Thursday, July 31, 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE SIKU YA IDDI PILI


Bondia Sadick Nuru kushoto akioneshana umwamba na Baraka Mchonge wakati wa mpambano wao ulifanyika Mazese Dar es salaam wakati wa sikukuu ya iddi pili Nuru alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Stevin Kobelo kushoto akirusha ngumi kumpiga Karim Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara park manzese Dar es salaam mpambano huo walitoka droo ya kufungana point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Joseph Gili kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa manyara park manzese Dar es salaam Tamba aklishinda kwa T.K.O  ya raundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach .blogspot.com
Bondia Julius Kisalawe kushoto akipambana na Ramadhani Kumbele wajkati wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam Kumbele alishinda kwa point na kufanikiwa kuchukua ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point kushoto ni Refarii Ally Bakari picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Diamond Platnumz arejea nchini na tuzo yake



 
 Diamond Platnumz  akionesha tuzo yake aliyoshinda kwa baadhi ya vyombo vya habari  na mashabiki waliofika kumlaki,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.
 Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnumz akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.Pichani akilakiwa na Mama yake Mzazi na baadhi ya washabiki na wapenzi wa muziki huo.
 Diamond Platnumz akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014. 

MATUKIO KATIKA PICHA MASHINDANO YA DANCE MIA MIA DON BOSCO OYSTERBAY WIKI ILIYOPITA


 Vijana wakionyesha umahiri wao wa kuchezea Baiskeli wakati wa mashindano ya Dance Mia mia, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Don Bosco Oysterbay wiki iliyopita.
 Kundi kutoka TMK, likishamblia jukwaa.
 Kundi kutoka Kigamboni, likishambulia jukwaa.
 Kundi lililoonyesha kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo.
 Si Kung Fu bali ni Dance Mia mia......
 Michezo ya Baiskeli....

Wednesday, July 30, 2014

MPAMBANO WA NGUMI ULIVYOFANYIKA MBEZI SIKU YA IDDI


Bondia Nenge Juma kushoto akipambana na Said Mohamed wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya sikukuu ya iddi mosi mbezi mwisho juma alishinda kwa TKO ya raundi ya tatu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Lugano Mwaikambo akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Michael Chinyama wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya sikukuu ya idi mosi mbezi mwisho jijini Dar es salaam Chinyama alishinda kwa point picha  na www.superdboxingcoach.blogspot.com

SIMANZI ZAENDELEA KUTAWALA NDANI YA NYUMBA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT)


Jaji Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
  Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo LUGHA GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa mwanzoni mwa wiki.
 Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago akifunika uso wake kwa kutoamini kuwa ameponea kwenye tundu la sindano kutokana na kuondolewa katika maumivu ya Jua la Utosi na kuendelea na mashindano hayo
 Mshiriki Wa TMT, Moses Obunde (Mwenye Suti) akimpongeza Mshiriki Mwenzie Mzee Kapalata Mtawa kwa kuweza kuondolewa Kwenye Jua la Utosi na Kupelekwa Kivulini katika Shindano la TMT linaloendelea.
 Washiriki walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.
 Simanzi Zikianzia hapo sasa mara baada ya Washiriki kupunguzwa ili apatikane mmoja wa kuondoka
 Wakabaki wawili na hatimaye mmoja kati ya hao aliweza kuondolewa katika mashindano hayo
Baadhi ya Washiriki wa TMT wakimuaga Mshiriki mwenzao Pendo Edward (Katikati) ambaye aliweza kutolewa kwenye mashindano kutokana na kura kuwa chache.Picha Zote na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatua ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia wiki ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano hilo wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti wake na uzuri wake pia.
Mshiriki mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza  kuchomwa na jua la utosi lililompelekea kutoka kwenye shindano hilo kubwa la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo mpaka sasa washiriki kumi na tano (15) ndio wamebaki katika nyumba ya TMT na hali ya simanzi bado inaendelea katika nyumba ya TMT kwa wiki hii ambapo mshiriki mwingine atatakiwa kutoka.
Shindao la TMT limekuwa likivuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje ya Tanzania kutokana na Utofauti wake na ubora wake na kupelekea watanzania wengi sana kufuatilia shindano hilo kwa ukaribu na umakini zaidi.
Hatimaye wiki hii Tanzania Movie Talents iliamua kuzindua Zoezi la kuwapigia kura washiriki wake kupitia ukurasa wetu wa facebook ambapo sasa watanzania na wapenzi wa TMT ambao wanauwezo wa kupata na kutumia internet sasa wanaweza kuwapigia kura washiriki waliowavutia kupitia ukurasa wetu wa facebook na vilevile kuendelea kuwapigia kura washiriki kwa kutumia simu zao za mkononi.
Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678
Na Jinsi ya Kumpigia kura mshiriki kupitia ukurasa wetu wa facebook BOFYA HAPA  kwa kupata maelezo.

WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)



Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha wageni wakati alipofanya  ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA.Wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Mbwana Mbwana.Kulia ni makamu Mwenyekiti Weggoro Nyamajeje na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya TCAA ,Charles Chacha. Waziri Dk. Harrison Mwakyemba ndiyo waziri pekee  aliyetembelea ofisi hizo tangua kuanzishwa.
Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini.              
Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akisisitiza jambo kwa  Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini
Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa  na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha moja ya tuzo waliyotunukiwa Tanzania na Baraza la Usafiri wa Anga Duniani kwa kutambua mchango wa TCAA.anayeshuhudia katikati ni Makamu Mweneyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo Weggoro Nyamajeje,  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mbwana Mbwana akitoa shukrani kwa niaba ya bodi na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe, (wapilia kutoka kulia)wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi Weggoro  Nyamajeje na Kaimu Mkurugenzi wa TCAA ,Charles Chacha.
Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya wafanyakazi wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Mbwana Mbwana, wengine ni  Makamu Mwenyekiti Weggoro Nyamajeje na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Charles Chacha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wakimsikiliza kwa makini Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani)  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA.

Monday, July 28, 2014

MWANAMUZIKI ALI KIBA ATEMBELEA CHUMBA CHA HABARI CHA GAZETI LA JAMBO LEO DAR ES SALAAM LEO




 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni  ya Jambo Concepts (T), Limited, Juma Pinto (kushoto), akipokea CD yenye nyimbo mbili za Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba wakati alipotembelea ofisi za gazeti hili Dar es Salaam leo kutambulisha nyimbo hizo pamoja na kuelezea mikakati yake ya baadaye kimuziki.
 Ali Kiba alimkabidhi CD Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts (T), Limited, Benny Kisaka.
  Ali Kiba alimkabidhi CD, Mmiliki wa Blog ya Wananchi, William Malecela.
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo, Nyendo Mohamed (kulia), akimtambulisha Ali Kiba kwa waandishi wwenzake.
 Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (kulia), akimueleza jambo Ali Kiba.
 Ali Kiba akisalimiana na Mhariri wa Makala wa Gazeti la Jambo Leo, Robert Hokororo.
 Ali Kiba akisalimiana na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Neema Mgonja.
 Ali Kiba akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa.
Ali Kiba akisalimiana na Msanifu kurasa Msaidizi wa Gazeti la Jambo Leo, Hamza Mussa.Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.

BONDIA WA KIKEKE LULU KAYAGE ANAYEWAZA KUWA NA MATUMAINI KIBAO KATIKA NGUMI

Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo  anaenolewa katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchiniwww,superdboxingcoach.
blogspot.com
 
Na Mwandishi Wetu
 Ukizungumzia mchezo wa masumbwi ulivyompatia hamasa mpaka kuanza mazoezi katika kambi ya ilala ya mchezo wa masumbwi bondia Lulu Kayage anasema mchezo anaupenda na pia unamjenga kiafya na ki mwili kwani amekuwa akishiriki mazoezi tangia mwaka 2012 mwezi April na maendeleo yake ni mazuri akiwa chini ya uwangalizi wa makocha wake hawo

Bondia huyo wa kike aliyezaliwa 1990 anamatarajio makubwa ya kuwa ingwa wa dunia katika masumbwi ususani upande wa wanawake 

bondia huyo anaye vutiwa na uchezaji wa mkongwe wa masumbwi nchini Rashidi Matumla 'Snake Man'  ambapo kwa nje anavutiwa na mabondia toafauti ambapo mmoja wapo ni Mbunge wa Filpino Manny Paquaio na bondia asiyepigika ambaye kwa sasa anatumikia kifingo cha siku 90 kwa kosa la kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake
Katika mazoezi anayofanya na kambi ya Ilala ambayo wanawake wapo wawili ambapo anaendelea kujisikia faraja kwa kuwa wapo katika mazoezi pamoja kama ndugu na nidhamu ya ali ya juu iliyopo hapo katika kambi hiyo

aliwataka wanawake wajitokeze katika mchezo wa masumbwi kwani ni mchezo kama michezo mingine ambapo ata ukiangalia mchezo watu wanapopigana wakimaliza wanakubatiana kwa furaha ni kwa ajili ya kutambua mchezo wa masumbwi si uadui bali ni mchezo


Vikwazo ambavyo amewai kukutana navyo ni pamoja na kukatishwa tamaa kwa watu ambao awapendi michezo kwani wanasema mwanamke mzima unacheza ngumi uogopi kutolewa manundu kuaribiwa sura ehee uzuri wote huo hizo ni sehemu tu za watu wasiopenda michezo kwani kuna vikwazo
 vingi ambavyo tuna vipata mabondia wa kike 

kwa mara ya kwanza nilipotokea kwenye magazeti tu watu walinifata na kunishauli niachane na mchezo lakini kwa sasa nimeshaiva na nipo tayali kwa mapambano mbalimbali yatakayojitokeza

kwa kuwa mimi ni bondia bora pekee wa kike nchini na ninaetoka katika kambi bora kabisa ya mchezo wa masumbwi nchini naisi cheche zangu mtaanza kuziona mwazi agost kwa kuwa kwa sasa nipo kwenye mazoezi makari ambayo yananipa uwezo wa ali ya juu katika masumbwi 

Aliongeza kuwa kwa kufundishwa na kocha wa kimataifa Super D anaefundisha mafundisho hayo kupitia DVD zake ambazo  amechanganya na clips za mabondia mabingwa wa dunia akiwemo Manny Paquaio,floyd Mayweather, Roy Jones, Mohamedi Ali, Mike Taysoni na wengine ameziona na kuzifanyia kazi ambapo kwa sasa anajua mbinu za Ndani na nje ya nchi kutokana na Supe D kumpatia uwezo wa kina katika maswala ya mchezo wa Masumbwi Duniani

Katika mchezo uhu siwezi kukata tamaa katika mazoezi na nawambia mashabiki wa mchezo wa masumbwi watarajie mafanikio yangu katika masumbwi

NAIPONGEZA SERIKALI KUSITISHA AJIRA UHAMIAJI



Mgombea Uraisi Tucta Dismas Lyassa akijadiliana jambo na wakili wake Jebra Kambole. Picha na Mpigapicha Wetu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE



Ndugu zangu Watanzania


Asubuhi ya leo tarehe 28 Julai 2014 nilitoa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari nikiitaka Serikali kutolea ufafanuzi malalamiko yaliyojaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari. Asante Mungu kwamba Serikali imetolea majibu jambo hili kwa kusitiza ajira zote.

 Rejea taarifa yangu kwa vyombo vya habari niliyoitaka Serikali kutoa majibu katika suala hili asubuhi ya leo tarehe 28 Julai na nakala yake kutumwa katika ofisi mbalimbali za Serikali.


Nachukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuwa sikivu katika hili na huenda katika mengi yajayo, kama Rais Mtarajiwa wa Tucta baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 4-5 Dodoma, naahidi kushirikiana na Serikali hasa kama itakuwa sikivu.

Nahitaji kupatiwa majibu pia juu ya hatima ya mabaamedi wanaolazwa chumba kimoja zaidi ya kumi tena siyo katika vitanda, bali zaidi huwa wanalala chini; wanafanyakazi hadi usiku, wengine wanakoishi ni mbali na baa, hoteli nk.

Nahitaji kuona kero za walimu, wafanyakazi wa Serikali za Mitaa, madini, simu, kilimo, utafiti afya, mawasiliano, reli, bandari nk zinakomeshwa; Ni aibu hadi leo kuna walimu wanapoanza kazi  wanalala kwa walimu wakuu wakisubiri kupatiwa sehemu za kuishi, ni aibu hadi leo mwalimu anafanyakazi kazi miezi sita inapita hakuna mshahara anaolipwa…hatuwezi kwenda hivi, ni lazima majibu yapatikane.

Wafanyakazi wa Tanzania  tunapaswa kuimba nyimbo zingine, siyo za kero zile zile kila kukicha. Naamini yote yanawezekana, cha msingi ni kwa Serikali na waajiri kusimamia kwa haki mambo yote juu ya wafanyakazi. Hakuna lisilowezekana tukipigania haki.

Imetolewa leo Julai 28, 2014

                                   Na Dismas Lyassa                                  


(Mgombea Uraisi TUCTA) 
0754 49 8972/0712183282

HEKA HEKA ZA SIKUKUU YA IDDI

 WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAKIPATA MAHITAJI MBALIMBALI KABLA YA SIKUKUU YA IDDI MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO
WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAKIPATA MAHITAJI MBALIMBALI KABLA YA SIKUKUU YA IDDI

VIONGOZI WA CHUO NA HOSPITALI YA IMTU WATINGA MAHAKAMANI, DPP AWAONDOLEA MASHTAKA



 Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi 
 Wakipanda gari baada ya kusomewa mashitaka
 Wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka
 
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani. Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika kufundishia kwa Kampuni Coroner. 

 Vigogo hao ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo  saa 8:07  mchana.  Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey Lusemwa. 

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu washtakiwa wakiwa na nyadhifa  tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri, kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). 

 Magina alidai kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo baada ya kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka.
Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja. 


Hata hivyo, kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP akidai kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya kuendelea kuwashitaki. 

 Ahmed alidai kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu cha 91 kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaka. 

 Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa.

Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa. 
Alisema kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana ili wakasote mahabusu. 

 Viwanja vya mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa IMTU wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na lile. 

Kupitia magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo.