Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, November 26, 2013

Rais Kikwete ndani kamata Fursa Twenzetu


  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.Mh. Rais ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha hiyo.Picha zote na Othman Michuzi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa,Ahmed Lussasi akizunguma katika Warsha ya Fursa namba alivyo
Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasseb Abdul a.k.a Diamond akitoa ushuhuda wake wa namna alivyoanza na mpaka alipofikia sasa,ambapo ameweza kuiona Fursa na kuweza kugawana fursha hiyo na vijana wenzake anaofanya nao kazi kila siku.Kushoto ni Mwanafursa Mwingine,ambaye pia ni Msanii wa Mashairi,Mrisho Mpoto.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatma Ally akielezea namna alivyoipata Fursa kwa kupitia Ufugaji wa Nyuki.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasikiliza vijana mbali mbali walopata Fursa na kuweza kufanikiwa katika maisha yao.
Mrisho Mpoto akizungumzia Fursa yake.

Wadau mbalimbali wa Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu wakimsikiliza kwa makini Mwenyeshaji wa Kampeni hiyo ya Fursa,Ruge Mutahaba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akiwapongeza vijana walioiona Fursa.
Wadau mbali mbali wakiwa kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja.

K-Guitar wa Bana Marquis wala hajutii



Kelvin Nyoni 'K Guitar' kaika pozi
MUIMBAJI wa bendi ya muziki wa dansi ya Bana Marquiz, Kelvin Nyoni 'K Guitar', amefyatua wimbo wake binafsi uitwao 'Sintojutia' uliopo katika miondoko ya Zouk.
Tayari wimbo huo umeanza kurushwa hewani na baadhi ya vituo vya redio nchini na kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kufyatua video yake ili mashabiki wapoate uhondo kamili.
Akizungumza na MICHARAZO, mwanamuziki huyo anayecharaza pia gitaa la rythm alisema wimbo huo ameurekodia katika studio za Swadt Records chini ya prodyuza T-Tach kwa msaada mkubwa wa mameneja wake watatu  akiwamo mchora katuni wa gazeti hili, Abdul King'O.
Kelvin alisema wimbo huo ni mwanzo wa safari ndefu ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki kupitia albamu yake binafsi itakayokuwa na nyimbo zaidi ya sita katikka miondoko tofauti za Zouk, Bongofleva na Rhumba.
"Baada ya kukamilisha kutoa video ndipo nitaanza kurekodi nyimbo nyingine ambapo mpaka sasa tayari ninazo kama tatu zilizokamilisha mashairi yake," alisema Kelvin.
Kelvin kabla ya kuingia kwenye muziki wa dansi akijiunga na bendi ya Bana Marquiz inayoongozwa na mwanamuziki nyota wa kimataifa, Tshimanga Assosa Kalala 'Mtoto Mzuri', alishawahi kutoa wimbo wa Bongofleva wa 'Mapenzi Siyo Pesa' kabla ya kuurudia tena katika bendi hiyo

Mechi ya Tanzanite sasa kuchezwa Dar


Mashujaa wa Tanzania, Tanzanite
MECHI ya kwanza ya raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini iliyokuwa ichezwe Mwanza sasa itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imebainika uwanja huo unatakiwa ufanyiwe marekebisho ambayo hayawezi kuwahi Desemba 7 mwaka huu, siku ambayo ndiyo mechi hiyo inatakiwa kuchezwa.
Vyumba vya wachezaji vya uwanja huo ndilo eneo ambalo linatakiwa  kufanyiwa marekebisho makubwa.

Zitto Kabwe, Dk Kitila wana mashtaka 11 ya kujibu CHADEMA


Zitto Kabwe
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe na Mjumbe wa kamati Kuu Dk Kitila Mkumbo ambazo wanapaswa kujieleza kwa siku kumi na moja, kisha watapata fursa kujieleza mbele ya kamati kuu maalumu kwanini wasifukuzwe Chama.
Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa habari na Uenezi John Mnyika, alisema barua hizo zipo tayari na wahusika watapatiwa wakati wowote kuanzia leo Novemba 26.

Mnyika alikuwa akitoa taarifa ya kikao cha Utekelezaji cha sekretarieti ya chama hicho iliyoketi baada ya mkutano wa kamati kuu iliyoketi tarehe 20 – 22 Novemba mwaka huu.

Ni katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu alisema kuwa mkutano uliofanywa na Zitto na Dk Kitila mbele ya waandishi hawajazungumzia tuhuma zinazowakabili, badala yake walichofanya ni  kujitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.

Lissu alisema, Zitto na Dk Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, Uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu zingine, na walitaja  hizo sababu ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii.

“Walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" (kubadili mwelekeo) wa  mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya Chama.  anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu" alisema Lissu.

Aliongeza kuwa Chadema kina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na kamati kuu, Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika kamati kuuu

Aidha Lissu alieleza kuwa Dk Kitilla anapotosha umma na wanachaka kwa kauli yake kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu, alimtaka Kitila na Zitto waangalie vema katiba ya chama hasa majukumu ya kamati kuu, pale yanaporuhusu Mwanachama yeyote kusimamishwa au kufutiwa uanachama haraka kama kamati kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya vile.

Kigaila alisema, Kamati kuu iliyoketi Novemba 20-22/2013 ilipitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ifuatavyo.

22/11/2013-14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa  wanachama, 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji, 16 januari 30 Januari 2014 Rufaa naukaguzi, ambapo tarehe 01 Februari hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.

Chadema pia ilisema 16 Februari hadi 29 mwezi huo huo ni kusikiliza rufaa na ukaguzi, ambapo uchaguzi wa majimbo utaanza rasmi 1 Aprili hadi Aprili 10, huku uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi mei 5 mwaka 2014, na ngazi ya Mikoa ni 20 Mei hadi 25 Mei.

Huku uchaguzi wa kanda ukitarajiwa kufanyika Julai 9, na haada ya hapo Julai 23 hadi Julai 30 utakuwa ndio muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha uchaguzi wa ndaniya chama.

CHEKA KUTETEA TAJI LA WBF APRIL 2014



  1. 22 November 2013
  2.  
  3. Attention:  Mr Kevin Luandes/Mr Yassin Abdallah
  4.  
  5. SANCTION APPROVAL:  FRANCIS CHEKA V TBA
  6. WORLD BOXING FEDERATION WORLD SUPERMIDDLEWEIGHT TITLE – APRIL 2014
  7.  
  8. Dear Sirs
  9.  
  10. This is to confirm that the World Boxing Federation, www.worldboxingfederation.net has officially approved and sanctioned the WBF first world title defense of champion, Francis Cheka against an opponent to be approved by the sanction committee of the WBF.
  11.  
  12. Mr Kevin Luandes has been approved to promote such a defense conditional to the fight taking place before the end of April 2014, and subject to the rules and regulations of the WBF.
  13.  
  14. All sanction fees must be paid in full and in reflect in the WBF account no later than 3 weeks prior to the staging of this fight.  Failure to comply with this may result in the WBF withdrawing its sanction for this fight.
  15.  
  16. The officials assigned to this WBF world title fight are:  Supervisor:  President of the WBF Howard Goldberg, Referee:  Darryl Ribbink, Judges Edward Marshall and two Tanzanian judges.
  17.  
  18. Howard Goldberg
  19. President WBF
  20.  
  21. 00 27 21 5510896
  22. 00 27 845814612
  23. ironfistpro@iafrica.com
  24. manic@iafrica.com
  25. Skype:  wbfpresident
  26. www.worldboxingfederation.net

KINANA ATEMBELEA KUKAGUA MAENDELEA YA MIRADI JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikata mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wanafunzi waongeze bidii kwenye masomo kwani elimu haina mwisho.

Sunday, November 24, 2013

KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA FILAMU YA DJ MARKETING AND PROMOSHEN YATOA MSAADA


Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kulia akigawa sabuni za Twiga Soup ambayo nayo inasambazwa na kampuni hiyo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo imetoa sabuni na baadhi ya nguo kwa watoto hawo
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Nassoro Hamisi kulia wengine ni Omari Saiki na Ramadhani Rashidi wanaolelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita   
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya usambazaji wa Filamu nchini Tanzania na bidhaa mbalimbali ya DJ Marketeng and promosheni chini ya mkulugenzi wake Daniel Haule mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa msaada wa sabuni ya  unga ya Twiga  ambayo wanazisambaza  na kuwapatia  watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam zawadi ya sabuni hizo

mbali na sabuni hizo za twiga walitoa na baadhi ya nguo kwa watoto wanaoishi hapo mkurugrnzi huyo ambaye amewaomba watu mbalimbali kusaidi watu wenye maitaji maalumu kama hawo ambao wengine ni walemavu wa macho

akielezea historia yake Haule ambaye ni mkurugenzi kwa sasa amesema unajua mie nimelelewa katika mazingila magumu sana kifupi mimi ni mtoto wa mtaani ambapo maisha mengi nimeishi kwenye mitaa nikiwa nalala nje
hivyo nimefutika katika kidogo nilicho nacho leo nakula na wenzangu naomba watu wawe na moyo wa kujitoa ili kusaidia maisha ya watoto hawa ili waonge mbele

nae Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka amesema huu ni mwanzo tu wa kujenga mahusiano hivyo tunajipanga ili mradi kila wakati tuwe tunawakumbuka mana maisha haya awajajitakia bali ni mungu ndie muweza wa kila jambo
Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inatamba na filamu zake mbili za Dasmila na Trouble Make ambazo zimeshirikisha wasanii mbalimbali wanaotamba katika tasnia hiyo

STARTIMES KUBURUDISHA WATEJA WAKE MSIMU HUU WA SIKUKUU


  Meneja Mauzo wa Channel wa Kampuni ya Star Times Bw.David Kisaka kushoto akiongea na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusu kuwazawadia wateja wake kwa njia mbalimbali ikiwemo simu za mkononi,fulana,mafuta ya kupikia, pamoja na mchele kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka
logoSTAR MEDIA (TANZANIA) LIMITED
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

For immediate release                  

STARTIMES KUBURUDISHA WATEJA WAKE MSIMU HUU WA SIKUKUU
22 Novemba2013,Dar-Es- Salaam:
Kampuniinayoongoza Tanzania katika TV zadigitali, Star Media Tanzania inayojulikanakama “StarTimes” inayoendeleakuburudishanakuelimishamamiayamaelfuyaWatanzaniainatangazauzinduziwapromosheniyakeyamsimuwasikukuukuanzia18 Novemba 2013 hadimwishowaJanuari 2014.
"Tungependakuwazawadiawatejawetuwamudamrefuna wale wapyakatikamsimuhuuwasikukuukwakuwapamachaguomengizaidiyavituovinavyoangaliwasana, pamojanazawadinyinginezo. WatejawatakapowekaTsh 80,000 katikapromoshenihii, watapatasimuyamkononiyenye line mbiliainaya M35 StarTimesambayoinatoahudumaya TV zadigitalipopoteulipo.'' alisemaKaimuAfisaMtendajiMkuuBw. Jack Zhou.
WatejawaStarTimespiawatapewamwezimmojawaburewakuangaliakifurushi cha juuzaidi “Kili” chenyethamaniyaTsh 40,000 watakaponunuaking’amuzi. ZawadinyinginewatakazopatawatejawatakaowekaTsh 40,000 nipamojanafulana, mafutayakupikia au mchele.
Mr Zhou alielezeazaidiahadiyaStarTimesyakuwatumikiaWatanzaniakwakuwapatiamatangazoyadigitaliyenyeuborawahaliyajuukatikamahitajiyaainambalimbali.
"Tunaonafaharikuwanazaidiyavituo 70 nahivikaribunitumeongezavituovitatuvyaFilamuviitwavyo, Star One ambachohuonyeshafilamuzilizotokahivikaribunizikiwemozilizofanyavizurikimauzo Hollywood, Star Movie 1 + 2, na Star Africa ambachohuonyeshafilamuzaKiafrika.” AliongezaBw. Zhou.
VituovinginenipamojanaSentanta Action ambayoitakuwakivutiokwamashabikiwandondina FLN (Fine Living Network), ambayoitalengamasualayoteyamienendoyamaishayakisasa.Watotowataburudishwanakuelimishwakupitia "Jim Jam" namatangazoyataarifazahabariyatapatikanakwenyevituoviwilivilivyoongezwahivikaribuni, Fox News na Bloomberg.
KatikakutimizaahadiyaStarTimesyakuongezavipindikutokanyumbani, SibukaMaishaitakuwainarushamchezowakuigizawa Kiswahili- 'High Heels" mwanzonimwaDesemba. Ili kupatakituohii, watejawatatakiwakulipanyongezayakilamweziyaTsh 3,000 tu.
Katikahatuanyingine, StarTimesinapanuahudumazakekwendamikoamitatuzaidi, ambayoniMusoma, TaboranaSingida.
HukoMusoma, TaboranaSingida, matangazoyakohewanikwasasawakatihukoKahamanaBukobawatazamajiwatawezakupokeahudumazaStarTimesmwishonimwaNovemba.
HiiitafanyaidadiyaofisizaStarTimeskufikia 14 nakuifanyaStarTimeskuwanikampuniya kwanza ya TV zadigitalikufanyashughulizakekatikamikoamingizaidinjeyaDar es Salaam.
TanguStarTimesilipozinduliwanchini Tanzania, kampuniimewekezazaidiyaDolazaKimarekanimilioni 265 nainabakiakuwakampuniyaving’amuziinayopendelewazaidinawatumiajiwamajumbani. Utawala wake katikasokoniushahidiwahudumazakezahaliyajuukwawatejanaorodhayakendefuyavituo.

KUHUSU STARMEDIATANZANIA
Star Media (Tanzania) Limited (jina la biashara - "StarTimes") ilizinduliwanchiniTanzania mwaka2009.Imewekaniayakuiwezeshakila kaya nchini Tanzania iliiwezekupatamatangazoya TV yadigitalikwabeinafuu, yenyeuboranawawezekuyafurahia.
WatejawanawezakupataStarTimesnchinikotekwakupitiaving’amuzinakwaDar es Salaam naArusha, wanawezapiakupatakwakupitiasimuzamkononi, TV ndogona TV zakwenyemagari.
Star Media mpakasasaimetengenezaajira370 zamojakwamojanaajira1750kwanamnanyingine.
Ni sehemuyaStar Media; kampuniinayoongozakatikakutoahudumazaTV zadigitalinchini China. Star Media inakampuni10 baraniAfrika: Kenya, Burundi, Tanzania, Guinea, Nigeria, Uganda, Rwanda, Afrikaya Kati, Msumbijiand DRC. HivikaribuniitafunguakampuniAfrikayaKusini, Malawi naGhana.

KWA MAWASILIANO:
David Kisaka
Simu: 0717073495    
Baruapepe:davidkisaka@yahoo.com
Kwamaelezozaiditembelea:www.startimes.co.tz/ kwenyeface book natwitter:TZStarTimes






MAJANGA!!!! KOPE BANDIA ZAMPOFUA MACHO MREMBO....ALIKWENDA SALUNI KUBANDIKWA KWA SUPA GLU...SOMA ZAIDI HAPA MKASA HUU




AMA kweli hujafa hujaumbika, mrembo Khadija Omar, mkazi wa Kigogo, Dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo....



Khadija Omar, mkazi wa Kigogo amepata pigo kufuatia kupofuka macho.
Tukio hilo lilitokea Novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo.

Akizungumza na paparazi wetu juzi huku akimwaga machozi, Khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya.


“Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga.


“Muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu walitumia gundi kali, ikabidi nirudi nyumbani,”alisema Khadija.

Akaongeza: “Nikiwa njiani macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini. Akatokea msamaria mwema na kunipeleka nyumbani,” aliongeza.    
                                                              
 Khadija Omar, mkazi wa Kigogo.

