Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 25, 2010

ITV NA SAFARI LAGER ZAUNGANA KUTAFUTA SHUJAA

Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah akielezea jinsi kampeni ya kumpata Shujaa wa Safari Lager itakavyoendeshwa katika sehemi mbalimbali ya nchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo ndani ya kiota cha Safari Pub kilichopo ndani ya kampuni ya bia Tanzania.
Mkurugenzi wa Radio One na ITV,Deogratius Rweyunga (shoto) akitoa shukrani kwa wadhamini wa kampeni hiyo ya kumtafuta Shujaa wa Safari Lager iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar.kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah.

Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi akuzungumza leo katika uzinduzi wa kampeni ya kumtafuta Shujaa wa Safari Lager uliofanyika katika kiota cha Safari Pub ndani ya kampuni ya bia Tanzania (TBL).kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager na ushirikiano wa kituo cha televisheni cha ITV leo wamezindua rasmi kampeni ya aina yake ya kuwatafuta mashujaa wa ukweli katika jamii ambao watapata tuzo za heshima kutokana na mambo waliyofanya katika jamii inayowazunguka na kuleta mabadiliko.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema; Shujaa huyu wa Ukweli, atajulikana kama “Shujaa wa Safari Lager” na ni lazima awe Mtanzania aliye na umri wa miaka 18 na kuendelea, anatakiwa awe amefanya kitu au jambo kubwa katika jamii inayomzunguka ambalo limeleta mchango mkubwa au mabadiliko katika jamii hiyo, mtu huyu anatakiwa awe amefanya mambo au jambo hilo bila kusukumwa na uwezo wa pesa au madaraka aliyo nayo bali msukumo toka ndani ya moyo wake.

Utaratibu wa kumpata “Shujaa wa Safari Lager 2010” utakuwa kama ifuatavyo;
Baada ya uzinduzi huu wa leo, kutakuwa na matangazo katika vyombo mbali mbali vya habari kuelezea jamii utaratibu mzima utakavyokuwa, na wananchi watatakiwa kupendekeza majina ya watu wanaoamini kuwa ni mashujaa katika jamii inayowazunguka, mapendekezo haya yatafanywa kupitia fomu maalum zitakazochapishwa katika magazeti ya NIPASHE na pia fomu hizo zitapatikana katika ofisi za mawakala wote wa TBL nchi nzima. Baada ya kujaza fomu hizo, wananchi watatakiwa kuzitumbukiza katika masanduku maalum yaliyo kwa mawakala wa TBL karibu na maeneo yao.

Fomu zote zilizokamilika zitakusanywa na majaji watazichuja na kupata fomu tatu zilizobeba mambo makubwa na yaliyogusa zaidi jamii ambapo watu hao watatu watatangazwa katika vyombo vya habari na kisha jamii itatakiwa kuwapigia kura kufuatia mambo au jambo walilofanya na jinsi lilivyogusa jamii, Jina litakalopata kura nyingi zaidi ndilo litakalokuwa mshindi na hivyo kupata tuzo ya “Shujaa wa Safari Lager 2010”.

Pamoja na tuzo hiyo, mshindi pia atapata zawadi ya pesa taslim shilingi milioni kumi, ambapo asilimia 30 ya pesa hiyo itaelekezwa katika jamii anayotoka mshindi huyo ili kusaidia mradi wowote wa jamii atakaochagua “Shujaa wa Safari Lager”, hivyo yeye kubakiwa na asilimia 70. Washiriki wawili waliobaki watapata shilingi Milioni moja kila mmoja kama kifuta jasho.Kampeni hii kwa mwaka huu inaanza leo tarehe 24 na itafikia kilele tarehe 14 Januari 2011 siku ambayo Shujaa wa Safari Lager 2010 atatawazwa rasmi.

Akizungumzia ushirikiano wa kituo cha ITV katika kampeni hii, Meneja Mawasiliano na Habari wa TBL, Editha Mushi alikipongeza sana kituo cha ITV kwa kukubali kushirikiana na Safari Lager kuendesha kampeni hii muhimu kwa watanzania, pia aliahidi ushirikiano wa kutosha baina ya TBL na vyombo vya habari katika harakati za kuinua jamii ya Watanzania.

