Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 25, 2010

DK. BILAL AKUTANA NA MWASISI WA AFRO SHIRAZ-PEMBA


Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Fatma Zahoro (70) ambaye ni miongoni mwa waasisi wa Afro Shiraz, mkazi wa Wete Pemba baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika jana okt 24 kwenye Uwanja wa Shule ya Kizimbani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Picha na Muhidin Sufiani

ZAIN YAKABIDHI ZAWADI ZA BAHATI NASIBU YA MTV AFRICA MISIC


Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Hellen Magessa (kulia) akipokea zawadi ya Runinga kutoka Zain mara baada ya kuibuka mshindi wa bahati nasibu ya kwa ajili ya maandalizi ya tamasha la MTv Africa Music Awards (MAMA). Makabidhiano haya yalifanyika Thai Village jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Anayekabidhi zawadi hiyo ni Meneja Masoko wa Zain, Kelvin Twissa. Tamasha kubwa la muziki barani Afrika la MAMA ambalo limedhaminiwa na Zain, litafanyika mwezi Disemba mwaka huu huko jijini Lagos Nigeria.

NCCR MAGEUZI YAWAKARIA KOONI TAMWA NA CHADEMA KWA KUMKASHIFU MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA KAWE


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha NCCRR-Mageuzi,Bw. James Mbatia, ametoa siku saba kwa Chama Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA)kumlipa fidia ya sh. bilioni 1 kwa kumdhalilishwa.

Wakati huohuo, Bw. Mbatia ametoa siku 3 kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kumlipa sh. bilioni 1 na kukilipa chama cha NCCR sh. bilioni 3 kama fidia ya kudhalilishwa.

Bw.Mbatia alibainisha hayo jijini leo alipozungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya kisiasa juma la mwisho kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Bw.Mbatia alisema, TAMWA kupitia Mkurugenzi wake,Bi. Annanilea Nkya imekuwa ikitoa taarifa za uzushi na uongo juu yake, ikimtuhumu kumyanyasa mpinzani wake jimbo la Kawe, Bi. Halima Mdee.

Alisema taasisi hiyo inamtuhumu kutokuwa na hoja wala sera,kutumia lugha za matusi, kutumia mbinu chafu na kejeli,kuwa na mtazamo potofu juu ya mpinzani wake jimbo la Kawe, jambo ambalo ni uzushi.

"Nilikuwa naiheshimu sana TAMWA lakini kunizushia kwamba nanyanyasa wanawake imeniuma sana... chama chetu kinatoa fursa sawa kwa wanaume na wanawake kama nembo ya chama chetu inavyoashiria, hata makamu Mwenyekiti wangu ni mwanamke" alisema.

Aliituhumu taasisi hiyo kuwa wakala wa CHADEMA,na hivyo kusambaza maneno ya uongo kwa vyombo vya habari, ambapo ametoa siku saba kwa chama hicho kumlipa fidia hiyo.

Katika hatua nyingine,Bw. Mbatia amekishukia chama cha CHADEMA,kwa kumdhalilisha kupitia mikutano ya kampeni inayofanywa na mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Kawe.

Bw.Mbatia alisema, Bi. Mdee amekuwa akimtuhumu kuwa kibaraka wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) na kupokea kiasi cha sh. milioni 80 kwa wiki kutoka chama hicho.

Alisema licha ya kufikisha malalamiko hayo katika Tume ya Maadili, tume hiyo haijatoa tamko lolote kuhusu suala hilo.

Alisema, amefikia hatua hiyo ya baada ya mgombea urais wa CHADEMA,Dkt. Willbroad Slaa kuonesha kuunga mkono tuhuma zinazotolewa na Bi. Mdee wakati akihutubia katika Viwanja vya Tanganyika Peckers juzi.

Alisema kupitia mkutanao wa Dkt. Slaa chama chake kilikashifiwa kwa kuitwa Chama Cha NCCR-'Manunuzi' huku Dkt. Slaa akimtaka Bw. Mbatia kama anataka kutangaza majina ya wabunge wa viti maalum CHADEMA, aombe ukatibu MKuu wa chama hicho.

"Namheshimu sana Dkt. Slaa lakini kitendo cha kusema kuwa mimi ndio nimesema Mdaa ni mbunge wa viti maluum akisahau kuwa yeye ndiye aliye tangaza na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi la Septemba 29 imenisikitisha sana" alisema.

Bw. Mbatia aliitaka CHADEMA kuitisha mkutano mahali palepale kwa watu walewale na kukanusha madai dhidi yake ndani ya siku tatu.

"Tumewapa siku tatu kuitisha mkutano wa hadhara, kama waliouitisha mwanzo, wakanushe uzushi huo vinginevyo tunawapeleka mahakamani" alisema.

HOME SHOPPING CENTRE KARIAKOOO

KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL YAMUAGA DR. AMANI KARUME


Your Excellency, Dr. Amani Abeid Karume President of Zanzibar Revolutionary Government,
Honourable Ministers,
Members of the Diplomatic corps,
Distinguished Guests,
Ladies and Gentlemen,

Your Excellency, Zantel is honored to be part of this momentous occasion in the history of Zanzibar.

On behalf of Zantel Staff, Management and Board, we thank the president for being instrumental in our formation as a company back in the days when we were starting out and for being part of our success today.

Your Excellency, we are also grateful for creating an enabling environment that has allowed us to grow and become the biggest telecom company in Zanzibar and the fastest growing network in Tanzania mainland. The support your government accorded Zantel in these 10 years, is a shining example of some of the offshoots of good governance.

Ladies and gentlemen, Zantel has achieved tremendous success the highest being able to successfully launch its services in mainland Tanzania 5 years ago.
Zantel has also won the several accolades and our proudest is being involved as a partner in the EASSY submarine cable project that will revolutionize internet connectivity in East Africa.

I am proud to say that Zantel is now the NUMBER ONE provider of internet services in Tanzania today. We have also extensively increased our network coverage nationally and internationally and now reach in more than 400 destinations around the world where the Zantel sim card works.

From its humble beginnings in Zanzibar to its current spread in the whole of Tanzania Zantel is now a renowned telecom giant in East Africa. Zantel is a pride of Zanzibaris and are proud of our contribution in making Zanzibar have one of the highest mobile penetration rates in Africa. We will strive to make Zanzibar a Communication hub for East Africa.
On behalf of the whole corporate sector, Etisalat, SMEs in Zanzibar we thank the president for creating a business friendly environment witnessed today through the flourishing business around the isles.

We hope you will continue to be an ambassador for Zantel as we grow and continue to make Zanzibar proud.

I thank you all.

Sunday, October 24, 2010

MSONDO WAENDELEZA MAKAMUZI

mashabiki wa msondo wakiburudika katika viwanja vya TCC Chang'ombe MWISHONI MWA WIKI

DK SLAA AUNGURUMA DAR ES SALAAM




Mgombea wa nafasi ya urais kupidia chama cha CHADEMA. Dk Willibrod Slaa akiwahutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Ndugumbi Shule ya Magomeni Dar es salaam

NCCR MAGEUZI YAPINGE NEC KUTOWALIPA POSHO MAWAKALA


CHAMA cha NCCR Mageuzi kimesema kinapokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa haitawajibika kuwalipa ama kuwapa posho mawakala wa Vyama vya Siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mkuu wa idara ya kampeni na uchaguzi ya chama hicho Bw.Faustin Sungura alisema NEC ina wajibu wa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi pamoja na sheria nyingine za nchi.

Bw.Sungura alisema Julai 26 mwaka huu NEC chini ya Jaji mstaafu Bw.Lewis Makame ilisaini kuheshimu kutii na kutekeleza maadili ya uchaguzi pamoja na wajibu wake.

"Ndugu waandishi wa habari,vifungu 92 (1) cha sheria na 4 (1979) ya uchaguzi wa madiwani ,pamoja na kifungu cha 93 (1) na (2) cha sheria na 1(1985) ya uchaguzi wa wabunge na Rais vinawataka mawakala wote wa vyama vya siasa kabla ya kuanza kazi ya kusimamia au kuangalia mchakato mzima wa kupiga kura kuhesabu na kutangaza matokeo,kula kiapo cha kutunza siri "alisema

Anaongeza "Aidha watendaji wote wanaosimamia uchanguzi chini ya NEC hutakiwa kwanza kula kiapo cha kutunza siri za uchaguzi na wote hawa wanalipwa posho bila kujali kama wanalipwa mishahara au la!,ni wazi kuwa watu hawa wamekuwa sehhemu ya uchaguzi "alisema

Bw.Sungura anasema serikali haiwezi kumpa mtu kazi ya kufanya bila kumlipa na hasa inapokuwa nyeti na inayomlazimu mtu huyo kula kiapo kwanza.

Hata hvyo amewaomba wapiga kura kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kupeleka madiwani wengi kwenye halmashauri za Wilaya ,miji na Manispaa na wabunge wengi kutoka upinzani.

Akizungumzia kusimamisha mgombea mmoja wa kambi ya upinzani wa nafasi ya Urais alisema vyama vya upinzani vimekubaliana kujipa mda ili kuimarisha nguvu ya upinzani.

Saturday, October 23, 2010

MASENETA WA MSONDO WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA BENDI HIYO


MASENETA wa Bendi ya Msondo Mgoma jana wamekunatana kujadili mstakabari mzima wa bendi hiyo ilipo sasa na inapoelekea tangu kifo cha Moshi William TX..

Masenata hawo walikutana katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya ya bendi hiyo Amana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila (Super D) alisema kuwa kati ya ajenda waliojadili ni pamoaja na mwenendo mzima wa bendi hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inazidi kupoteza mashabiki.

Alisema pamoja na hilo pia walijadili jinsi watavyo anza kuifufua upya bendi hiyo na kuongeza wasanii wawili wapya ili kuongeza nguvu katika kutoa burudan.

"Sasa bendi yetu haipo kama zamani hivyo tunakaa vikao kujadili ni namna gani tutakavyoweza kuitengeneza upya bendi yetu ikiwa na kuongeza wasanii wengine wapya ambao tunaimani watareta nguvu ndani ya bendi yetu," alisema Super D.

Pia alisema baada kikao hicho wanatarajia kukutana tena Novemba 5 mwaka huu ili kuwatangaza wasanii wapya ambao watatoka ndani ya bendi za jijini Dar es Salaam.

Alisema tangu alipofariki Moshi Williamu TX bendi hiyo imekuwa na muelekeo mbaya ambapo ndiyo mtu aliyekuwa tengemezi kubwa ndani ya bendi hiyo ambayo ilijipatia umaarufu mkubwa miaka ya nyuma na kuleta tunzo 4 mfululizo ndani ya miaka hiyo ikiwemo Kilimanjaro Music Awards.

DK. BILAL AUNGURUMA MASWA MAGH-SHINYANGA


Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Kijiji cha Masai Kata ya Seng’wa Wilaya ta Maswa Mkoa wa Shinynga, wakati alipowasili kijijini hapo leo mchana kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Robrt Simon Kasena
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya asili cha Bugayangi cha Kijiji cha Ngongo Wilaya ya Maswa, wakicheza na nyoka wakati wa mapokezi ya mgombea mwenza wa urais wa CCM Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Masai kufanya mkutano wa kampeni

MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS KUPITIA CHAMA CHA UPDP AZINDUA KAMPENI MANZESE LEO













exclusive-interview-and-pictures-with julieth william MISS PROGRESS INTERNATIONAL 2010

CCM YATOA ZAWADI KWA WASHINDI


WASHIRIKI tisa wa Bahati Nasibu ya Changia Chama cha Mapinduzi (CCM), wamezawadiwa zawadi zao katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa, Asha Baraka, alisema Mtanzania yeyote anaruhusiwa kucheza bahati nasibu huyo.

Asha alisema CCM haina ubaguzi, hivyo mwanachama wa chama chochote anaruhusiwa kucheza bahati nasibu hiyo, na ikiwa atashinda atakabidhiwa zawadi yake kama kawaida.

¡°CCM hatuna ubaguzi, milango iko wazi kwa kila mtu, hata awe wa chama kingine, akishinda tutamkabidhi zawadi yake kama kawaida,¡± alisema.

Aliwataja walioshinda pikipiki ni Paul Wanyama na Deus Makua, wakati John Mfomoka, alishinda zawadi ya baiskeli.

Wengine waliojinyakulia kitita cha sh. 100,000 kila mmoja ni Nice Kisunte, Leah Pascal, Sama Rashid, Juma saleh, Sunday Mchunga na Joshua Alloyce.

Asha alisema walioshinda walituma ujumbe wa kuichangia CCM na namba zao kuingizwa kwenye bahati nasibu hiyo.

¡°Hawa walituma ujumbe wa kuchangia CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu, namba zao zikaingizwa kwenye bahati nasibu, wameibuka na pikipiki,alisema.

MSONDO NGOMA RATIBA YA WIK END


BENDI YA MSONDO NGOMA ITAENDELEA KUTOA BURUDAN LEO KATIKA UKUMBI WA TCC CHANG'OMBE LEO AMBAPO KESHO WATAKUWA KATIKA UKUMBI WA MAX BAR ILALA BUNGONI KWA KIINGILIO CHA 5000 KARIBU UOPATE NYIMBO MPYA NA ZAZAMANI

SABODO AENDELEA KUWACHANGIA CHADEMA


MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustapha Jaffar Sabodo, kwa mara ya pili tena amejitokeza hadharani kukichangia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiasi cha sh mil 100.
Hii ni mara ya pili kwa kada huyo maarufu wa CCM, kutoa kiasi kama hicho, kwani Julai 12, mwaka huu aliichangia Chadema na kuitaka kuendeleza mapambano ya upinzani kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania

Sabodo alikabidhi hundi ya kiasi hicho jana nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliyeambatana na viongozi wa kitaifa akiwemo Mbunge wa viti maalum anayemaliza muda wake Suzan Lyimo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Antony Komu.

Akikabidhi hundi hiyo, Sabodo alisema licha ya kuwa mwanachama halisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mingi, angependa kuona upinzani na demokrasia ya kweli inaimarika nchini huku akisisitiza kuwa CHADEMA ni chama makini ambacho kitawakomboa watanzania.

Sabodo mmoja wa wazee wanaoheshimika katika jamii kutokana na msimamo wake hata kufikia hatua ya kuikosoa serikali pindi anapoona mambo yanakwenda kinyume hasa kukiuka misingi ya utawala bora, iliyojengwa na mwasisi wa taifa hili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

“Mimi ni mwanachama wa CCM, lakini napenda kuona demokrasia inakua, huku kambi ya upinzani ikiimarika na kuwa na wabunge wengi bungeni ili kushamirisha maendeleo nchini… leo (jana) nawachangia CHADEMA kwa kwa mara ya pili na ninatambua umakini wenu katika siasa za hapa nchini na hasa bungeni,” alisema Sabodo.

“Nitaendelea kuwa mwanachma halisi wa CCM na nitaendelea kukiunga mkono, lakini bila upinzani kama CHADEMA ilivyo, CCM italala na hakiwezi kuwa makini,” aliongeza mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa kipenzi cha hayati Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake.

Katika kuonyesha kuwa CCM kinahitaji kuwa na chama mbadala, mfanyabishara huyo alisisitiza kuwa kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni ni jambo muhimu ili kutoa upinzani kwa CCM na kusukuma maendeleo ya wananchi.

Alisema hali ilivyo sasa nchini ni lazima upinzania uimarike ili kuisukuma serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi waliokataa tamaa na serikali yao huku akisisitiza upinzani sio uadui na kutoa wito kwa wafanyabiashara wengine kulitafari hilo ili kustawisha demokrasia nchini.






















HABARI NA PICHA KWA HISANI YA http://bongoweekend.blogspot.com/
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...