Friday, February 28, 2014

MASHINDANO YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA ILALA WAPATA MAFUNZO


Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kushoto akifafanua jambo wakati wa mafundisho ya uchomaji nyama bora kwa wachoma nyuma wa bar mbalimbali za Ilala

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kushotoakijibu maswali mbalimbali ya kuhusu uchomaji wa nyama kwa njia ya kitabu alichonacho kwa ajili ya uchomaji nyama bora

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akimkabidhi cheti Richard Mushi kwa ajili ya kushiliki semina ya uchomaji mzuri wa nyama

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akimkabidhi cheti Mary Komba kwa ajili ya kushiliki semina ya uchomaji mzuri wa nyama

Baadhi ya washiliki walioshiliki katika semina ya uchomaji nyama wakiwa katika picha ya panmoja

KAMPENI ZINAVYOENDELEA JIMBONI KALENGA



Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrfod Slaa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni wa uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Juu na chini Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni juzi.

Wananchi wa kijiji cha Kiwele wakiitikia moja ya salama za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho za uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega akisalimiana na mmoja wa wazee wa kijiji cha Kiwele, baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo juzi.

DR.MAGUFULI AKAGUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM: BARABARA YA KIMARA HADI KIVUKONI KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI SITA


Waziri wa Ujenzi Dr.John Pombe Magufuli Kituo cha BRT kivukoni jijini Dar es salaam leo akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
 Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyekaa kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe (katikati) pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale (aliyesimama) wakisafiri kwa basi kukagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa DART Asteria Mlambo (kulia) akimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki anayefuatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kuegesha mabasi ya haraka kinachojengwa eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari (aliyeshika kijiti) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam  

Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza. 

 Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu. 

 Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.  Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280. 

 Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo. 
 Waziri Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyokusudiwa. 

“Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo wake” alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara kinyume na sheria. 

 Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu. 
“Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa visingizio vya kutokamilika kazi hii kwa wakati” ametahadharisha Mhe. Magufuli. 

 Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara hiyo upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa eneo kati ya Ubungo na Kiamara. 

 Naye Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa haraka utajengwa katika awamu sita.  Awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu unaoendelea inahusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni – Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha kamilisha asilimia 55 ya mradi

BENKI YA DUNIA 'YABANA' MSAADA KWA UGANDA


Benki ya dunia.
Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.

Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
CHANZO NI BBC SWAHILI

Thursday, February 27, 2014

SAFARI NYAMA CHOMA YATOA MAFUNZO KWA BAR ZA TEMEKE


Supervisar Onesmo Swilla akizungumza na wauzaji wa nyama choma wa bar mbalimbali za Temeke Dar es salaam

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akionesha vifaa vya kupimia joto chakula wakati wa mafunzo kwa wachoma nyama wa bar za Temeke

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akipima nyama iliyokuwa tayali kwa ajili ya kuliwa wakati wa mafunzo hayo

Baadhi ya wachoma nyama wa TEmeke

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya nyama choma Carpar Kimario baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika kilwa road pub Dar es salaam

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya nyama choma Chavalimembe Lutambi baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika kilwa road pub Dar es salaam

Jaji mkuu wa shindano la Safari lager nyama choma Lawrence Salvi kulia akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya nyama choma Jerome Kavishe baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika kilwa road pub Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya nyama choma wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo yao

NMB YASOGEZA HUDUMA KARIBU ZAIDI NA WAKAZI WA BARABARA YA MANDELA



Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Bw. Meck Sadick akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road .Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam ,Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni  Mkuu  wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa  NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.

NMB yazindua tawi jipya barabara ya Mandela mkoani Dar es Salaam.Hili ni tawi la ishirini  na tatu kufunguliwa katika mkoa wa Dar es Salaaam, na hii inafanya NMB kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania, ikiwa na matawi zaidi ya 150 yaliyosambaa nchi nzima.


Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay akimwelezea  Mheshimiwa Mmkuu wa mkoa wa Dar es salaam (kwanza kushoto ,Bw. Meck Sadick huduma mbali mbali zitolewazo na tawi jipya la NMB mandela Road


Tawi hili la NMB Mandela Road, linatoa huduma mbali mbali za kibenki ikiwemo akaunti za akiba, mikopo , huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipia kwa niaba  ya serikali na taasisi mbalimbali. Tawi hili litakua wazi kila  Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili  na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi - 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Bw.Meck Sadick (kwanza Kushoto akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.


Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya. Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 



Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick (pili kulia kwenye viti) akiwa kwenye picha ya Pamoja na maafisa wa NMB tawi la Mandela Road.

MWILI WA BALOZI FULGENCE KAZAURA WAAGWA LEO KATIKA KANISA LA MT. PETER JIJINI DAR


Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura likiwa ndani ya Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam tayari kwa Ibada maalum ya kumuombea Marehemu huyo iliyofanyika mchana wa leo kanisani hapo.
Viongozi wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala (mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.Ibada hii ya kuaga mwili wa Balozi Kazaura imefanyika mchana wa leo katika Kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji Mjane wa Marehemu pamoja na watoto wakati wa Ibada maalum ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Peter,Osterbay jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.

Airtel yadhamini Tuzo ya Mwanamakuka 2014

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  leo imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamakuka zenye lengo la kusaidia wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali kujiinua kiuchumi

Tuzo za Mwanamakuka zinaandaliwa na The Unity of Women friends kila mwaka zikiwatambua wanawake jasiri waliopambana kubadili maisha yao kutoka katika hali ngumu, duni na umaskini

Akiongea kuhusu udhamini wa Tuzo hizo Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Airtel inaamini kwamba ujasiriamali ni muhimu katika kufikia maendeleo ya kiuchumi na kuondoa umaskini. Kwa kudhamini tuzo hizi za mwanamakuka tunajikita katika kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuwa sehemu ya shughuli za maendeleo ya wanawake nchini”.

