Tuesday, December 31, 2013

MABONDIA WATAMBIANA KUMALIZA UBISHI DESEMBA 31 MSASANI KLABU




Bondia Joshua Amukulu kushoto kutoka Kenya akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho wakati wa upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Kalama Nyilawila kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Maokola  baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Miyeyusho akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake  Joshua Amukulu kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO AKIOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE NA MKENYA JOSHUA AMULU UTAKAOFANYIKA DESEMBA 31 KATIKA UKUMBI WA MSASANI KLABU PICHA ZAIDI TEMBELEA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class 'king Class Mawe'  kushoto akitunishiana misuli na Mustafa Dotto  baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Desemba 31 siku ya jumanne katika ukumbi wa Msasani klabu  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE AKIP[IMWA AFYA
 IDDY MNYEKE AKIPIMWA AFYA YAKE

TASWA FC KUPAMBA BONANZA LA TWANGA PEPETA LA MWAKA MPYA VIWANJA VYA LEADERS CLUB




Na Leca Kimaro, Dar
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC kesho itapambana na timu inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars (Twanga FC) katika mechi malaum ya kukaribisha mwaka mpya.
Mechi hiyo imepangwa kwenye viwanja vya Leaders Club inatarajia kuwa na msisimko wa aina yake ambapo baada ya mechi hiyo, bendi ya African Stars itatumbuiza jukwaani kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mechi hiyo itaanza saa 7.00 mchana ili kutoa nafasi kwa wanamuziki wa Twanga pepeta kupanda jukwaani kutumbuiza nyimbo zao mbali mbali ikiwa pamoja na mpya mbali mbali zitakazosikika kwa mara ya kwanza.
Alisema kuwa wameamua kucheza na Twanga Pepeta kutokana na ushindani uliopo ambapo katika mechi ya mwisho, Taswa FC ilishinda kwa mabao 3-1. Alisema kuwa ushindani wa timu hizo mbili ndiyo umepelekea kufanyika kwa mechi hiyo ambapo awali, timu ya kombaini ya Jogging itapambana na timu ya makempu ya Twanga pepeta.
Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani alisema kuwa kiburudani wamejiandaa vizuri na wanamuziki wake wamepania vilivyo kuanza mwaka vyema ili kutoa burudani ya aina yake. “Hii ni sehemu ya zawadi ya mwaka mpya na wanamuziki wamepania kupiga nyimbo zote zilizotamba mwaka 2013 na pia watakaribisha maombi maalum ya nyimbo kutoka kwa mashabiki.
“Tuna albamu nyingi na nyimbo kibao zilizotamba, hivyo ni wakati wa mashabiki kufanya kile wanachokitaka kutoka katika bendi yetu, wamepewa fursa hiyo nasi tupo kambili kutimiza maombi yao,” alisema.

SHEREHE ZA RAIS KIKWETE KUKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA




 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya mwisho ya Katiba mpya, Dar es Salaam leo baada ya kumaliza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi. Picha ya chini:Warioba akimkabidhi Rasimu ya Katiba, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

 Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete (kulia), akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
 Viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.

KONYAGI YAFANIKISHA FAINAL ZA KAWABWA CUP




meneja wa masoko wa kampuni ya Konyagi Joseph Chibehe,(Kulia) akimkabidhi kepteni wa timu ya Mwambao Selemani Lugono baada ya timu hiyokuibuka washindi wapili katika ligi ya kawambwa cup iliyomalizika Mjini Bagamoyo mwishoni mwa wiki Wanaoshuhudiakutokakulia ni Mbunge wa jimbo hilo Dr Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa BMT Idi KIpingu

Monday, December 30, 2013

KONYAGI YAFANIKISHA FAINAL ZA KAWABWA CUP

meneja wa masoko wa kampuni ya Konyagi Joseph Chibehe,(Kulia) akimkabidhi kepteni wa timu ya Mwambao Selemani Lugono baada ya timu hiyokuibuka washindi wapili katika ligi ya kawambwa cup iliyomalizika Mjini Bagamoyo mwishoni mwa wiki


Wanaoshuhudiakutokakulia ni Mbunge wa jimbo hilo Dr Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa BMT Idi KIpingu

Sunday, December 29, 2013

CLOUDS MEDIA GROUP YAVURUGWA 3-1 NA TIMU YA MAKIPA WANAOCHEZA LIGI KUU



 Mbwiga Mbwiguke (kushoto), akichuana na Hussein Sharif.
 Mbwiga Mbwiguke (kushoto), akichuana na Hussein Sharif.

