Tuesday, May 25, 2010

BENDI ya muziki wa dansi Orchestra Mlimani Park yakamilisha mbili myaa

BENDI ya muziki wa dansi Orchestra Mlimani Park
maarufu kama wanasikinde ngoma ya ukae imekamilisha
nyimbo mbili tayari kwa maandalizi ya albam mpya.
Ofisa habari wa bendi hiyo Jimmy Chika alizitaja nyimbo
hizo kuwa ni Tunu ya upendo iliyotungwa na mwimbaji
mkongwe Shaaban Dede na CCM uliotungwa na
wanamuziki wa bendi yote kwa pamoja.
Chika alisema nyimbo hizo zimendaliwa ikiwa ni mwanzo
wa kuanza albam nyingine baada ya kukamilika ile ya
awali inayojulikana kwa jina la Supu umetia nazi.
Naye katibu wa bendi hiyo Hamisi Milambo alikanusha
uvumi ulioenea kwamba mpiga gitaa la besi wa bendi hiyo
Shaaban Mabuyu ameihama bendi hiyo na kujiunga na
bendi ya Tlent inayomilikiwa na aliyekuwa kiongozi wa
bendi hiyo Hussein Jumbe.
Alisema Mabuyu yupo kundi kama kawaida na kwamba
jumapili iliyopita alikuwa miungoni mwa wanamuziki
waliotumbuiza kwenye ukumbi wao wa nyumbani DDC
Kariakoo.
Alisema kufuatia tukio hilo Milambo alisema kwamba
wanachama wa bendi hiyo wanaoujulikana kama Sikinde
Familly

No comments:

Post a Comment