Thursday, November 18, 2021
BONDIA RAMADHANI MIGWENE AMUWEKEA MIKWALA ALBANO CLEMENT BAADA YA KUKIMBIWA NA HABIBU PENGO
BONDIA RAMADHANI MIGWEDE baada ya kukimbiwa na mpinzani wake Habibu Pengo aliesaini nae kuzipiga mara ya kwanza sasa amebadilishiwa mpinzani na atacheza na bondia machachali kutoka mlandizi Albano Clement Desema 3 mpambano wa raundi nae utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango jijini Dsar es salaam
akiongea wakati wa kutambulisha mpambano wa rasmi Migwede amesema kuwa yeye ni bondia hivyo uwezo wake una mruhusu kucheza na mtu yoyote atakaekuwa mbele yake ili mradi walingane uzito tu aliongeza kwa kusema unajua mimi ni bondia hivyo kazi yangu mimi ni kupigana hivyo siwezi kuacha kupigana kwa sababu Pengo kanikimbia hii ni kazi kama kazi nyingine nimepewa kazi na Albano hivyo ajipange kwa kuwa kipigo nitakachompa ni cha mbwa mwizi mimi ni mtu mwingine kabisa niwapo ulingoni hivyo ajitahalishe sasa sijui mwenzie kaona nini mpaka kakimbia na mimi naishi huyu kadandia treni kwa mbele sasa kipigo nitakachompatia atashindwa kuhadithia nae
Clement amesema kuwa yeye ni bondia na ngumi ni kazi yake hivyo kazi kazi watakutana ulingoni sdiku hiyo mimi nimewapiga mabondia wakubwa kuliko yeye nimempiga Saidi Mundi kutoka Tanga bondia ambaye ni hatari sana kwa tanzania lakini nimemkalisha na cha moto kakiona nimemtwanga bila huruma bondia Seba Temba kutoka Morogoro na yeye alikuwepo katika mpambano huo sasa sidhani katika raundi nane hizo hatamaliza yote kwa yote mikono yangu ndio itakayo amua mpambano uho mbali na mpambano uho unaosubiliwa kwa hamu siku hiyo pambano ilingine kali litawakutanisha mabondia machachali Muksin Swalehe ;Alkasusu; na Cosmas cheka mabondia ambao walikuwa wakitafutana kwa mda mrefu sasa kumaliza ubishi Desemba 3 katika uwanja wa kinesi