 Wachezaji wa timu ya Clouds Media Group wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mtanange wa kufunga mwaka dhidi ya timu ya magorikipa wanaocheza Ligi Kuu ya soka tanzania Bara.
 
 Wachezaji wa timu ya Makipa wanaocheza Ligi Kuu wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Makurumla jijini Dar es Salaam.
 Mchezajki swa timu ya Makipa, Ivo Mapunda akisalimiana na Shaffih Dauda.
 Kikosi cha Clouds Media Group
 Timu ya Makipa wa Ligi Kuu wakiwa katika picha ya pamoja.

 Mchezaji wa timu ya Makipa Shaban Kado akimiliki mpira huku Bakari Masuli (kulia) akijaribu kumzuia.
Said Saleh 'Mbwiga Mbwiguke' (katikati) akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Ivo Mapunda. 
"Huchukui mpira hapa,mwenzio nilianzia huku kabla ya kuwa nyanda"Ivo Mapunda huo akifanya yake.

MWAMBUSI: YANGA, SIMBA , AZAM AFADHALI NIMEKUTANA NAZO, TIMU ZA KENYA, UGANDA SIJUI MUZIKI WAKE KOMBE LA MAPINDUZI


1a3Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi (katikati), akiwapatia maelekezo vijana wake Hassan Mwasapili (kushoto) na Peter Richard (kulia)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
KLABU ya Mbeya City Kwa mara ya kwanza inakutana na timu kutoka nje ya Tanzania ambazo zitashiriki michuano ya Mapinduzi inayotarajia kuanza kushika kasi januari mosi mwakani katika Uwanja wa Amaan mjini Unguja na Gombani kisiwani Pemba.
Klabu hii imepanda ligi kuu msimu huu na tayari imeshaonesha kiwango cha juu kwa kuziwekea ngumu timu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc , na kumaliza ngwe ya kwanza  ligi kuu ikijikusanyia pointi 27 katika nafasi ya tatu bila kupoteza mchezo wowote.
Mbeya City wanakwenda Zanzibar huku wakijua wazi kuwa wanakwenda kukabiliana na changamoto kubwa tatu.
Moja; wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hii mikubwa tangu kuanzishwa kwao.
Pili; wanakwenda kukutana kwa mara ya kwanza  na timu za Kenya , Uganda zenye wachezaji wanaocheza mazingira tofauti na ligi kuu Tanzania bara.
Tatu; wanakwenda kukutana na timu za visiwani Zanzibar kwa mara ya kwanza.
Ukiangalia mambo haya matatu, utagundua kuwa Mbeya City ni wageni wa kila kitu kuelekea mashindano haya.
Lakini ni nafasi yao kuoenesha ubora wao kama walivyofanya ligi kuu. Pia itasaidia kupima uwezo wa wachezaji wao mbele ya timu ngeni kabisa machoni kwao.
Itakuwa changamoto mpya kwa wachezaji wa Mbeya City,  ambapo wengi wao ni vijana wanaochipukia katika soka la ushindani.
Ukitazamana timu zenye majina makubwa mfano URA, Tusker,  AFC Leopard , KCC, Simba, Yanga, na Azam fc, Mbeya City imekutana na timu tatu tu yaani Simba, Yanga na Azam fc kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Na ndipo kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi anakiri wazi kuwa michuano hii ni migumu kwake, hivyo ameichukulia uzito wa hali ya juu.
IMG_2090Kikosi cha Klabu ya Mbeya City
Ili kukabiliana na changamoto mpya, Mwambusi alisema atatumia kikosi cha kwanza  kupima uwezo wa wachezaji wake mbele ya wachezaji wa kimataifa kwa lengo la kujiridhisha kabla ya kuanza mzunguko wa pili ligi kuu.
“Tunaenda kushiriki kwa mara ya kwanza. Vitu vingi sisi ni wageni, lakini naamini maandalizi yetu yatatupatia mafanikio. Mwenyezi Mungu akitupa uzima, tutawasili Zanzibar desemba 31”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi alisema uwepo wa Simba sc, Yanga na Azam fc sio tatizo kwao kwani afadhali wameshakutana ligi kuu, lakini changamoto kubwa ni timu ngeni kutoka Kenya na Uganda .
Hata hivyo, Mwambusi aliongeza kuwa timu za Tanzania bara zimeongeza wachezaji wapya , hivyo wataongeza kasi  tofauti na mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.
Yanga wameongeza nguvu kwa kumsajili Kipa, Juma Kaseja, Kiungo, Hassan Dilunga , na mshambuliaji , Mganda Emmanuel Okwi
Michuano iliyopita, Yanga haikushiriki kwani kwa wakati ule ilikuwa na ziara nchini Uturuki (Barani Ulaya) kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ambao waliishia kutwaa ubingwa na kuivua Simba sc.
Kwa upande wa Simba,  nao wameongeza wachezaji wapya katika dirisha dogo ambao ni Uhuru Selemani, Ivo Mapunda, Ali Badru, Awadh Juma, Donald Mosoti na Yaw Berko.
Azam fc wao hawakuona haja ya kuongeza wachezaji wengi, lakini wamemsajili mshambuliaji mmoja kutoka nchini Ivory Coast, Mouhamed Kone, hivyo kuongeza kasi  zaidi katika safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Kipre Tchetche pamoja  na nahodha John Bocco, `Adebayor`.
Mabadiliko hayo katika vikosi vya timu hizi za Bara yanampa shida kocha Juma Mwambusi kwani ni wachezaji mahiri, lakini ametamba kuonesha kandanda bora kama kawaida yao.
Timu za Azam fc, Simba sc na Yanga zimeshatangaza kushuka na vikosi vyao vya kwanza  “full nondo”  kwa lengo la kupima uwezo wa wanandinga wao.
Tofauti na Simba, Mbeya City ambazo malengo yao ya kushiriki mashindano hayo ni kuandaa vikosi kwa ajili ya ligi kuu, klabu za Yanga , KMKM na Azam fc zitayatumia mashindano haya kuandaa vikosi vyao kwa ajili ya michuano ya ligi kuu na  kimataifa barani Afrika.

MH. SUMAYE ACHANGISHA MILIONI 225 UJENZI WA UKUMBI, KANISA KATOLIKI MAWELA


Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza katika harambee ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kanisa katoliki Parokia ya Maonano Mawela jana.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye pamoja na mshereheshaji wa shughuli hiyo Godwin Gondwe wakijadiliana jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya harambee ya Ujenzi wa ukumbi huo wa kisasa Anthony Komu.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami kuchangia katika harambee ya Ujenzi wa Ukumbi wa kisasa katika kanisa katoliki Parokia ya Maonano Mawela .

Lowassa na Makamba, Hizi Fedha Mnazogawa Mnazitoa Wapi?



-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?



-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?

MSONDO NGOMA WAENDEREA KUITEKA TTC CHAN'GOMBE

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani kwa mashabiki walioudhulia onesho lao lililofanyika TTC Chang'ombe jumamosi kutoka kushoto ni Eddo Sanga,Othumani Kambi , Shabani Dede na Hasani Moshi Picha na www.burudan.blogspot.com
Wapuliza ara wa bendi ya Msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao kutoka kushoto ni Shabani Lendi,Hamisi Mnyupe na Romani Mng'ande picha na www.burudan.blogspot.com
Wapiga magita wa msondo ngoma wakifulumusha magita hayo wakati walipokuwa wakitoa burudani kutoka kushoto ni Abdul Ridhiwani na Mustafa Pishuu picha na www.burudan.blogspot.com

BONDIA MOHAMED MATUMLA ATIMKA NA BODABODA YAKE



BONDIA Mohamed Matumla akiwa amepanda pikipiki yake baada ya kukabidhiwa

Promota wa mpambano wa masumbwi Kaike Siraju katikati akimwinua mkono juu bondia Mohamed Matumla baada ya kumkabidhi pikipiki yake kwa kumshinda Nasibu Ramadhani wakati wa sikukuu ya krismas na kuibuka na bodaboa hiyo kushoto ni Baba wa bondia huyo Rashidi Matumla na wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa G S Group Limited wasambazaji wa pikipiki ya Haojue ambao wametoa pikipiki hiyo,Bruce Shi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa mpambano wa masumbwi Kaike Siraju katikati akimpongeza bondia Mohamed Matumla baada ya kumkabidhi pikipiki yake kwa kumshinda Nasibu Ramadhani wakati wa sikukuu ya krismas na kuibuka na bodaboa hiyo kushoto ni Baba wa bondia huyo Rashidi Matumla na wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa G S Group Limited wasambazaji wa pikipiki ya Haojue ambao wametoa pikipiki hiyo,Bruce Shi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Meneja Mkuu wa G S Group Limited wasambazaji wa pikipiki ya Haojue ambao wametoa pikipiki hiyo,Bruce Shi akimpongeza bonia Mohamed Matumla baaa ya kumkabidhi bodaboda hiyo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

TAN COMMUNICATION MEDIA YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU



DSCF1967Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akimkabidhi Mlezi mkuu wa kituo cha Moshono Fundation msaada katika kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo jijini Arusha juzi tarehe 26/1213 katika viwanja vya Matongee  Carnivo.
DSCF1941
KAMPUNI ya Tan Communication media imetoa misaada ya chakula yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili kupitia kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo kumi jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa chakula cha pamoja  cha mchana jana Meneja mbunifu wa kampuni hiyo Vicky Mwakoyo alisema kuwa lengo ni kuwafariji watoto hao ambao jamii ya watanzania imewasahau.
Mwakoyo alisema kuwa  watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwajali watoto yatima ikiwa ni pamoja na kutenga muda wao kukaa  na kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ili wasijione kama ni wapweke na wameachwa peke yao.
“Watoto wote ni sawa na watoto hawa hawajapenda ni mapenzi ya Mungu hivyo tunawajibu wa kutenga muda wetu na kukaa na watoto hawa kama hivi leo unaona wamefurahi kama watoto wengine wenye wazazi”alisema Mwakoyo
Aidha aliongeza kuwa ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kuwasaidia watoto hawa na isiishie misimu ya kipindi cha sikukuu tu kwa kuwa wanamahitaji ya chakula kila siku.
“Naomba niiombe serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto kuangalia namna ambavyo inaweza kushirikiana na vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia fungu ili kupunguza ukali wa maisha katika vituo hivyo kwa kuwa vina mchango mkubwa kwa taifa”alisema meneja huyo
Tukio hilo liliofanyika katika viwanja  vya  Matongee  Carnivo  limewakutanisha watoto Yatima zaidi ya Mia moja na hamsini ambapo walipata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali kama kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia,mashindano ya kula na kuimba muziki.
Vituo hivyo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na Bethlehemu,Moshono Foundation,Tumain,Mama na Watoto,St.Joseph,Camp Mosses,Kambarage Lemara na Karama.

MISS TANZANIA 2013 AWAFARIJI WATOTO YATIMA



 

Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa ( kushoto) akipinga hodi ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika Kituo cha kuleta watoto yatima Mgolole cha Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro , ambapo alifuatana na warembo wengine wawili, Miss Tanzania mshindi wa tano, Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013, wazazi wake na Viongozi wa juu wa Kamati ya Miss Tanzania na kupokelewa na Mama Mkuu wa Kituo hicho, Sista Flora Maria Chuma ( mwenye kutabasamu ) Desemba 25, mwaka huu walipotembelea kwa ajili ya kutoa zawadi ya vyakula vya aina mbalimbali ikiwa ni mpango wake wa kusaidia makundi ya aina hiyo.

Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa ( kulia) akimkabidhi kopo la maziwa Mama Mkuu wa Kituo cha kuleta watoto yatima Mgolole cha Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro ,Sista Flora Maria Chuma ( kushoto) Desemba 25, mwaka huu walipotembelea kutoa zawadi ya vyakula vya aina mbalimbali kwa Kituo hicho ikiwa ni mpango wa kusaidia makundi ya aina hiyo akiambatana na warembo wengine wawili, Miss Tanzania mshindi wa tano, Elizabeth Perty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013, wazazi wake na Viongozi wa juu wa Kamati ya Miss Tanzania.

Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa ( kushoto) akiwa amempataka mikononi mtoto yatima Happiness, akiwa na warembo wengine wawili, Miss Tanzania mshindi wa tano, Elizabeth Perrty, ( kulia) na mwezake Sabra Islam Miss Morogoro 2013, na Viongozi wa juu wa Kamati ya Miss Tanzania, akiwemo Mkurugenzi Hashim Lundega, wakisikiliza maelezo ya Mama Mkuu wa wa Kituo cha kuleta watoto yatima Mgolole cha Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro ,Sista Flora Maria Chuma ( hayupo pichani ) ,Desemba 25, mwaka huu walipotembelea na kutoa zawadi ya vyakula vya aina mbalimbali kwa Kituo hicho siku ya sikukuu ya Christimas ikiwa ni mpango wake wa kusaidia makundi ya aina hiyo.

THABIT ABDUL AACHANA NA MASHAUZI CLASIC AIBUKA NA BENDI YAKE YA WAKALI WAO, KUZINDULIWA PASAKA


Mwanamuziki mkali wa kuandaa na kupangilia muziki mwenye uwezo wa kupiga ala zote za muziki, kama, Kinanda, Gitaa zote yaani Solo, Bass na Rhythim, na zaidi katika kukaanga 'Chips', kuzicharaza drams, Thabiti, Abdul, ameamua kuachana na kazi za kutumwa na badala yake ameamua kuunda kundi lake jipya la Taarab, linalokwenda kwa jina la Wakali wao.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Thabit, alisema kuwa kundi lake hadi sasa lina jumla ya wasanii 13, na linaendelea na mazoezi yake maeneo ya Kinondoni katika ukumbi wa Way Bar ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuandaa albam yao ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne.

Aidha alisema kuwa katika bendi hiyo iliyo chini ya Meneja wake, Godfrey Ngowi, hadi sasa imekwishaanza kufanya shoo katika baadhi ya maeneo huku ikiwa na waimbaji wengi wapya yaani Ma Under Ground, na wapiga vyombo aliowataja kwa majina kuwa ni Jumanne Ulaya, anayepiga solo, Shomari Zizu, anayepiga Gitaa la Bass, Omary Alli na Ndage Ndage, wanaopiga Kinanda.

Bendi hiyo inatarajia kutambulishwa rasmi mwezi Februari na kuzinduliwa ramsi mwezi wa nne katika Sikuku ya Pasaka, ambapo itazinduliwa rasmi bendi hiyo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Video zake, Albam na Vyombo vipya, ambapo kila shabiki atakayeingia getini atapatiwa Cd moja ya Audio yenye nyimbo za bendi hiyo.

Thabiti, alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Kalieni Viti Sio Umbea, Lipo Linalo Kusumbua, Mtu Mzima Hovyo na Subira Haina Kikomo.

ZAIDI BOFYA www.sufianimafoto.com

Rais Shein wa Zanzibar katika Mahafali ya 9 ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamuhuna,wakati alipowasili Chuo Kikuu cha Taifa,kampasi ya Tunguu,katika sherehe za mahfali ya 9 ya chuo hicho,ambayo wahitimu wa fani mbali mbali wamepatiwa Shahada,Stashahada na Vyeti.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,akisalimiana na walimu wa Chuo Kikuu cha SUZA,alipowasili katika mahfali ya 9 yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja, leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,(wa pili kulia) akiongoza maandamano wakati wa sherehe za mahfali ya 9 chuo hicho,yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja leo,yaliyowashirikisha baadhi ya wahitimu na walimu