Wednesday, May 26, 2010

CHIKICHA ORIGINAL BAND KUZINDULIWA JUNI 5

Chikicha Original Band kuzinduliwa Juni 5 Bagamoyo



Na Mwandishi wetu, Bagamoyo

WAKAZI wa mjini Bagamoyo na wa vitongoji vyake wanajiandaa kuona uzinduzi wa bendi mpya ya muziki wa dansi ya Chikicha Original band ambao utafanyika siku ya Jumamosi ya juni 5 kwenye ukumbi wa Saadan Club mjini Bagamoyo.

Mratibu wa uzinduzi huo Edgar Nazar wa kampuni ya Edgar Arts Promotion Co. Ltd amesema kuwa kila kitu kimekamilika ambapo wakazi wa Bagamoyo na wa vitongoji vyake wasubirie kuona raha kutoka katika bendi hiyo mpya ambayo itakuwa na maskania yake mjini Bagamoyo.

Amesema kuwa katika kuipanga kuishindania imefanikiwa kuwakamata nyopta wawikli ambao ni repa na mwimbaji Masoud Kilimanjaro ‘Masoud wa Ukweli’ aliyewahi kuwa mwanamuziki wa Genda E’ka ya Bagamoyo na Elly Chinyama ambaye ni mpiga gitaa la solo.

“Ni wapenzi wa muziki wa dansi kuja kuingalia bendi yao mpya kwa kiingilio kidogo cha shilingi 3,000 huku unaondoka na bia moja ya bure mlangoni, pia ni siku ya pekee kuja kuwaona wanenguaji wa ukweli watakaoonyesha umahiri wa kucheza Chikicha Original” amesema Edgar.

Ameongeza onyesho hilo la uzinduzi wa Chikicha Original Band umedhaminiwa na kituo bora cha Redio 100.5 Times Fm mguso wa jamii, Top Life Bar, Pop Juice Safari’s na gazeti la Sauti huru.

No comments:

Post a Comment