Thursday, August 27, 2015

BONDIA LULU KAYAGE ATIMKIA AFRIKA YA KUSINI KUKIPIGA TENA

Bondia Lulu Kayage akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yake ya Afrika kusini kupigana mpambano mwingine agoust 28 picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Lulu Kayage akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yake ya Afrika kusini kupigana mpambano mwingine agoust 28 picha na SUPER D BOXING NEWS

Mdau wa mchezo wa ngumi nchini Hamissi Berege kushoto akizungumza na George Sabuni ambaye anambatana na bondia lulu Kayage kulia kwenda kwenye mpambano wake mwingine utakaofanyika agous 28 Afrika ya kusini picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa Kike Lulu Kayage amenda tena nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya mpambano wake mwingine na bondia mwingine kutoka uko utakaofanyika agost 28 nchini Afrika ya kusini

akiongea kabla ya kupanda ndege bondia huyo alijingamba kuwa ataenda uko na atashinda kwa kuwa yupo fiti zaidi kwa sasa

hivyo nitaendeleza wimbi la ushindi aliongeza kwa kusema anaomba duwa kwa watanzania wamuombee ili aweze kumchakaza msauzi uyo tena kwa K,O mbaya kama alivyo mpiga 

mwenzake Lizbeth Sivhag bondia huyo aliyeambatana na bondia mkongwe wa siku nyingi George Sabuni kwa ajili ya kumbumbusha mambo mbalimbali awapo uringoni

amesema kwa sasa watanzania wategemee furaha kutoka kweke kwani mchezo anaocheza ni mgumu sana na yeye amejizatiti kuleta mafanikio kwa taifa nzima la Tanzania

Tuesday, August 25, 2015

ONESMO NGOWI AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA LULU KAYAGE


Rais wa I.B.F Africa Onesmo Ngowi kulia akimkabidhi vifaa vya mchezo wa ndondi bondia Lulu Kayage baada ya kutembelea ofisi za rais huyo zilizopo posta Dar es salaam Lulu Kayage ataondoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wake mwingine kabla ya kugombania ubingwa wa I.B.F Afrika mnamo Desemba 2 mwaka uhu
Rais wa I.B.F Africa Onesmo Ngowi wa pili kulia akiwa na bondia Lulu Kayage wa pili kushoto kulia ni George Sabuni na kushoto ni Hamisi Berege
BONDIA LULU KAYAGE AKIPOZI KATIKA OFISI ZA I.B.F AFRIKA
BONDIA LULU KAYAGE AKIPOZI KATIKA OFISI ZA I.B.F AFRIKA
BONDIA LULU KAYAGE AKIPOZI KATIKA OFISI ZA I.B.F AFRIKA

Sunday, August 23, 2015

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AMDUNDA ALLY MUHURO KWA T.K.O YA RAUNDI YA TATU


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akimshambulia kwa makonde mazito Ally Muhuro wakati wa mpambano wao ulifanyika siku ya jumamosi Class alishinda kwa T.K.O ya raund ya tatu Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akimtupia konde mpinzani wake Ally Muhuro wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamos Class alishinda kwa T.K.O raundi ya tatu Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akimtupia konde mpinzani wake Ally Muhuro wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamos Class alishinda kwa T.K.O raundi ya tatu Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Rojas Massamu kushoto akipambana na Subea Chube wakati wa mpambano wao Massamu alishinda kwa K,O ya raundi ya nne Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Awadhi Faraji kushoto akipambana na Shomari Mirundi wakati wa mpambano wao Mirundi alishinda kwa .K.O ya raundi ya pili Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Kelvin Majiba kushoto akipambana na Vicent Mbilinyi wakati wa mpambano wao uliofanyika katika viwanja vya shule ya Uhuru kariakoo Dar es salaa Mbilinyi alishinda kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS




Thursday, August 20, 2015

MABONDIA KUPIMA UZITO IJUMAA KUPIGANA JUMAMOSI KARIAKOO UHURU WASICHANA

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Ally Mulo watapima uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi utakaofanyika katika viwanja vya basketball vilivyopo katika shule ya uhuru wasichana Kariakoo Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu ambaye pia ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema mabondia hawo watapima uzito siku ya ijumaa sdaa tatu asubui kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi agost 22

mbali na mabondia hawo mabondia wengine watakao oneshana kazi siku hiyo ni kelvin Majiba atakaepambana na Vicent Mbilinyi wakati Husein Pendeza akioneshana umwamba na Shomari Mirundi na Raymond Mbwago atazidunda na Roger Masawe na mapambano mengine mengi ya mabondia chipkizi

mabondia hawo watapima uzito katika tawi la mashabiki wa yanga bomba lililopo mtaa wa ndanda Kariakoo na mpambano wao kufanyika siku ya jumamosi kuanzia saa kumi na mwisho kabisa itakuwa saa kumi na mbili jioni ili kila mtu afurahie ngimi izo zitakazochezwa mapema na kumalizika mapema kabisa katika siku hiyo
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile



Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi



pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Thursday, August 13, 2015

FAINALI YA TMT KUFANYIKA AUGUST 22, MAKUMBUSHO YA TAIFA POSTA


WWW.BUKOBASPORTS.COM Shindano la kuibua na Kusaka Vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limedumu kwa takribani Miezi Minne hatimaye shindano hilo linakaribia kufika tamati mnamo tarehe 22 August 2015 huku Mshindi Mmoja Akiondoka Na Kitita Cha Shilingi Milioni Hamsini Za Kitanzania.

Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.

Shindano la TMT lilianza mapema mwezi wa Nne kwa kutafuta vipaji katika Kanda ya Ziwa ambapo usaili ulifanyika Mkoani Mwanza na kuhitimishwa Kanda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam kwa kupatikana Jumla ya Washindi 20 kutoka Kanda sita za Tanzania
Washindi wa kanda sita walipata fursa ya kuingia ndani ya mjengo wa TMT huku wakipatiwa mafunzo ya sanaa kutoka kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam huku mchujo ukiendelea na kupelekea kila wiki Washiriki wawili kuaga shindano, takribani wiki tano jumla ya washiriki 10 waliweza kuaga shindano hili ambalo limefikia hatua ya kuwapata washiriki 10 waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora huku wakingojea fainali itakayotoa mshindi wa kitita cha shilingi milioni hamsini za kitanzania
Mpaka sasa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora wanaendelea na kujifua Kwaajili ya fainali ambayo imebaki wiki moja tu kwa fainali hiyo kuliteka jiji la Dar huku hofu na presha zikiwapata Washiriki hao.
Fainali ya TMT itafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa makumbusho ya taifa karibu na Chuo cha IFM kwa viingilio vya shilingi Elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa viti vya kawaida.
TMT 2015 inapigwa tafu na Precious Air, Cam gas, ITV na Radio One, Global Publishers, I-View Studio, Paisha na Hussein Pamba Kali

PETER MUHUNZI WA TEFA APETA RUFAA YAKE MUHIBU KANU AONDOLEWA



Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA, Advocate Rashid Saadallah (katikati) akiongea na wandishi wa habari kuhusu maamuzi ya rufaa za wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Chama cha Soka Temeke (TEFA) jana kwenye ofisi za DRFA jijini Dar es Salaam. Kulia ni katibu wa kamati hiyo Fahad Katanga na kushoto ni msemaji wa DRFA, Omar Katanga. (Picha na Rahel Pallangyo)

MWENYEKITI wa TEFA, Peter Muhunzi na Sizza Chenja wameshinda rufaa baada ya kuwekewa pingamizi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Soka mkoa wa Temeke. (TEFA)
Akitoa maazimio ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA,Mwenyekiti wa Kamati, Advocate Rashid  Saadallah, alisema kamati yake ilipitia mapingamizi yake kwa makini na kina kwa kufuata katiba ya TEFA, DRFA na ya chama mama ambacho ni TFF na kutoka na maamuzi ambayo hata hivyo alikiri kama mgombea hataridhika anaweza kukata rufaa kwenye ngazi nyingine ambayo ni TFF.
“Peter Muhunzi ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa TEFA, ameshinda rufaa yake baada ya kuthibitisha kigezo cha elimu kwa maana ya kumaliza kidato cha nne na Sizza Chenja kamati imempitisha aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa mpira wa miguu kama katiba ya TEFA Ibara ya (31)(1)(j) inavyotaka”, alisema Saadallah
Pia alisema Rashid Salim, ambaye pia anagombea nafasi ya Mwenyekiti -ameshindwa kuleta vielelezo kuthibitisha uzoefu wake katika masuala ya mpira kama Ibara ya 31(1)(j) inavyosema pia Aziz Mohamed Khalfan, kamati imegundua kwamba alienda kwenye mchakato wa uchaguzi akiwa hana sifa kwa sababu alifungiwa na kamati ya nidhamu na usuluhishi ya kutokushiriki au kujihusisha na mpira kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) na TEFA.
Saadallah alisema kwenye nafasi ya Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti, Shufaa Jumanne amepitishwa aendelee na mchakato wa uchaguzi baada ya kuridhika na uthibitisho wa uzoefu wa zaidi ya miaka mitatu katika uongozi wa soka Daudi Mumbuli, kamati inaitupilia mbali rufani baada muweka pingamizi kushindwa kutokea mbele ya kamati kuthibitisha madai yake.
Naye Omary Kapilima ambaye anagombea makamu wa kwanza wa Mwenyekiti  ameondolewa baada ya kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne kinachotambulika na Baraza la Mitihani la Taifa yaani (NECTA) ili kukidhi kigezo cha elimu kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA japo  kathibitisha uzoefu wa uongozi wa mpira na Salehe Mohamed kamati inamuengua katika mchakato wa uchaguzi kwa kushindwa kuthibitisha kiwango chake cha elimu kwa  kushindwa kuleta cheti cha kidato cha nne(Academic Certificate) kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA pia Bakili Makele ambaye alikuwa anagombea makamu wa pili ameenguliwa kwa kigezo hicho cha elimu kwani amekiri kwamba elimu yake ni ya darasa la saba
 Amack Nabola ambaye anagomea Ujumbe wa soka la wanawake na vijana ameenguliwa katika mchakato kwa kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne kama ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA inavyotaka lakini Fikiri Magoso ambaye anagombea mjumbe wa kamati ya Utendaji amepitishwa kugombea nafasi hii kwa sababu anakidhi vigezo kwa kuwa na cheti cha darasa la saba kama katiba ya TEFA anavyomtaka mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kuwa na elimu isiyo chini ya darasa la saba.
Mgombea Muhibu Kanu ambaye alikuwa nagombea nafasi mbili, ya makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kamati imemuengua kwa sababu  ni kinyume cha kanuni za uchaguzi za TFF za mwaka Ibara 10(9) ambayo inakataza mgombea kugombea nafasi zaidi ya moja.
Pia Saadallah alisema kamati yake imefanyia kazi pingamizi la ambazo kikatiba na kanuni kwani zile za matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu, kamati haina mamlaka ya kuyatolea maamuzi hivyo yanapelekwa kwenye kamati ya maadili ya DRFA.
 
