Saturday, May 29, 2010

ADRIANO ATIMKIA ROMA

Adriano atimkia Roma

Rome, Italia

MSHAMBULIAJI wa Flamengo, Adriano anajiandaa kurejea tena Italia. Mchezaji huyo wa zamani wa Internazionale amesema yuko mbioni kujiunga Roma.

Nina furaha kurejea Italia, nilihitaji kitu fulani kwa ajili ya kufuata wakati mbaya na ninahisi kuwa nimejitoa kwa watu wa Italia," alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Baada ya kujifunza sana nikiwa Flamengo, ninajijisi kuwa ninaweza kufanya vizuri. Ni uamuzi ambao nineufikiria kwa muda mrefu, kwani nimefurahi kwa kurejea makao makuu ya nchi.

Ni miongoni mwa sababu zilizofanya nichague Roma, Nimeona ni sehemu inayonifaa zaidi kuliko fedha. Ninapenda mipango yao wamekuwa wakinifuatialia mimi kwa miezi sita.

Ingawa uhamisho haujakamilishwa, Adriano anatumaini kuwa atavalia jezi za Giallorossi, ndani ya wiki chache.

Kwa asilimia 90 ni mchezaji wa Roma na nimezunguma na Rais wa Klabu, Rosella Sensi ili Juni 6, mwaka huu kumalizia usajili.

"Sina matatizo na Flamengo ya kuhamia niliondoka hapa kirafiki. Nilikuwa na furaha sana lakini leo (jana) ninajisikia muhimu kurejea Italia. Sitakia kurudia mambo yaliyotokea kwangu.

"Siko kwenye kiwango cha juu kama Francesco Totti, lakini ninasonga mbele kufikia kiwango chake na ninaweza kutoa mchango kwa Roma," alisema.

No comments:

Post a Comment