ZANTEL KUDHAMINI MASHINDANO YA GOFU GYMKHANA

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel,Ikechukwu Kalu (kushoto) akizungumza na waandish wa habari wakati wa kutangaza kuzamini mashindano ya mchezo wa Golf ya wazi ya mwisho wa mwezi yatakayofanyika jumamosi Viwanja vya Gymcana Dar es Salaam.Wa kutoka kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Zantel, Nitish Malik, Kaptani wa Golf, Joseph Tango na Mkuu wa mawasiliano wa Zantel, William Mpinga.

ZANTEL YADHAMINI MASHINDANO YA MCHEZO WA GOFU

Dar es Salaam, Novemba 24, 2010: Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel imetangaza kudhamini mashindano ya mchezo wa gofu ya ya wazi ya mwisho wa mwezi yatakayofanyika Jumamosi ya wiki hii katika viwanja vya mchezo huo vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Masoko wa Zantel Nitish Malik alisema kuwa Zantel imeamua kudhamini mashindano hayo ili kusaidia kukuza mchezo huo ili uweze kufahamika kwa watu wengi zaidi. “Gofu ni mojawapo ya michezo maarufu sana duniani kwahiyo nina imani kuwa udhamini wa Zantel katika mashindano haya utazidi kuutangaza huu mchezo zaidi na pia kupitia udhamini huu watu wengi wataweza kujitokeza zaidi kucheza mchezo huu’, alisema

Aliongeza kusema kuwa ana uhakika kwamba mwendelezo wa udhamini wa Zantel katika mchezo wa gofu utakuwa changamaoto kwa watu wengine kujifunza gofu na pia kupitia njia hiyo kuna uwezekano wa kupata wachezaji wazuri ambao hapo baadaye wanaweza kuiwakilisha Tanzania katika michezo ya kimataifa na kuiweka katika ramani ya kimataifa.

CHEKA, MAUGO KUMALIZA UBISHI JANUAR MOSI



Mwandaaji wa pambano la ngumi za kulipwa kati ya Francis Cheka na Mada Maugo, Kaike Siraju akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, kuhusu la ngumi litakalofanyika Januari mosi 2011 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO), Yassini Abdalah

KOMBE JIPYA LA CHALENJI HILI HAPA


Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Carolaine Ndungu akikabidhi Kombe la (CECAFA) Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Iddi Kipingu (kushoto. kulia ni Meneja Mkuu wa MAhusiano wa kiwanda hicho, Teddy Mapunda

TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA

Tuesday, November 23, 2010

MITIKISIKO YA PWANI KURINDIMA DESEMBA 3


Kwa mara nyingine tena Times radio fm imeandaa Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lenye kauli mbiu isemayo “MITIKISIKO YA PWANI 2010 NI ZAIDI YA BURUDANI”

Mitikisiko ya Pwani - Burudani ya Taarabu ilianzishwa miaka mitatu iliyopita na hadi sasa imeendelea kuvutia wapenzi wengi wa muziki wa Taarabu, na utamaduni wa pwani na hivyo kuwa tukio maarufu hapa Tanzania hususan Dar es salaam.

Mwaka jana Mitikisiko ya Pwani ilifanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba ikiwa na lengo la kuvitambulisha na kuzisaidia bendi bora za muziki wa Taarabu Jijini Dar Es Salaam huku likihudhuriwa na maelfu ya watu.

Burudani ya Mitikisiko ya Pwani mwaka huu ina madhumuni ya kusaidia jamii na pia kutoa burudani kwa wapenzi wa Taarabu na Watanzania kwa ujumla.

Tamasha hili litakuwa nafasi kubwa ya wapenzi wa muziki wa Taarabu kusikiliza, kuangalia na kucheza tungo bora kutoka kwa bendi zote mahili za Taarabu nchini.

Zawadi kadhaa zitatolewa kwenye Tamasha hilo ikiwa pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wetu, oryx wauzaji wa mafuta, gesi na majiko ya gesi nchini pamoja na fedha taslimu ambazo zitachukuliwa na wapenzi wa Taarabu huku watu mia moja wa kwanza watajipatia t-shirts.

Mpaka sasa ni bendi tisa ambazo zimethibitisha kushiriki katika tamasha hilo ambalo litafanyika 03/12/2010 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee huku likimshirikisha msanii mkongwe wa Taarabu, Bi kitude ambaye pia mbali na kutumbuiza atakabidhiwa Tuzo ya Heshima kulingana na Mchango wake wa muziki kwa muda mrefu.

Bendi hizo ni pamoja na:

1) Coastal Modern Taarab
2) Dar Modern Taarab
3) East African Melody
4) Five Star Modern Taarab
5) Jahazi Modern Taarab
6) New Zanzibar Modern Taarab
7) Super Shine Modern Taarab
8) Tandale Modern Taarab
9) TOT Taarab

Tunawashukuru Mazula,Public Relation officer ,100.5. Times Radio fm

+255713412872
+255787412872

sana wadhamini wetu ambao ni ORYX, wauzaji wa mafuta, gesi na majiko ya gesi nchini, Tigo, Regency Hotel, PSI, ICV Security Company, Malaika Beach Resort, Zizou Fashion, Dida classic boutique, Jolyety Saloon.

ALI KIBA USO KWA USO NA JK

Mwanamziki Ali Kiba akilia kwa machozi ya furaha alipokutana na Rais Jakaya Kikwete kushoto ni Mkurgenzi mtendaji wa Airtel nchini Sam Elangalloor


New Post

AIRTEL ONE8 KUSAIDIA SHULE BAGAMOYO KUPITIA WIMBO WAKE UNAOTAMBA


KAMPUNI ya simu za Mkononi Airtel watautumia wimbo wa 'Hands across the World' ulioimbwa na wanamuziki mbalimbali wa kimataifa akiwemo Ali Kiba pamoja na wanamuziki wengine saba akiwemo R Kell kujengea shule ya msingi ya Kiromo
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurgenzi mtendaji wa Airtel nchini Sam Elangalloor alisema wimbo huo utachangia ujenzi wa shule hiyo kupitia mlio wa simu wa one kupitia mtandao wa Airtel live port au kutumia ujumbe wenye neno ONE8 kwenda 6262 ambapo pesa atakayokatwa mteja huyo itaingia moja kwa moja katika ujenzi wa shule hiyo

Alisema Airtel pia itaendela na mradi huo wa kusaidia shule zaidi ya 50 kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na kwamba na kwamba mradi huo wa kujendga shule ya KIromo unatarajia kumalizika Machi mwakani
Kwa upande wake Ali kiba alisema wimbo huo umeweza kumpatia manufaa makubwa ikiwemo kufanya kazi pamoja na wasanii wa kubwa akiwemo msanii wa kimataifa R Kelly, Afrika 2face (Nigeria), Amani (Kenya), Movaizhalene (Gabon), JK (Zambia), Fally Ipupa (Kongo) na Navio (Uganda).

Alisema ngundi hilo la ONE8 litatengeneza albam ya pamoja itakayokuwa na jumla ya nyimbo 12 ambapo katika albamu hiyo kila msanii atapata nafasi ya kutunga wimbo wake mmoja.




MKAMBI AZIKWA JIJINI DAR ES SALAAM

Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Juma Mkambi wakati wakielekea katika maziko yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam .
Rais wa Shirikisho la Soka Nchini TFF, Leodger Tenga, (katikati) akiwa ni miongoni mwa watu waliohidhulia maziko ya Juma Mkambi .
Wananchi waliojitokeza katika maziko ya Juma Mkambi wakiwa katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam

Monday, November 22, 2010

BALAZA LA MAWAZIRI LILILOPITA NANI KURUDI NANA KUTEMWA

MANAIBU WAZIRI WARIOPITA
http://bashir-nkoromo.blogspot.com/

HASSANI MOSHI TX AKIFUNDISHWA JINSI YA KUJIUNGA NA FACE BOOK NA FUNDI MITAMBO WA MSONDO




CHADEMA YAMEGUKA MWEKA HAZINA WA MADIWANI AJIUNGA NCCR MAGEUZI



aliyekuwa Mwenyekiti wa Balaza la Wanawake CHADEMA Taifa
Mjumbw wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa
Mwka Hazina wa Umoja wa Madiwani CHADEMA Bi. Lwticia Ghati ajiunga na NCCR Mageuzi leo akichukuwa kadi kutoka kwa Mwenyeki wa Chama cha NCCR Mageuzi,Bw. James Mbatia

TIMU YA TAIFA YA POOL YACHEMSHA MASHINDANO YA DUNIA YAJIPA MATUMAINI KUFANYA VIZURI MWAKANI


MASHINDANO YA DUNIA UFARANSA 2010 (WORLD BLACK BALL CHAMPIONSHIP- FRANCE-2010).

Dar es Salaam, : Chama cha mchezo wa Pool Table Tanzania (TANZANIA POOL ASSOCIATION- TAPA) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa mchezo wa pool table Tanzania Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) tunatoa rasmi taarifa na matokeo ya timu yetu taifa kwenye mashindano ya Dunia yaliyofanyika katika Ukumbi wa hotel ya Cheops iliyoko katika mji wa Limoges nchini Ufaransa.

