Wednesday, October 31, 2012

SHINDANO LA UNIQUE MODEL LAZINDULIWA KWA KISHINDO HOLIDAY INN JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model) linaloandaliwa na Unique Entertainment limezinduliwa leo jumatano kwa kishindo katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo katika ya jiji la Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari hao katika ufunguzi huo mkurugenzi wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa mchakato wa shindano umefunguliwa rasmi ili kutoa fursa ya wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo ambalo litakuwa na mvuto wa aina yake kwa msimu huu wa pili.

Pia wanamitindo wenye sifa za kimataifa wameombwa kujitokeza kwa wingi katika usaili utakaofanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada Apartments.

 Tumeboresha shindano kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali,lengo ni kulifanya shndano hili liwe la heshima,hadhi na linalotimiza lengo lake la kuvumbua na kuinua vipaji vya wanamitindo wa kchipikizi.

“Tunaomba wabunifu wadogo kwa wakubwa wajitokeze kuja kuonyesha umahili wao katika shindano hili ambapo mwaka huu tutakutanisha wabunifu wengi wa mavazi nchini Tanzania katika shindano moja kwa lengo la kuwainua wabunifu wadogo na kuendelea kuwatangaza wabunifu wenye majina makubwa katika tasnia ya mitindo hasa katika kipindi hiki maridhawa cha mwisho wa mwaka” alisisitiza Magese.

Katika msimu huu wa pili wa unique model kutakuwa na nyongeza ya mataji mengine madogo matatu amabayo ni “model photogenic 2012”,”model talent 2012” na “model with good manner 2012” ambapo mataji hayo yatakuwa chini ya taji kuu la “Unique model of a year 2012”.

Fainali za shindano la Unique model 2012 zitafanyika mwishoni mwa mwezi Desemba ambapo kamati ya maandalizi imedhamilia kufanya onyesho lenye hadhi kuanzia ubora wa washiriki wenye vigezo vya uanamitindo ambao wataleta mabadiliko katika tasnia ya mitindo nchini.

Shindano la Unique model lilianzishwa mwaka 2010 ambapo kwa mwaka huu ni mara ya pili kufanyika,Asia Dachi ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo mpaka sasa.

Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kuchukua mabalozi ambao ni wanamitindo washiriki kwa lengo la kufanya nao kazi za kutangaza bidhaa ama huduma inayotolewa na kampuni husika kwa lengo la kutoa ajira kwa wanamitindo hao wanaochipukia katika tasnia.

Unique model 2012 imedhaminiwa na Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,Mashujaa investment ltd,Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu investment ltd,Oriental bureau de change,100.5 Times fm,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel, na Unique entertainment blog.

Afande Sele anaukaribisha mwaka mpya



Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Soma Ule’ ambayo itakua ngoma ya kuukaribisha mwaka 2013.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Afande Sele alisema wimbo huo utakua ujumbe wa kufungia mwaka na kuukaribisha mwaka mpya na kwamba yupo katika hatua za mwisho za uaandaaji wa kibao hicho.

“Audio nishamaliza saivi nafanya video, unajua redio saivi hazina soko sana watu wengi wanapenda kuangalia na sio kusikiliza, hivyo namalizia kurekodi video baada ya hapo ntaipelela sokoni, kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki,” alisema Afande Sele.

Mbali na hilo, Afande Sele alisema kwasasa wanaendelea na mchakato wa kusaidia jamii kwa kutoa fedha pamoja na vifaa vya hospitalini kama shukrani kwa wadau wa kazi zao, ambapo unaongozwa na mkali wa muziki huo, Joseph Haule ‘Professa Jay’.

“Professa kaanzisha mchakato huo, ambao unajulikana kama ‘Nishike mkono’ na hivi karibuni tumesaidia vifaa katika hospitali ya watoto  ya Tumbi iliyopo kibaha, hivyo tunaomba sapoti kwa wadau wa muziki na mashabiki wa kazi zetu,” alisema Afande Sele.

