Tuesday, July 31, 2012

MKURUGENZI MWANAHALISI AILALAMIKIA SERIKALI BAADA YA KUFUNGIA GAZETI LAKE



 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali halisi , inayo chapisha
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akiongea na Waandishi wa
habari katika Ofisi za Kampuni hiyo juu ya malalamiko yake kwa
serikali kutokana na kufungiwa kwa gazeti lake la Mwana halisi jana
ambapo alilaani vikali uamuzi huo uliochukuliwa na serikali na hivyo
kuitaka serikali kufuta mara moja Tamko lake Kushoto ni Mhariri wa
Gazeti  hilo Bw, Jabir Idrissa.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kubenea
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali halisi , inayo chapisha
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akionyesha baadhi ya Magazeti
yaliyolalamikiwa na Serikali.

DEWJI AZIPATIA USHAURI TIMU ZA SIMBA, YANGA





MWANACHAMA maarufu wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Azim Dewji amezishauri klabu kubwa za Simba na Yanga nchini kuanza kuutumia mtaji wa wanachama wake kujijenga kiuchumi, na kuepuka kuwa tegemezi.
Dewji, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashatra maarufu nchini, alisema kwamba kila klabu ina zaidi ya wafuasi milioni 15 nchi nzima, lakini ajabu klabu zinaendelea kuwa ombaomba.
“Huu ni mtaji mkubwa sana, lakini utashangaa klabu haina hata asilimia moja (150,000) ya wanachama wa kweli. Kila siku utasikia wanachama 3,000 hadi 6,000. Kiongozi wa klabu anachaguliwa na wanachama wasiofika 2,000?
“Jamani, kwa klabu inayoshabikiwa na mamilioni ya watu inashindwaje kujijenga kiuchumi kwa kuwatumia mashabiki wake waliozagaa kila kona ya nchi? Jiulize, kama angalau hao watu 150,000 tu wakilipa ada ya mwaka ya 12,000 ambayo hata hivyo bado ni ndogo, si wanaweza kuvuna sh
bilioni 1.8 kwa mwaka, hizi si fedha nyingi?
“Kuna haja ya kufanya mapinduzi ya kweli, badala ya kufikiria kuifunga Simba au Yanga na kutwaa ubingwa wa Bara. Timu yenye uchumi imara, ndiyo inayokuwa na jeuri ya kuwa na kikosi imara na hivyo kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Huko ndiko tunakopaswa kwenda,” alisisitiza.
Aidha, Dewji ameipongeza Yanga kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwishoni mwa wiki, baada ya kuizamisha Azam kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Dewji, aliyewahi kuifadhili Simba na kuifikisha fainali za Kombe la CAF mwaka 1993, alisema pamoja na yeye kuwa `Simba Damu’, ana kila sababu za kuimwagia sifa Yanga kwa kuwa imezika haraka matatizo yake na kugeukia kusaka maendeleo.
“Huwezi kuamini kama Yanga iliyopigwa 5-0 na kuibua tafrani nzito Jangwani, ndiyo hii ya leo. Wameikubali hali na kubadilika ndani ya muda mfupi sana. Wana amani na matunda yake yameonekana ingawa walikuwa na kipindi kifupi cha kusuka timu na kurejesha mshikamano ndani ya klabu.
“Naipongeza Yanga na hasa Mwenyekiti wake, Yussuf Manji kwa sababu naamini imani ya wanachama juu yake ndiyo iliyorekebisha hali haraka, naye kama kiongozi kuhakikisha usajili makini unafanyika, kocha anapatikana na uzalendo ndani ya Yanga unarejea,” alisema Dewji.
Aliongeza kuwa, pamoja na matunda ya haraka ya uongozi wa Manji, wana-Yanga wanapaswa kumpa ushirikiano ili kuiondoa Yanga katika utegemezi wa miaka nenda rudi, huku akisisitiza Manji hatabaki Yanga milele.
“Wana kiongozi shupavu, sasa washirikiane naye kuujenga uchumi wa klabu. Haya mambo ya kutegemea mtu kila kukicha si mazuri. Na hili si kwa Yanga tu, hata Simba na klabu nyingine zinapaswa kujikita katika kujijenga kiuchumi ili ziwe na jeuri ya fedha bila ya kutegemea mifuko ya mwanachama mmoja mmoja,” alisema.

MABALOZI WA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSTELI ZA WASICHANA WA SEKONDARI WAZINDUA KAMPENI YA ELIMU YAO WAJIBU WETU

Mabalozi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog)  Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na asiyekuwepo ni Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004) ambaye alikuwa na udhulu na atakuwepo katika kampeni zinazoendelea.

Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa katika mradi huu.


Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.

Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.

Mabalozi hawa wameiita kampeni yao “Elimu Yao. Wajibu wetu” maana ya usemi huu ni kwa kila mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha mtoto wa kike anapewa haki yake ya kuwa na elimu bora. Haki hii ya elimu inajumuisha mazingira mazuri ya kusomea. Hivyo huu ni wito kwa watanzania, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanawake watanzania waliofanikiwa na watanzania wa ughaibuni kujitokeza kwa wingi na kuhusika moja kwa moja na jitihada hizi.

Changamoto ambazo mtoto wa kike anakumbana nazo hususani anayetokea nyumbani kwenda shule ni pamoja na kukosa muda wa kujisomea kutokana na kazi za nyumbani ambazo zinapelekea kuathiri maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike, mimba na ndoa za utotoni ni kati ya changamoto kubwa zinazowakumba wale waliopanga karibu na maeneo ya shule, kutokana na hayo, Mabalozi hawa wameamua kujitolea kwa kuweka mpango mkakati utakaosaidia ujenzi wa hosteli tano na kuendelea kati ya hizo 30 ambao TEA imepanga kujenga.

Mpango mkakati huo ni pamoja na kufanya kampeni katika vyomba mbalimbali vya habari nchini na kuandaa  mbio za hisani ambapo hela zitakazopatikana zitapelekwa katika mradi huo. Mabalozi hawa wanaamini kuwa tofali moja kutoka kwa kila mtanzania linaweza kuleta mabadiliko “changia Tofali”. Unaweza kuchangia kwa kutuma neno "Changia Tofali"kwenda namba 15564, na utakuwa umechangia Tshs 250/-. Changia mara nyingi uwezavyo.
Tunakuomba mchango wako wewe mzazi, wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla wenu kuchangia katika kampeni hii. Mchango unaweza kuwa ni wa fedha taslimu au vifaa vya ujenzi wa hosteli na samani. Kwa upande wa fedha taslimu unaweza kuweka fedha katika akaunti ya “mfuko wa elimu” benki ya CRDB, namba ya akaunti 01J027639900 au kupitia akaunti ya M-pesa 404040, au tuma ujumbe Changia Tofali kwenda namba 15564. Pia unaweza kuleta mchango wako katika ofisi zetu zilizopo mikocheni barabara ya kambarage au kupitia vituo vya Televisheni vya ITV, Channel 10 na Star TV.

ERASMUS MTUI KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA YA MADEREVA


  Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Scania nchini Tanzania, Mark Cameron(kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa dereva, ErasmusMtui ambaye ni mshindi wa mwaka 2011 anayekwenda kwenye mashindano ya Kimataifa ya Bingwa wa Mabingwa yanayotarajiwa kufanyika  Afrika Kusini.Makabidhiano hayo yalifanyika makao makuu ya ofisi za Scania Dar es Salaam 
Erasmus Mtui akizungumza na waandishi wa habari

KAMPUNI ya Scania Tanzania leoimeandaahaflafupikumuagamshindiwamashindanoyamaderevayanayojulikanakama“Tanzania Driver Of The Year” yaliyofanyikakatikaviwanjavya Biafra sikuyaJumamositarehe 19th November mwakajana. 
Mr. Erasmus Mtui, mwenyeumriwamiaka 44 aliyebukamshindibaadayakufaulukatikangazizotetatuzashindanohilomwakajanaameajiriwakamaderevakatikakampuniyausafirishajiya Super Star Forwarders iliyokobarabarayaNyerere, Dar Es Salaam. “Nimefanyamazoezinanimepatamafunzoyakutoshakabisa, kwasasanikotayarikukabiliananashindanolijalo, naahidikufanyajitihadazanguzoteiliniiwakilishevizurinchiyangu, benderaya Tanzania ipeperukevizurikwenyemashindanohaya!” AlijigambaBw. Mtui.  
Akiongeanawaandishiwahabari, Bwana Mark Cameron MenejaUendeshajiwakampuniyaScania Tanzania alisemakwamba‘Derevandiokiungomuhimupekeekatikauchumi, mazingiranausalama. Maderevawenyeutaalamunawanaopendakaziyaohusaidiakuendeshakwausalamabarabarani, hutumiamafutakidogo, hiihusaidiakiwangokidogo cha uchafuziwamazingira”.AlisemakwambaScaniailianzishamashindanoyamaderevakwamaraya kwanza mwaka 2003 katikanchizaulaya. Mashindanohayayalieneanakuwayadunianzima, yakionyeshaumuhimuwautaalamukwamaderevapamojanakusisitizamafunzokwamaderevailikuboreshaufahamuwausalamabarabaraninauchafuziwamazingiraunaosababishwanamoshiwamagari. Mr. Cameron alimalizakwakusema “Maderevandioutiwamgongowasektayausafirishaji. Pamojanakutengenezamagarimakubwa bora, salamanayanayotumiamafutavizuriScaniamudawoteinamuangaliamtualiyekonyumayausukani. Kwamaraya kwanza tumewezakufanikishamashindanohayahapa Tanzania, tukonamshindiwetuMr.Mtuiambayeamejiandaavizuri, tunamuamininatunatarajiaatatusababishiasifakubwa, tunamtakiakila la kheri!. 
Naye Bi. Margaret Legga, afisamasokomsaidiziwakampuniyaScania Tanzania alisemakwambamashindanohayayaliyopewajina la “BingwawaMabingwa”yatafanyikakatikamjiwa Sun City hukoAfrikayaKusinimapemamweziujaokuanziatarehe 09 hadi 11. Mashindanohayayatajumuishamaderevakutokamabaramenginekamabara la Ulaya, Asia naAmerikayaKusini, kutokanchizaAfrikakunamaderevakutokanchiza Botswana, Lesotho, Malawi, Namibia nasisi Tanzania. WaandaajiwamashindanohayanikampuniyaSwiss organisation UICR Union Internationale Des ChaffeursRoutiersna The South African RTMC Road Traffic Management Corporation, Scanianimojawapoyawadhaminiwakuuwashindanohili. Shindanohilihufanywamarambilikilamwaka.Mwakahuujumlayamadereva 105 kutokanchi 17 kotedunianiwatachuanakatikangazitofauti 6 zashindano.Mr.Mtuiatashindanakatikakitengo cha “Semi truck and trailor” ambachoatapambanakikwelikwelikwanikiladerevaatatakiwakuonyeshaufundikwakuendeshanakupitavipimo 19 vyamchuano. Vipimohivinipamojanauendeshajiunaotumiamafutakidogo, namnayakubebamzigokiusalama, kulifahamugarianaloendesha, bilakusahauuendeshajimakinibarabarani. KufanyikakwashindanohilihapabaranikwetuAfrikakunatuongezeauwezekanowakufaulusisiwenyeji” Alimaliza Bi.Legga. 
Kama mojawapoyawatengenezajiwamagarimakubwanamabasiwanaoongozaduniani, Scaniainaendeleakuonyeshakujitoleakwakenakuwajibikakatikakujengasekta bora yausafirishajiinayosababishafaidakwapandezote. Ili kufikiahili, utaalamunauelewawamaderevanivitumuhimusana. 
Mashindanoyamaderevayajulikanayokama“The Scania - Tanzanian Driver of the Year competition”yanatoanafasikwamaderevakujadilinakuelezea mambo ambayoyatasaidiakupunguzaajalibarabarani, yataongezafaidabainayawadaumbalimbaliwasektahii. Yanaonyeshapiakwawananchiwotevipajivyamaderevawetunamchangowaomuhimusanakwausalamawetuikiwanichangamotokwamaderevawenginekuongezaujuzi, navijanakujiunganaajirahii.

Wateja wa Airtel sasa kutuma pesa Bure kupitia Airtel money


Kupata huduma ya Airtel money  sasa piga *150*60# Bure

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa  muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure  
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi  nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma  na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa  na mengine mengi
tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60#   na kuunganishwa moja kwa moja
vilevile  tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha  wateja wetu wote na wakala  wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii  iliyorahisi ni rahisi aliongeza” Mmbando
Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha  na kusaidia wateja wetu kuokoa muda  kwenda mbali kupata huduma za kibenki.
Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi

Monday, July 30, 2012

BONDIA IBRAHIMU CLASS AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WA IDI PILI


Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com