Tuesday, May 25, 2010

SASA NCHI YAELEKEA KUBAYA,MAKARANI WA MAHAKAMA MBOZI WADAIWA KUIBA VIELELEZO VYA KESI FVYENYE THAMANI YA SH,MILIONI 25

SASA NCHI YAELEKEA KUBAYA,MAKARANI WA MAHAKAMA MBOZI WADAIWA KUIBA VIELELEZO VYA KESI FVYENYE THAMANI YA SH,MILIONI 25


Na Moses Ng’wat,
Mbozi.

SAKATA la kuibiwa vocha za ruzuku za pembejeo zenye thamani ya shilingi milioni 86,lililowahusisha watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,na baadaye kushinda kesi,limeibua utata mpya baada ya vielelezo vya vyocha zilizotumika kama ushahidi zenye thamani ya sh,millioni 25 kudaiwa kuibwa zikiwa zimehifadhiwa katika bohari(Stoo )ya mahakama.

Wizi wa vielelezo hivyo ulibainika baada ya ofsi ya kilimo na mifugo wilaya ya hiyo kuziomba vocha hizo kutoka mahakamani hapo baada ya kesi kumalizika,ili ofisi hizo izihifadhi kusubiri maelekezo ya ya Wizara.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba vocha hizo za vielelezo zilizoibiwa zikiwa mikoni mwa mahakama ya wilaya ya Mbozi ni vitabu kumi vyenye thamani ya shilingi milioni 25, huku vitabu vingine vyenye thamani ya shilingi mlioni 62 hazikuweza kupatikana.

Vielelezo hivyo vilikuwa mahakamani hapo tangu kutokea kwa tukio la wizi wa pembejeo hizo octoba 17 mwaka jana ambapo jumla ya watumishi watano wa halmashauri hiyo walikamatwa na kufikishwa mahakamani na baadaye kushinda kesi.

Taarifa za ndani ambazo gazeti hili ilizipata zinadaiwa kuwa mara baada ya kesi hiyo kumalizwa katika mahakama hiyo wakala wa pembejeo za kilimo aliyeko mjini Vwawa wilayani Mbozi(jina linahifadhiwa) alianza kuhaha kutafuta mbinu za kupata vielelezo hivyo kutoka katika mahakama ya wilaya ili aviingize benki ya NMB kwa ajili ya mchakato wa kupata fedha.

Inadaiwa kuwa katika hali ya kushangaza wakala huyo alifanikiwa kupata vocha 1000 ambazo ni vitabu kumi vilivyokuwa vielelezo katika kesi iliyomalizika kupitia kwa mmoja wa watumishi wa mahakama ya wilaya ambaye anadaiwa kupewa kiasi cha sh. Milioni 7.

Habari za uhakika zinadai kuwa baada ya wakala huyo kupata vitabu hivyo kupitia mtumishi wa mahakama kwa njia ya magendo kwa malipo ya sh. Milioni 7,alilazimika kuvipitisha katika ofisi ya idara ya kilimo wilayani humo ili visainiwe kulingana na taratibu za mchakato wa pembejeo hali ambayo ilishitukiwa na mmoja wa maofisa wa kilimo.

Mara baada ya ofisa kilimo kushituka baada ya kubaini kuwa vitabu hivyo ni vielelezo vya mahakamani ambavyo kesi yake imemalizika hivi karibuni akaamua kutoa taarifa katika Benki ya NMB ili isiweze kuvithibitisha na kutoa fedha.

Baada ya kupata taarifa hizi waandishi wa habari wanaofuatilia sakata hili walimfuata Ofisa Kilimo wa wilaya, Richard Silili kujua ukweli wa upotevu huo alikiri kuwa ofisa wake mmoja alisaini vitabu hivyo kumi na kushtuka ambapo yeye alimtuma kwenda kutoa taarifa katika benki ya NMB ili izuie kupokea vocha hizo kutoka kwa wakala huyo.

Aliendelea kusema baada kubaini kuwa wakala huyo ameendeleza mchezo mchafu juu ya vocha hizo ofisi yake iliamua kuioandikia mahakama barua ya kuomba kuchukua vitabu kumi vya vocha za pembejeo zilizotumika kama kielelezo katika kesi namba 167 ya mwaka 2009.

Barua hiyo yenye kumbukumbu A 30/MDC/10 ‘’E’/126 ya Machi 22, 2010 ilyoelekezwa katika mahakama ya wilaya kutoka idara ya kilimo wilaya ilikuwa na lengo la kutaka kuvichukua ili virudi katika ofisi ya kilimo wilaya ili kusubiri maelekezo kutoka wizarani jinsi zitakavyoweza kutumika au vinginevyo.

Hata hivyo mara baada ya kupelekewa barua hiyo kwa takribani kwa takribani miezi miwili mahakama hiyo haikuweza kutoa jibu kwa njia ya maandishi badala yake ilidaiwa kuwa baadhi ya maofisa wa mahakama hiyo walitoa majibu yam domo kuwa vitabu hivyo havionekani katika stoo ya mahakama hiyo.

Aidha, Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo za kilimo wilaya ya Mbozi ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo Gabriel Kimolo alipoulizwa juu ya sakata hilo alishangaa kuwepo kwa taarifa za upotevu wa vielelezo hivyo mahakamani na kueleza kuwa anachojua kuwa bado vipo mahakamani na utaratibu wa kuvichukua ulikuwa ukiendelea.

Hata hivyo alionekana kuhamaki na kueleza kuwa anachojua yeye ni kwamba kamati yake ilikuwa iketi kujadili tathmini ya kilimo kwa msimu uliopita ambapo suala la wizi wa pembejeo za kilimo za sh. Milioni 87 zikiwemo zile za vielelezo ambazo zilikuwa mahakamani zenye thamani ya sh. Milioni 25 ilikuwa ni miongoni mwa ajenda za kujadiliwa.

Uchunguzi wa sakata hilo ulibaini kuwa baada ya mahakama ya wilaya kupata taarifa hiyo, viongozi wake wa ngazi ya juu waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi juu ya upotevu huo polisi kupitia RB namba MBO/RB/1024/2010 ya Mei 18 mwaka huu.
ili tatizo hilo lisibaki mikononi mwao huku wakiendelea na jitihada za kubaini ni nani aliyehusika kutoa vielelezo hivyo mahakamani hapo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la upotevu wa kielelezo mahakamani na kwamba jeshi la polisi tayari limewakamata watumishi wawili wa mahakama hiyo ya wilaya na kuhojiwa,ingawa hakuwataja majina yao.

Watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya hiyo waliohusishwa na wizi huo na baadae kushinda kesi ni Charles Makunja, ofisa Kilimo Asante Ndimbo (46), Joseph Mbogela(59)afisa kilimo, Tekra Luoga (54) Mtunza Bohari, Maiko

No comments:

Post a Comment