Friday, May 21, 2010

Cech ampigia debe James kwa Capello


Cech ampigia debe James kwa Capello

LONDON, England
MLINDA mlango wa Chelsea, Petr Cech, anaamni kuwa, kipa wa timu ya Portsmouth, David James, anapswa kuwa namba moja wa timu ya Taifa ya England wakati wa fainali za Kombe la Dunia za majira haya ya joto.

Mwishoni mwa wiki, Cech alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa Chelsea wa bao 1-0 dhidi ya Portsmouth katika mechi ya fainali ya Kombe la FA baada ya kuokoa mkwaju wa penalti iliyochongwa na kiungo wa Pompey, Kevin Prince Boateng.
Hata hivyo, pamoja na ushujaa huo, kipa huyo wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Czech, anaona kuwa, mlinda mlango huyo ana kiwango cha hali ya juu.
Katika kuwania nafasi hiyo, James atakuwa akichuana na makipa Robert Green na Joe Hart, lakini Cech anaamni kuwa, mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 39 anapaswa kuwa chaguo la kwanza la kocha Fabio Capello wakati wa fainali hizo zitakazofanyika nchini Afrika Kusini.

"Nadhani ana uzoefu kuliko walinda malngo wote wa England na ameokoa mabao mengi katika mechi hii,” Cech aliliambia gazeti la The Mirror.
"Jambo la muhimu sana kwake ni kwamba, yupo katika hali nzuri na anacheza, kwa mtazamo wangu ni mlinda mlango namba moja," aliongeza.

No comments:

Post a Comment