Kwa miaka mitatu mfululizo Airtel tumekuwa moja ya wadhamini wa tuzo hizi za mwanamakuka ambazo zimebadili maisha ya wanawake na kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutaendelea kuonyesha dhamira yetu katika mipango ambayo itasaidia wanawake walio katika mazingira magumu kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa."

Jane aliongeza kwa kusema , kuna msemo unaosema ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima. Airtel tumejipanga kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewezesha jamii kwa ujumla

Kwa upande wake mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema” Tunashukuru Airtel kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha tuzo hizi ambazo ushirika huu umekua wa mafanikio makubwa. Lengo la tuzo hizi ni kuwahamasisha na kuwavutia wanawake  kufikia ndoto zao. Lakini hasa tuna hakikisha kuwa zoezi hili na matokeo yake yanaleta mafanikio ya kudumu na kubadili maisha yao”

 Tuzo za mwanamakuka za mwaka huu zitafanyika sambamba na kusherehekea siku ya wanawake Dunia, Mwanamakuka family bonanza itafanyika tarehe 15 machi 2014 , siku ya Jumamosi katika viwanja vya Escape 1 Dar es Saalam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 2 Usiku.

27 warejesha fomu Uchaguzi wa Taswa, Shafii Dauda 'achomoa'


Shafii Dauda aliyeshindwa kurejesha fomu ya uchaguzi wa Taswa
JUMLA ya waombaji 27 kati ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.

Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.

Mhazini Msaidizi ni Elius John Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija Richard Shija na Mohamed Salim Mkangara.

Katibu Msaidizi ni Alfred Lucas Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Patrick Raymond Nyembera. Katibu Mkuu ni Amir Ally Mhando pekee.

Waombaji nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed Omary Masenga. 
Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John Ishabairu, Juma Abbas Pinto.

Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Shaffih Kajuna Dauda hakurudisha fomu kwa madai ya kubanwa na moja ya vipengele vya katiba ya chama hicho na yeye ameonyesha kuridhika kujiweka kando bila kinyongo.

Titina wa Extra Bongo ajiandaa kuacha kunengua


Mnenguaji Titi Mwinyi 'Titina' akiwa katika pozi
MNENGUAJI mahiri wa bendi ya Extra Bongo, Titi Mwinyiamir maarufu kama 'Titina' amesema anajipanga kuachana na fani hiyo baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 10.
Akizungumza na MICHARAZO, Titina aliyewahi kutamba na Double M Sound, Twanga Pepeta na FM Academia, alisema anataka kuachana na fani hiyo ili kujikita kwenye uimbaji.
Titina alisema muda aliotumika kama dansa tangu mwaka 2000 umeufanya mwili wake kuchoka na sasa anadhani ni muda muafaka kuhamia kwenye uimbaji ili kuendeleza kipaji alichonacho.
"Natarajia kuachana na unenguaji ili nijikite kwenye uimbaji, kipaji hicho ninacho tangu utotoni sema kunengua kuliniathiri na kukisahau, ila sasa sina jinsi zaidi ya kukiendeleza," alisema.
Dansa huyo alisema tayari ameanza mazoezi ya kuimba ili akiwiva vyema ahamie huko kufuata nyazo za akina Tshallah Mwana na Mbilia Bel waliowahi kutanga kwenye unenguaji kabla ya kuhamia kwenyue uimbaji na kuishika Afrika.
Titina, alisema anaamini bidii yake katika kujifunza kuimba kwa sasa ndiko kunakoweza kumfikisha pale walipofikia wakali hao kutoka Kongo au baadhi ya wanamuziki wa kike wanaotamba nchini kama akina Luiza Mbutu na wengine ambao walianzia kwenye unenguaji kabla ya kuwa waimbaji.

ZIARA YA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI TBL DAR



 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia) akielezea utendaji wa kampuni hiyo, wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea  Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
 Robin akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Habari Leo, Joseph Kulangwa
 Wahariri wa Vyombo vya Habari wakitembelea eneo la upikaji bia wakati wa ziara yao iliyofanyika  kwenye Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam
 Mtalaam wa Upishi Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benjamin Budigida akitoa maelezo ya jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia njia ya kisasa ya kompyuta  wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
 Meneja wa Usimamizi wa Ubora wa Bia wa TBL, Conchesta Ngaiza (kulia) akielezea jinsi wanavyodhiti ubora wa bia.
 Wahariri wa Vyombo vya Habari wakitembelea idara ya uchachuaji wa bia wakati wa ziara yao iliyofanyika  kwenye Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam
 Fundi wa Upishi Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benjamin Budigida akitoa maelezo ya jinsi bia inavyochujwa  wakati wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea juzi Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam.
Mhariri kutoka Gazeti la Mwananchi, Rashid Kejo akifurahia kupata zawadi yake
 Joseph Kulangwa wa Gazeti la Habari Leo, Joseph Kulangwa akipatiwa zawadi
 Mhariri wa  Gazeti la Uhuru, Jane Mihanji akipokea zawadi ya bia baada ya kumaliza ziara TBL
 Meneja Mawasiliano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Orio akifafanua jambo mbele ya wahariri
 Wahariri wakiwa katika picha ya pamoja a viongozi wa TBL wakati wa ziara hiyo
                  Rashid Kejo wa gazeti la Mwananchi akipokea zawadi ya bia baada ya ziara
Wahariri wakizuru Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam