Saturday, April 25, 2015

COLECTION ZA DVD ZA MAYWEATHER NA PACQUAIO SASA ZINAPATIKANA UHURU / MSIMBAZI DAR



Na Mwandishi Wetu 

IKIWA zimesalia siku chache kufanyika mpambano wa kusisimua wa mchezo wa masumbwi Duniani kati ya bondia Floyd Mayweather na Manny Paquaio mei 2 mwaka uhu mpambano uho uliovunja rekodi ya mapato mbalimbali ya ngumi zilizofanyika kwa kipindi hichi

kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekwisha toa Coretion  DVD  za mapambano ya wakali hawo yaliyopita nyuma dvd hizo zenye mafunzo mbalimbali pamoja na mazoezi wakati wakijiandaa kupigana mpambano wao

ambao utafanyika mei 2 Super D alisema nimetoa video zao ili watu wazione pamoja na kumbukumbu zao za nyuma ambapo kila DVD moja ina mapambano manne ya bondia mmoja

ambapo ukiwa kama mpenzi au shabiki wa bondia mmojawapo unaweza kujifunza mambo mengi kupitia video hizo

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya uhuru na msimbazi Dar es salaam kituo kikuu cha mawakala wa magazeti mbalimbal;i masaa 24 zaidi unaweza kuwasiliana moja kwa moja na kocha Super D kwa namba za simu 0787406938 AU 0754406938

Tuesday, April 14, 2015

SELCOM YAMWAGA MAPESA KWA WASHINDI WA SHINDA NA SELCOM

Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori kushoto akimkabidhi mshindi wa shindano la shinda na Selcom kiasi cha shilingi laki moja Bi.Winfrida Shoo mkazi wa sinza Dar es salaam anaeshuhudia katikati ni  Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta mshindi huyu alinunua muda wa maongezi kupitia Advans Bank Mobile banking

Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori kushoto akimkabidhi mshindi wa shindano la shinda na Selcom kiasi cha shilingi laki moja Bw.Khalid Kasim mkazi wa mbagala  Dar es salaam anaeshuhudia katikati ni  Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta mshindi alinunua LUKU kwa wakala wa Selcom

Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori kushoto akimkabidhi mshindi wa shindano la shinda na Selcom kiasi cha shilingi laki moja Bw.Shafii Liumbo mkazi wa Mtoni Mtongani Dar es salaam anaeshuhudia katikati ni  Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta mshindi huyu alinunua LUKU kwa Wakala
Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori kushoto akimkabidhi mshindi wa shindano la shinda na Selcom kiasi cha shilingi laki moja Bw.Bonface Richard wa Banana Dar es salaam anaeshuhudia katikati ni  Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta mshindi huyu alinunua
 LUKU kwa Wakala
WASHINDI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

WASHINDI WALIO PATIKANA 

Friday, April 10, 2015

Safari ya Mwisho ya Mpiganaji Benard Rwebangira


Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Bernard Rwebangira likiwa tayari kwa safari ya kwenda kwenye nyumba yake ya milele kwenye Makaburi ya Kawe,Jijini Dar es salaam leo.Marehemu Bernard Rwebangira aliwahi kuwa Mpiga picha wa Kampuni ya TSN wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News pamoja na Habari leo.Mungu aiweke roho ya Marehemu mahapa pema Peponi, Amin. PICHA ZOTE KWA HISANI YA FATHER KIDEVU BLOG
Sehemu ya Ndugu wa Marehemu Bernard Rwebangira wakiwa ni wenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao, wakati wa Ibada ya kuaga mwili iliyofanyika leo Nyumbani kwao, Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
Waombolezaji wakiwa Msibani hapo.
Na hii ndio ilikuwa Safari ya Mwisho ya Mpiganaji Bernard Rwebangira kwenye Makaburi ya Kawe, jijini Dar es Salaam

Ajali mbaya yatokea katika eneo la Mbweni Mkata Handeni mkoani Tanga na kuua


Basi la Ngorika lenye namba za Usajili T770 BKW lililokuwa kitoka jijini Dar es Salaam kwenda Arusha  na lile la Kampuni ya RATCO T 274 DCP Tanga kwenda Dar es Salaam yamegongana uso kwa huso na kulihusisha gari lingine dogo aina ya Toyota Pass T 628 CXE  na kusababisha vifo vya abiria 10 na majeruhi. Ajali hiyo ilitokea eneo la Mbweni Mkata, wilayani Handeni mkoni Tanga. 

Inaelezwa kuwa basi la Ratco lilgongana kwanza na gari dogo na kisha kwenda kugongana uso kwa uso na basi la Ngorika ambapo abiria 8 walifariki katika basi hilo na wawili waliokufa walikuwa katika gari dogo wakipeleka mgonjwa hospitali.
Wakati huo huo habari kutoka Morogoro zinaarifu kuwa Basi mali ya kampuni ya Happy Nation lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya limepata ajali eneo la Kikwaraza Mikumi na kuuwa watu wawili na kusababisha majeraha kwa abiria wengine 48.
Gari dogo  lililohusika katika ajali ya Tanga na abiria wake wote waliokuwa wa familia moja kuripotiwa kufa.

SELCOM WAZINDUA UKUSANYAJI WA KODI KWA NJIA ZA KIELEKTRONIC MANSIPAA YA MOROGORO


Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kushoto akiwa na
Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori na
Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta wakati wa uzinduzi wa
mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic mkoa wa Morogoro
Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta kushoto akimwelekezaKaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bakari Sagini jinsi ya kutumia
 mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic wakati wa uzinduzi rasmi wautumiaji wa mashine hizo kwa Manspaa ya Morogoro

Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta kushoto akimwelekeza Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele jinsi ya kutumia
 mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic wakati wa uzinduzi rasmi wautumiaji wa mashine hizo kwa Manspaa ya Morogoro

Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori katikati akitoa mahelezo ya mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic wakati wa uzinduzi rasmi wautumiaji wa mashine hizo kwa mkoa wa Morogoro kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele na  Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta