Friday, July 19, 2019

SUPER D ATAMBA KUWA CHOKI HATACHUKUWA UBINGWA WA MASHINDANO YA KING OF THE RING 2019



Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazozi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam

Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazozi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam
                                                Na Mwandishi Wetu

BAADA ya mchujo wa kwanza kupita katika mashindano ya King Of The Ring sasa ni hatua ya nusu fainali itakayowakutanisha mabondia wanne kutoka wilaya za jiji la Dar es salaam ambapo katika Wilaya ya Ilala anatoka Juma Choki ambaye anapeperusha bendera ya wilaya hiyo bondia huyo machachali anatoka katika kambi ya kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amesema amemuandaa choki kwa ajili ya ushindi

kwani yeye ni mshindani wa kweli ambapo katika mashindano hayo mara ya kwanza katika hatua ya mtoano alimchakaza bondia mgumu zaidi Peter Makundi katika mashindano hayo na sasa yupo katika nusu fainali atuwezi kuwangusha wapenzi wa ngumi kwani ubingwa tunautaka na ninawambiwa king of the Ring 2019 inakwenda Ilala bila kipingamizi wala kikwazo chochote kile

kwa upande wa bondia Choki amesema kuwa yeye yupo fiti kwani anaona mpambano upo mbali anataka ata leo zipigwe kwa kuwa yupo fiti mpaka anajiogopa hivyo basa wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kuona nafanya nini siki hiyo katika mchezo wa masumbwi nchini nitandika historia mpya kabisa katika ngumi ambayo aijawai kutokea ila kila mtu atajua kazi ya mikono yangui ni nina na maamuzi yapo katika mikono yangu kwa kutoa vipigo vya paka mwizi

Katika mashindano hayo mabondia wengine waliopita ni Emanuel Mwakembe Issa Nampepeche na Emanuel Timtim mabondia wote hawo ni wa uzito wa kg58

Katika mashindano hayo washindi watapata zawadi kem kem kama kifuta jasho 

1 comment: