Tuesday, May 18, 2010

WAJASILIA MALI WAPIGWA MSASA


mmoja wa wajasilia mali akitoa neno la shuklani

Waandishi wakimuhoji Mwenyekiti wa bodi Bw. Salumu Shamte

Wajasilia mali wakifatilia mada mbalimbali wakati wa semina hiyo

Mkurugenzi wa Halmashaul ya Biashara ya Nje (BET) Bw.Ramadhani Khalfan akizungumza wakati wa semina ya Maonesho ya Kisekta Bidhaa za Sanaa na Utamaduni,Ngozi,Nguo na Mavazi, na Chakula na Usindikaji uliofanyika Dar es salaam jana kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Salumu Shamte

Baadhi ya Wajasiliamali wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa semina ya Maonesho ya Kisekta Bidhaa za Sanaa na Utamaduni,Ngozi,Nguo na Mavazi, na Chakula na Usindikaji uliofanyika Dar es salaam LEO.

WAJASIRIAMALI wametakiwa kuongeza thamani na kuzingatia viwango vya ubora wa bidhaa wanazozalisha za ndani ili waweze kupata soko kwa urahisi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es salaam na Mwenyekiti wa bodi ya wafanyabiashara wa nje Bw. Salum Shimte kuwa kuongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini watapata masoko sehemu mbali mbali.

Alisema kuwa nilazima wahakikishe bidhaa zinazozalishwa na kuongezwa thamani zinamfikia mlaji kwa wakati unaohitajika na kwa bei nafuu.

"Mkusanyiko huu utawapa fursa ya kubadilisha mbinu na teknolojia zinazotumika katika uzalishaji, utasaidia kujenga mitandao ya kibiashara hatua itkayosaidia kuongeza ufanisi na tija katika kazi zao,"alisema Bw. Shimte.

Alisema kuwa nchi yetu inampango wa kufanya mageuzi makubwa katika sekta mbali mbali za uchumi mageuzi yanayolenga kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima na kuwaongezea kipato.

BW. Shimte alisema kutokana na kuanguka kwa uchumi wa dunia sambamba na kuanguka kwa sekta ya fedha duniani kumeziweka nchi zinazozalisha malighafi Tanzania katika kipindi kigumu sana kiuchumi.

Alisema hivyo usindikaji ndani ya nchi ni moja ya suluhu kwa kuondokana na changamoto za kuanguka kwa bei za mali ghafi katika masoko ya nje.

Hata hivyo alisema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kuwa na makakati wa kuzalisha bidhaa zao zinazopkidhi viwango ili waweze kuondokana na umasiki wa kujitakia.

No comments:

Post a Comment