ya Matumla, katika uzani wa fly weight, Mwaite Juma kutoka Bigright Boxing,ambaye atapigana mkongwe Anthony Mathias, katika uzani wa Bantam.
Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa ni kati ya JUMA
FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo kutoka kambi ya mzazi
Rehema mbegu, mara kadhaa amekuwa akishirikiana na vijana wa Kata yake katika masuala mbalimbali ya Kijamii na ya kuendeleza michezo, ambapo amekuwa karibu zaidi na vijana wa rika zote na kuwapa sapoti kubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri kujishughulisha na michezo zaidi ili kuepuka kutojiingiza katika mkumbo wa matumizi ya madawa ya kulevya.
Mabondia hao baada ya kuhakikishiwa zawadi nono ya kila atakayeshinda kuibuka na Baiskeli, wamezidi kuwa na morali zaidi na kutoa ahadi zao kwa Katibu huyo kuwa watafia ulingoni hadi kieleweke kwa kutupa mawe ya ukweli kwa wapinzani wao watakaokutana nao siku hiyo ya pambano.
Vijana hi wamekwishaanza kambi yao ya pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja kama timu chini ya Kocha wao, Ibrahim Bigright na kuongeza muda wa mazoezi ambapo kwa sasa wanafanya mara tatu hadi kwa siku.
Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele, kutoka Kambi ya Matumla, katika uzani wa fly weight, Mwaite Juma kutoka Bigright Boxing,ambaye atapigana mkongwe Anthony Mathias, katika uzani wa Bantam.
Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa ni kati ya JUMA
FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo kutoka kambi ya mzazi
Katika Mchezo huo kutakua na DVD Mpya kabisa za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili
ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua
sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny
Paquaio, Amiri
Khani,
Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na
matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa
dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa
MASANJA NA WAKUVANGA WA KUNZI NZIMA LA ORINGINAL COMEDY KUPAMBA TAMASHHA LA TIGO COCO BEACH KESHO
.
DEIDRE LORENZ KAINGIA KWENYE MAPENZI NA TANZANIA
Deidre Lorenz akimkabidhi picha ya Ground
Zero (New York) Rais wa Mt. Kili Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya
kukimbia mbio hizo.
Deidre Lorenz akiwa anahojiwa na waandishi wa Habari mjini Moshi.
---
Na Grace Soka, Afisa Uhusiano
MT. KILIMANJARO MARATHON 1991
Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre
Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio
za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka
23 tangu zianzishwe mwaka 1991.
Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu
ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa
Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na
timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania
ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini
Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea
kuipenda sana Tanzania.
“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii”
alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4
kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro
ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote” aliendelea
kusema Deidre Lorenz.
Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye
mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake
katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu
wakarimu sana.
Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon
zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la
matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa
zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi
zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima
Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental
Races.
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa kutambua mchango wake katika uchumi
wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani
Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu
aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.
“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi
mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi”
alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya
ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.
Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa
klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya
makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio
hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia
kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston
Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia”
alibainisha Frances.
Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances
pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika
jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu
mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu
la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.
ZANZIBAR FILM FESTIVAL July 5
Mwaka huu mastaa kibao watashuka Bongo. Kutoka Marekani anakuja Mario
Van Peebles. Kama umeangalia filamu ya All Things Fall Apart ya 50
Cent utakuwa umewahi kumuona huyu jamaa, mle ndani aliigiza kama baba
wa 50 Cent.
Cabo Snoop naye atadondoka kutoka Angola, yote ni kuzifanya siku tisa
za tamasha zisimchoshe mtu yoyote, bila kwuasahau mastaa wetu Bongo
kama Diamond, Linah, Barnaba, Roma na Sultan King.
Bongo Movies wao ndio wataongoza jahazi la filamu, JB, Davina, Irene
Uwoya, Jackline Wolper, Cloud na wengine wengi wataheadline katika
tamasha.
Van Peebles. Kama umeangalia filamu ya All Things Fall Apart ya 50
Cent utakuwa umewahi kumuona huyu jamaa, mle ndani aliigiza kama baba
wa 50 Cent.
Cabo Snoop naye atadondoka kutoka Angola, yote ni kuzifanya siku tisa
za tamasha zisimchoshe mtu yoyote, bila kwuasahau mastaa wetu Bongo
kama Diamond, Linah, Barnaba, Roma na Sultan King.
Bongo Movies wao ndio wataongoza jahazi la filamu, JB, Davina, Irene
Uwoya, Jackline Wolper, Cloud na wengine wengi wataheadline katika
tamasha.
AZAM MARINE KUMALIZA TATIZO ZANZIBAR
a
Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
Azam
yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni
kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli
hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI
ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa
ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka
huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.