Khadija alisema kesho yake alikimbizwa Hospitali ya Amana, Dar ambako alipatiwa dawa bila ya kutolewa kope hizo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nilipofika nyumbani hali ilizidi kuwa mbaya nikalazimika kupelekwa  Hospitali ya Macho ya CCBRT (Msasani, Dar) ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo,” aliongeza Khadija kwa majonzi.

Alisema kule CCBRT alijikuta akiangua kilio baada ya madaktari kumwambia kope hizo haziwezi kutolewa mpaka zikatwe na mkasi.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Jumapili iliyopita Khadija aliweza kufungua macho kwa mara ya kwanza tangu alipotokewa na hali hiyo lakini bila kuona sawasawa.


Jumatatu iliyopita Khadija aliruhusiwa kurudi kwake lakini akiwa hana uwezo wa kuona na kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo baada ya wiki tatu kwa uchunguzi zaidi.

Daktari mmoja wa CCBRT ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini alisema: “Khadija anaweza kuona kama zamani lakini itamchukua muda mrefu kutokana na madhara ya gundi ya ‘supa glu’ iliyotumika.

Taarifa zaidi zinasema, Jane na Koku wafanyakazi wa saluni waliomuweka kope hizo Khadija  walikamatwa na Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba MGN/RB/13021/2013.

-GPL

Mahafali ya Tano ya Kidato cha Nne Mwandege Boy's yalivyofana leo Mkuranga


Wanafunzi waliosalia shuleni wakisimama kumpokea mgeni rasmi
Hata wazazi na walezi nao walisimama wima
Pre Form One nao walikuwapo katika mahafali hayo
Wanafunzi wa kidato wa tatu wakionyesha onyesho la lugha ya Kiswahili kusherehesha mahafali hayo ya leo
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wakiwa wametulia vitini
Mwandege Boys kuna vipaji vya uigizaji usipime!
Yaani ni Full Kidigitali Mwandege Boys
Igizo likiendelea kuhusiana na umuhimu wa kuzingatia masomo shuleni

MALINZI AMRUDISHA MWAKALEBELA TFF, WAPO PIA NASSIB NA MADEGA


RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogondogo wakiwemo Katibu Mkuu wa zamani, Fredrick Mwakalebela na Makamu wa pili wa TFF aliyemaliza muda wake, Ramadhani Nassib (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya Utendaji.
Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.
Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.
Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega.
Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.

Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.

Saturday, November 23, 2013

KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA FILAMU YA DJ MARKETING AND PROMOSHEN YATOA MSAADA

Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kulia akigawa sabuni za Twiga Soup ambayo nayo inasambazwa na kampuni hiyo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo imetoa sabuni na baadhi ya nguo kwa watoto hawo
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Nassoro Hamisi kulia wengine ni Omari Saiki na Ramadhani Rashidi wanaolelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita 
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya usambazaji wa Filamu nchini Tanzania na bidhaa mbalimbali ya DJ Marketeng and promosheni chini ya mkulugenzi wake Daniel Haule mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa msaada wa sabuni ya  unga ya Twiga  ambayo wanazisambaza  na kuwapatia  watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam zawadi ya sabuni hizo

mbali na sabuni hizo za twiga walitoa na baadhi ya nguo kwa watoto wanaoishi hapo mkurugrnzi huyo ambaye amewaomba watu mbalimbali kusaidi watu wenye maitaji maalumu kama hawo ambao wengine ni walemavu wa macho

akielezea historia yake Haule ambaye ni mkurugenzi kwa sasa amesema unajua mie nimelelewa katika mazingila magumu sana kifupi mimi ni mtoto wa mtaani ambapo maisha mengi nimeishi kwenye mitaa nikiwa nalala nje
hivyo nimefutika katika kidogo nilicho nacho leo nakula na wenzangu naomba watu wawe na moyo wa kujitoa ili kusaidia maisha ya watoto hawa ili waonge mbele

nae Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka amesema huu ni mwanzo tu wa kujenga mahusiano hivyo tunajipanga ili mradi kila wakati tuwe tunawakumbuka mana maisha haya awajajitakia bali ni mungu ndie muweza wa kila jambo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...