Monday, May 31, 2010
NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUHAKIKISHA WANATENGA BAJETI YA MICHEZO MBALIMBALI
ABDALAH MAGONZA
Na Benedict Kaguo,Tanga
NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo,Joel Bendera ameziagiza Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha wanawatengea bajeti kwa ajili ya michezo,Maofisa Utamaduni ili waweze kufufua michezo kwenda sambamba na Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuhamasisha michezo hasa wa riadha.
Bendera alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa RCC kilichokutana kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa.
Alisema Halmashauri za Wilaya,Miji,Manispaa na Majiji hazina budi kutenga bajeti ili kuwawezesha Maofisa Utamaduni waweze kufanya kazi yao ya kuinua michezo mbalimbali katika Halmashauri hizo.
"Sote tunatambua kuwa michezo ni furaha,Amani,na ajira sasa ni vema Halmashauri zikatenga fedha kwa ajili ya maendeleo ya michezo kuanzia ngazi za chini"alisema Bendera.
Aliwataka viongozi wa Mkoa wa Tanga kushirikiana katika kuhamasaisha michezo ili kupunguza matatizo mbalimbali ndani ya jamii ikiwemo ugonjwa wa UKIMWI,matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu.
No comments:
Post a Comment