Saturday, May 29, 2010

50 CENT AJIKONDESHA KWA AJIRI YA KUJINYIMA KULA


50 Cent ajinyima kula ili akonde

NEW York, Marekani

MWANAMUZIKI 50 Cent, amefanya mazoezi magumu ili kupungua uzito kwa ajili ya kuigiza filamu.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 34, mbali ya kufanya mazoezi amejinyima chakula kwa wiki tisa kwa ajili ya kucheza filamu, akiigiza kama mwanasoka wa Kimarekani anayepambana na kansa.

Nyota huyo wa In Da Club, alikuwa akitumia saa tatu kwa siku kwa kufanya mazoezi na kupungua uzito kwa ajili ya kucheza picha ya Things Fall Apart.

Mzaliwa huyo wa New York "Fiddy" ambaye jina lake ni Curtis Jackson, ametumia picha yake kwenye Twitter yake ambayo inaonesha jinsi alivyokonda kama mtu aliyeteseka kwa njaa.

Mbali ya kutunga nyimbo na kuimba, mwanamuziki huyo wa amekuwa na kipaji cha kuigiza filamu, amesema anawaza kama anaweza kurudisha mwili wake baada ya kuisha kwa filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment