HAMAD FURAHISHA
BONDIA HAMAD FURAHISHA ambaye ya sasa ameingia katika ngumi za kulipwa kwa mara ya kwanza june 27 atapanda ulingoni kuzichapa na Godfrey Polino mpambano wa raund 4 kg 55 katika uwanja wa Kifa uliopo Mburahati
Mpambano huo utafanyika katika uwanja wa kifa uliopo Mburahati umekuwa ukisubiliwa kwa hamu kubwa sana ambapo mabondia hawo ni mtu na kocha wake zamani wakati Polino alikuwa kocha uku Furahisha alikuwa bondia katika ngumi za Ridhaa wote wakiwa katika kam,bi ya JKT
Mabondia hawo watapigana kwa mara ya kwanza wakiwa na historia kubwa ya mchezo wa masumbwi katika ngumi za ridhaa na kuliletea sifa Taifa lakini kwa sasa watapigana katika ngumi za kulipwa uku kila mmoja akitaka kukuonesha
Umwamba wake katika ulingo jinsi anavyozipiga kwa ufundi zaidi majina ya Polino na Furahisha sio mageni katika ulimwengu wa masumbwi nchini ila ni mageni katika ngumi za kulipwa ambapo kupitia mabondia hawo mashabiki watapata burudani ya kutosha ya mchezo wa masumbwi nchini
akizungumza na mwandishi wa habari hizo Hamadi Furahisha anasema kuwa ngumi alianza mwaka 2009 Yombo dovya boxing Clab iliyopo chini ya kocha haji Pela ambaye mpaka leo hii wapo pamoja
alishiriki katika mashindano mbalimbali ya masumbwi ya Ridhaa yakiwemo mashindano ya clab bingwa pamoja na ya taifa na kufanikiwa kuchaguliwa na timu ya Taifa ya ngumi mwaka 2016 ambapo alidumu katika timu ya Taifa mpaka mwaka 2018 ambapo alipata nafasi ya kujiunga na JKT hata hivyo baada ya miaka kazaa akakosa ajira na sasa yupo mtaani na ameamua na kujiunga na ngumi za kulipwa
anakumbuka kipindi hicho yupo JKT walipita mabondia ambao ni maarufu na mashughuli kwa sasa akiwepo Hassani Mwakinyo Salim Matango na wengine ambao nao waliachana na JKT na kujiunga na ngumi za kulipwa mara moja
katika mchezo wa masumbwi yeye alivutiwa zaidi na Ismail Galiatano ambae nae ni bondia wa jeshi mpaka hivi sasa ndio aliekuwa akimpenda tangu anaanza ngumi mpaka sasa na kwa nje anamkubali zaidi
Bondia Manny Paquai ambaye amekuwa akimkubali zaidi kwa mapigo yake ya kasi na jinsi anavyo zitendea aki ngumi apiganapo ulingoni
Furahisha amemwambia Polino kuwa supu aitiwi nazi ikitiwa nazi inakuwa mchuzi hivyo kipigo atakachompa ni cha pekee kwani kipigo hicho akijawai kutokea tangu aanze mchezo wa masumbwi nchini
akizungumza mabondia wa Tanzania amewasii mabondia wasiwe wanaingia mitini pindi wanapopewa mapambano na yeye kwani yeye anamikono miwili na wao miwili
pia ilitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu vijana wao pamoja na watoto kuwapa sapoti ili wacheze mchezo wa masumbwi kwani kwa sasa ni ajira na inaweza kukutoa sehemu moja kwenda nyingine hii ni kazi kama zilivyo kazi zingine wanazofanya watu maofisini
aliongeza kwa kusema anampiga kocha wake pia mabondia wengine wajipange foleni ambao watakuwa katika uzito wa kg 55 kuwa hizi ni salam kwao
asesema anawaomba sapoti kwa mashabiki zake wote wa dabo kibini wakionozwa na Habib Othumanbig kuja kumunga mkono na kumsapoti kwa ali na mali
mpambano huo ulioratibiwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion umeandaliwa na Kwame Sports Promotion chini ya Promota mkuzaji wa Vipaji Kwame Hamisi Matwani mpambano utafanyika june 27 |