Mashindano yalianza tarehe 08.11.2010 mpaka tarehe 13.11.2010 kwa kushirikisha nchi 12 badala ya nchi 32 kama ilivyokuwa imetarjiwa mwanzo. Sababu ya nchi nyingine kutohudhulia ni baada ya kukosa wadhamini wa kuwalipia gharama za ushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa chama cha pool Tanzania, Amos Kafwinga alisema; Timu yetu haikuweza kufanya vizuri sana baada ya kushika nafasi ya 10 kati ya nchi 12 zilizoshiriki ( nchi zilizoshiriki ni wenyeji France, N. Ireland, S. Ireland, Catalonia (Spain), S. Africa, England, Wales, Gibraltar, Scotland, Tanzania, Libya na Morocco) lakini tumeweza kupanda kiwango cha ubora wa nchi kutoka namba ya 16 mwaka 2008 mpaka namba ya 12 mwaka 2010 haya ni mafanikio makubwa yanayoonyesha wapi tunakwenda kupitia udhamini wa Bia ya Safari Lager.

Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA), Isack Togocho; kwa niaba ya Chama Cha Pool Tanzania alitoa shukurani zake za dhati kwa Bia ya Safari Lager kuweza kufanikisha safari ya timu ya taifa na kuhakikisha mchezo wetu wa Pool unaendelea kukuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini. Pia aliwapongeza sana mkurungezi wa masoko wa TBL Ndugu, David Minja na meneja wa Bia ya Safari Lager Ndugu Fimbo Butallah na kampuni ya promotion ya Integrated Communication kwa kuweza kufanikisha safari ya timu ya taifa katika mashindano ya dunia mwaka huu.
Kwa kweli TBL kupitia BIA yake ya SAFARI LAGER wamekuwa Ni mfano mzuri katika udhamini Kwa kutekeleza ahadi Na kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa hapa nchini na kuifanya nchi yetu ijulikane kimataifa kupitia mchezo huu wa pool table.

Leo hii kwa kupitia mchezo wa pool raisi wa dunia wa mchezo pool ametuomba tumwalike kwenye mashindano yetu ya Taifa ya pool mwaka 2011..

KAMPUNI YA ZAIN YABADILIKA RASMI SASA KUITWA AIRTEL


Sunday, November 21, 2010

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU


MZIGO MPYA UMEINGIA

DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI

KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA http://enzoy.org/index.php?lang=EN

PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366

KARIAKOO SOKONI LANGO KUU ULIZA LUKINDO 0755686929

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884


KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870


GONGOLAMBOTO GRAD'S BAR ULIZA MAPUNJA 0713388956

ULIZIA FUNDI MITAMBO ALLI MOMBA POPOTE ALIPO 0715260220

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492

Saturday, November 20, 2010

MAMA ASHA BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA KAZI ZA WAKE WA MABALOZI DAR

Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua rasmi maonyesho ya kazi za wake wa Mabalozi, yaliyoandaliwa na Kikundi cha wake wa Mabalozi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki jijini Dar es Salaam
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiangalia bidhaa za Vitenge vya Nigeria katika Banda la Nigeria wakati wa Maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo Nov 2o. Kushoto ni Wabunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu na Halima Mamuya




TAMASHA LA VYUO VIKUU LILILOZAMINIWA NA GRAND MALT RAFANA

Rashidi Abdallah 'CHID BENZ' akifanya makamuzi wakati wa tamasha la Grand Malt leo
CHIDI BENZIIIII


MSANII CHIPUKIZI MARYAM MWISHEHE ALIPATA NAFASI YA KUKAMUA
ALLY DAUDI WA D.S.J AKIFANYA FITU VYAKE


WATU KIBAOOOO WALIKUWEWPO KUONA TAMASHA HILO

MPIRA WA MIGUU ULIKUWEPO
GODWIN NTAWANJA WA ROYAL COLLEGE ALIKAMUA KINOMAAA
GODWIN AKIWA NA WILLHARA MALIMBO


MCHEZO WA POOL AUKUACHWA NYUMA ULIKUWEPO GODFREY MKANDALA AKIJITAALISHA KUPIGA MPIRA
GOOOO AHAAAA KAKOSAA HILO NI SOKAA
MTAALAMU WA MCHEZO WA POOL JIMMY BALUNGU
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...