Barnaba: Sijutii kwa niliekuwa nae



Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barnaba Elias ‘Barnaba’ ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Sijutii kwa niliekuwa nae’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barnaba alisema wimbo huo kaupeleka sokoni wiki iliyopita na kwamba imeshaanza kufanya vizuri katika soko hilo, kitu ambacho kinampa moyo wa kufanya kazi hiyo.
“Kama kawaida yangu nyimbo zangu nyingi huwa haziwachukizi mashabiki wangu ni jambo ambalo namshukuru mungu kwani ni wasanii wachache ambao nyimbo zao zinafanya vizuri mtaani,” alisema.
Barnaba alisema anawaomba mashabiki wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya kuzipokea kazi nyingine.
Mbali na kibao hicho, Barnaba alishawahi tamba na vibao vyake kama, Magubegube, Wrong number, Tulizana, Milele daima na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini.

IZO ZILIPENDWA YA MATONYA VIDEONI




Na Elizabeth John
BAADA ya kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Taxi bubu’, Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Seif Shaban ‘Matonya’, ameachia video ya kibao chake cha ‘Izo Zilipendwa’ kinachofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaama jana, Matonya alisema anamshukuru Mungu kibao chake kufanya vizuri kwani ni dalili nzuri ya kazi zake kukubalika, hivyo kuwaahidi wapenzi na mashabiki wake mambo mazuri zaidi.

“Kiukweli kazi hii imefanya vizuri, kitu ambacho kinanipa matumaini katika ‘game’ na natumaini video hii itakuwa bora zaidi,” alisema Matonya.

Matonya amewasihi mashabiki wake kukaa mkao wa kula kukisubiri kibao hicho na kwamba yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho.

Mbali ya kibao hicho, Matonya amewahi kutamba na vibao mbalimbali mahiri kama ‘Anita’,  ‘Vaileth’ na vinginevyo ambavyo vilimtambulisha kwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

UZINDUZI WA SHINDANO LA UNIQUE MODEL 2012 WAFANYIKA LEO

Mkurugenzi wa shindano
  la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model)   Methuselah Magese (kulia) akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es salaam leo wengine kushoto ni Planning Officer Hyassinter Julius na Head Finance Happy Mushi

Mkurugenzi wa shindano
  la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model)   Methuselah Magese (kulia) akizungumza mbele ya waandishi

Mkurugenzi wa shindano
  la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model)   Methuselah Magese (kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es salaam leo wengine kushoto ni Planning Officer Hyassinter Julius na Head Finance Happy Mushi

Mkurugenzi wa shindano
  la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model)   Methuselah Magese (kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es salaam leo wengine kushoto ni Planning Officer Hyassinter Julius na Head Finance Happy Mushi

WAKAZI WA DAR WAFURAHIA USAFIRI WA GARI MOSHI



Bi. Rose Ngauga akizungumza na mwandishi wetu aliyemtembea ofisini kwake kujua mawili matatu kuhusiana na usafiri huo.
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wamefurahia kuanza kwa usafiri wa treni waliousubiri kwa muda mrefu ulioanza juzi.
Abiria wakigombea kupanda treni kutoka katikati ya jiji kueleke Ubungo.
Kamera yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri huo.
Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.
Wanafunzi wakipanda katika behewa lao maalumu tayari kwa safari.
Bi. Rose akimuonyesha mwandishi wetu (hayupo pichani) tiketi zinazotumika kwa abiria wa kawaida na wanafunzi.
Abiria wakiwa katika dirisha la kukatia tiketi.
Wanafunzi wakikata tiketi katika dirisha maalumu kwa ajili yao.
Kichwa cha treni kikiunganishwa na mabehewa kabla ya kuanza safari.
Abiria wakiwa wameketi ndani ya behewa wakisubiri kuanza safari.
Mkuu wa Kituo cha Reli, Bi. Rose Ngauga akikagua mabehewa kabla ya gari moshi kuanza safari leo saa 9.40 alasiri.
...akikabidhiwa ripoti.
Gari moshi likiwa katika mwendo na baadhi ya abiria wakionekana wakichati na simu.
Mwandishi mwanadamizi wa Global Publisher, Haruni Sanchawa akishuka kutoka katika treni hiyo maeneo ya Ubungo Maziwa ambako treni hiyo umalizia safari yake.
Abiria wakishuka kwenye treni.
Pamoja na usafiri huo kuanza, mafundi wa shirika la reli bado wanaendelea na ukarabati wa reli kama wanavyoonekana pichani.