 

Uchaguzi Ubunge Jimbo la Handeni lawaka moto



“Kimsingi hakuna mgombea anayejua amepata kura ngapi na wapi amekosa, maana hata huyo Salu anayedaiwa ameshinda amepewa ushindi wa jumla na hakuna anayejua namna  gani mchakato huo umefanyika, ndio maana ofisi ya CCM wilaya iliamua kufanya  siri, huku kila mgombea akiambiwa jambo la kumpa moyo,” alisema Mbwana.

Naye Chifu Msopa alisema kwamba hawawezi kukubali mtu mmoja afanye mambo kwa maslahi yake, hivyo wagombea wote wa ubunge watasusia mchakato wa kampeni katika jimbo la Handeni, kama hali ya kubebana itaendelea dhidi ya Katibu na washindi wake aonao wanafaa kuliko wengine.

“Hatutaki kuendelea kuwa waoga huku wachache wakiendelea kuiharibu CCM yetu, uchaguzi huu urudiwe au kufuata maagizo ya Kamati ya Siasa ya wilaya na ile ya Maadili ambayo kwa bila kujua kwanini, Katibu aliyaweka kando mapendekezo hayo na kufanya anavyotaka mwenyewe,” alisema Msopa.

Kwa kipindi cha wiki moja sasa jimbo la Handeni limekuwa kwenye mgogoro mkubwa kati ya viongozi wa CCM wilaya ya Handeni na wagombea ubunge ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha kuchukizwa na mwenendo mbovu wa katibu wa CCM handeni, ambaye ameendelea kuwabeba wagombea, wakiwamo wale waliotajwa kwenye kashfa za rushwa.

Monday, August 10, 2015

BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA KIDEDEA AFRIKA YA KUSINI

BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibada   Lizbeth Sivhaga wa nchini humu
huu ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za awali

ata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili

ushindi wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote

bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne

Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi
Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili

Friday, August 7, 2015

MABONDIA RAMA SHAURI NA LULU KAYAGE WAPAA AFRIKA YA KUSINI


Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwa na mabondia Lulu Kayage kulia na Ramadhani Shauri wakienda kupanda ndege kwenda afrika ya kusini mabondia hawo wanapanda uringoni agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA LULU KAYAGE

MABONDIA WAKIWA NA WADAU MBALIMBALI WA MASUMBWI KABLA YA KUPAA AFRIKA YA KUSINI KWA AJILI YA MCHEZO WAO WA AGOST 9


Bondia Lulu Kayage kulia  akihakiki nyalaka zake za kusafiria kushoto ni mshauri wake wa karibu Hamisi Berege kutoka kambi ya mchezo wa ngumi Ilala Lulu amenda Afrika ya kusini kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akingia katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa julius nyerere kwa ajili ya safari pamoja na mabondia Lulu Kayage kushoto na Ramadhani Shauri mabondia
kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Wednesday, August 5, 2015

SUPER D AZAWADIA BONDIA LULU KAYAGE VIFAA



Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila amemzawadia bondia Lulu Kayage vifaa vya mchezo wa masumbwa baada ya bondia huyo kuchaguliwa kwenda kupigana Afrika ya kusini agust 9 mwaka uhu vifaa hivyo alivyokabidhiwa bondia huyo ni Gumshilt 'kikingiakinywa' clip bandeji pamoja na fulana yenyenembo ya Tanzania vifaa ambavyo ni lazima bondia awe navyo

Lulu kayage anaondoka nchini agous 7 kwenda afrika ya kusini kupambana na Lizbeth Sivhaga Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo siku ya jumapili

akizungumza baada ya kupokea msaada huo Lulu alimshukuru Super D kwa kujitolea alichojaliwa kwa kuwa sio watu wote wenye mioyo ya kujitolea kama yeyey hivyo amemwakikishia kumpa zawadi ya ushindi ili aendelee kuwa na furaha mana ushindi wangi ni wa watanzania wote hivyo sito wahangusha

nae Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallahh 'ostadh' aliongeza kwa kusema Lulu atambatana na bondia Ramadhani Shauri atakaekwenda kupambana na bondia mzoefu Philip Ndlovu  siku hiyo hiyo msafara huo utakuwa na watu watatu ukiongozwa na mimi mwenyewe pamoja na mabondia wawili 

ata hivyo namshukuru kocha Super D kwa kumzawadia Lulu kwani tungepata watu wengi wa kujitolea kwa moyo mmoja kama yeye michezo yetu ingefika mbali zaidi Duniani

LULU KAYAGE KUZIPIGA AFRIKA KUSINI




Bondia Lulu Kayage (kushoto) akimrushia konde bondia  Hamisi Berege wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwene Uwanja wa Msimbazi Rovers Ilala jijini


MABONDIA wawili wa ngumi za kulipwa wanatarajia kuondoka nchini kesho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika Agosti 9, mwaka huu.

Akizungumza jijini kocha wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila  'Super D' aliwataja mabondia hao kuwa ni Lulu Kayage na Ramadhan Shauri.

“Lulu na Shauri wamepata mapambano yatakayochezwa Agosti 9, hivyo wataondoka kesho kwa ndege ya shirika la Ethiopia “, alisema Mhamila.

Pia Mhamila alisema Lulu atapigana na Lizbeth Sivhaga na Ramadhan Shauri atapigana na bondia mzoefu Philip Ndlovu 

Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo hivyo watanzania mnawaombwa kuwaombea mabondia hao ili waweze kupeperusha bendera ya taifa vema.

FAMILIA INAPOKUTANA KWA MARA NYINGINE STAR BOY NA SUPER D

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akiwa na kaka yake Shabani Mhamila Star Boy wa pili kulia baada ya kupotezana kwa mda




Rajabu Mhamila Super D kulia

YOLANDA SHAYO BALOZI WA MKOA WA KILIMANJARO ATEMBELEA VITUO VYA WATOTO YATIMA


Mrembo aliebuka kidedea kwenye shindano la kumsaka barozi wa mkoa wa Kilimanjaro 2015,Yolanda Shayo ametembelea vituo vya watoto yatima katika eneo la mamba Malangu moshi vijijini.

Shughuli hiyo ilifanyika mapema jana ambapo mrembo huyo alitembelea vituo vinee ambavyo ni Msoroe,Mrieni,Kikoro na kotela kwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto na kula nao chakula cha pamoja.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa na mrembo huyo ni kalamu,madaftari,rula na sabuni za kufulia na kuogea,Yolanda alipata fulsa ya kuongea na viongozi wa vituo hivyo ambapo alibaini  changamoto balimbali zinazokabili vituo hivyo.

Yolanda ambae ni Miss Kilimanjaro Ambassador wa mara ya kwanza ameonesha jitihada zake za kuanza kazi ya urembo kwa kuitumikia  jamii yake ambapo alikuwa ana wito huo tangu akiwa mtoto.

Kwa nafasi aliyoipata mrembo huyo ameaidi kuwa kinara kuutangaza utamaduni wa mkoa wa kilimanjaro na kuvitangaza kitaifa na kimataifa vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya mkoa huo.

"mbali ya kuwa mrembo na balozi wa mkoa wa kilimnjaro nitahakikisha natumia fulsa hii kupeleka ujumbe mbalimbali kwa jamii yangu ikiwemo kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika octoba" aliongea Yolanda.
Miss kilimanjaro ambassador 2015,Yolanda Shayo akiwa katika picha ya pamoja na mtoto ambae anaosha kalamu ikiwa ni sehemu ya zawadi zilizogawiwa na mrembo huyo.
 Yolanda Shayo akisaidia kugawa chakula kwa watoto na viongozi wa vituo hivyo,ambapo alishiriki kwa pamoja nao katika chakula cha mchana.