YANGA YAIFUNGA MGAMBO 3-0


 Beki wa Yanga, Mbuyi Twite akimpongeza Nadir Haroub ‘Canavaro’ baada ya kufungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Mgambo ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 3-0.
 Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva akimpongeza Nadir Haroub baada ya kufunga bao la kwanza

Didier Kavumbagu na Ramadhan Malima wa Mgambo kwenye mchezo wakichuana katika mchezo huo.

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA KWA SADALA-MASAMA HAI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongezza Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe kwa hotuba nzuri ya kumkaribisha na kumsifia kwa kazi anayofanya katika maendeleo ya miundombinu nchini katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati)  na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe wakizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani Hai. (Picha kwa hisani ya Ikulu)

Rais Jakaya Kikwete akisaidiwa kuzindua jiwe la msingi na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani Hai.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe wakikata utepe mojawapo ya magreda katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na wananchi katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo

Serikali Kusaidia Kubana Wanaokiuka Sheria Za Filamu



Maelezo 31/10/2012 

 KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976. Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania. Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria. Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni. “tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan. Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya Mtanzania. “Sisi kama bodi kazi yetu ni kukagua filamu na matangazo yake kama yapo kimaadili na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madaraja filamu hizo kabla hazijaenda sokoni.”amesema Bi.Fissoo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM-TAIFA, MJINI DODOMA LEO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo Oktoba 31, 2012 kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo baada ya ufunguzi uliofanyika leo, mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na William Malecela, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo.

DOKEZO LA AMIR MHANDO KUTOKA TASWA


Naomba kuwajulisha kuwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) na Muungano wa Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA) kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wameandaa mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake wa Afrika itakayofanyika Desemba 10 na 11 mwaka huu Nairobi, Kenya.

Kutokana na hali hiyo Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimepewa nafasi ya waandishi wa habari wanawake watatu washiriki kwenye mafunzo hayo na imepokea barua hiyo leo na inatakiwa hadi Ijumaa wiki hii iwe tayari majina hayo yametumwa pamoja na wasifu wa wahusika walioteuliwa.

Kwa msingi huo kwa kutumia njia hii ya uwazi zaidi, naomba waandishi wanawake wenye nia na muda wa kushiriki mafunzo hayo wawasilishe CV zao kabla ya Ijumaa (Novemba 2, 2012) saa sita mchana ofisini kwa Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (Hifadhi House ghorofa ya 9 zilipo ofisi za JamboLeo, Posta)  au kwangu mimi ofisi za Daily News Tazara, Dar es Salaam.

Masharti ya mafunzo ni kuwa yataendeshwa kwa lugha ya Kingereza na Kifaransa, lakini pia watakaoshiriki wawe tayari kuja kutoa elimu watakayaoipata huko kwa wenzao pindi watakaporudi nchini.

Suala la CV ni la umuhimu kupita maelezo, kwani baada ya hapo mchana siku hiyo TASWA itateua majina matatu na kuyatuma TOC kwa taratibu nyingine.

Watakaoteuliwa watalipiwa nauli ya kwenda Nairobi na kurudi Dar pamoja na malazi na chakula kwa siku zote watakazokuwa huko.Tuchangamkie nafasi, kumbuka ni kwa wanawake tu.

Nawasilisha kwa utekelezaji.(Kama hujaelewa tuwasiliane 0713415346)
Katibu

REDDS MISS TANZANIA YATANGAZA VIINGILIO NA WASANII 31 Oktoba 2012 .



Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano la Taifa la Redds Miss Tz kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz Bosco majaliwa

Fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  Ubungo Plaza jijini D’salaam
Akizungumza na waanmdishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari na leo tupo hapa kuwatangazia watanzania na washika dau wote wa tasnia ya Urembo kuwa tiketi kwaajili ya shindano letu la mwaka huu zipo tayari na zipo kwa idadi maalum na leo hii zinaanza kuuzwa katika vituo tulivyovipendekeza kulingana na maoni ya wadau
Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagarimu kiasi cha shilingi laki moja (100,000) za kitanzania.
Katika kufanikisha shindano hili kutakuwa na vitu tofauti na miaka ya nyuma na tutarajie kuona shindano lenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya warembo wetu ni wasomi walio katika ngazi ya elimu ya juu nchini
Vituo vinavyoanza kuuza tiketi hii leo ni. Stears samora
Regency park Hotel,Rose garden Mikocheni,Share illusion-Mlimani City,Giraffe Hotel,Ubungo Plaza na ofisi za Lino.
Nitoe rai kwa wapenzi wote waweze kupata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu kwa sababu ya kikomo cha tiketi kilichopo kama tulivyotangaza awali
Kwa upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii nguli hapa nchini kama
1)   Diamond Platnum
2)   Winfrida Josephat’Rachel’
3)   Wanne star ngoma troupe
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo yanayojulikana kama [Fast Tract] Tayari washiriki 5 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika kundi la Warembo 15 Bora.     [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni
Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Babylove Kalalaa – Miss Talent
City sports lounge-iliyopo posta mpya mkabala na mnara wa askari.
Happiness Daniel – Miss Personality
Mwisho napenda kutoa shukrani zangu kwa wadhamini wetu ambao ni TBL kupitia kinywaji chao cha Redds Original,Star Tv na Giraffe Hotel
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI

DROO YA PILI YA SHINDA NOAH YAFANYIKA, WASHINDI WAZIDI KUPATIKANA




Mshindi wa Kompyuta aina ya Dell, Rehema Kigadye wa Tegeta akiwa amepozi na zawadi yake.
DROO ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Noah inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi leo imewapata washindi wengine katika Viwanja vya Karume, jijini Dar.
Meneja mkuu wa Global, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa papo kwa papo.
Washindi waliopatikana katika droo hiyo na kujinyakulia zawadi tofauti ni, Rukia Vitali wa Boko, Dar (TV Flat Screen), Leah Andrew wa Mwananyamala (Simu aina ya Samsung Galaxy), Rehema Kigadye wa Tegeta (Jezi) huku wengine wakijinyakulia zawadi za papo kwa papo (kama wanavyoonekana pichani).
Mfanyakazi wa Global, Jimmy akimwelekeza mshiriki namna ya kujiunga kwenye shindano.
Droo ikichezeshwa.
Afisa Masoko wa Global, Benjamini Mwanambuu (kulia) akimkabidhi zawadi ya T- shirt mmoja wa washiriki waliojitokeza.

(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA KIWANDA CHA KUSINDIKA TANGAWIZI MAMBA MIAMBA


 Rais Jakaya Kikwete akiangalia chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda cha kuzalisha Tangawizi kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mambakatika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
Rais
Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi,
kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda wakati amkaribisha kufungua kiwanda cha kusindika Tangawizi.
 Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda  na Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda
 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi langop kuu la Kiwanda hicho.
 Rais Jakaya Kikwete akikagua uzalishaji wa Tangawizi mara baada kufungua rasmi kiwanda cha kusindika Tangawizi kinacho milikiwa na Ushirika wa wakulima wa Tangawaizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda (kushoto) juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 Rais Jakaya Kikwete akioneshwa chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa .Kushoto  ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda akimpa maelezo  juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 Rais Kikwete akisalimina na wananchi wa rika mbalimbali waliofurika katika uiwanja wa michezo wa Goha kata ya Mamba Miamba kumsikiliza.
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti cha shukrani Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kwa kufanikisha ujenzi wa Kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Rais Kikwete alifungua kiwanda hicho juzi.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecelaakizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kabla ya Rais Kikwete kuhutubia hadhara hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Kata ya mamba Miamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.