Friday, May 28, 2010

WAREMBO MBEYA WADAI WAPEWE ELIMU FEDHA ZITAWEZA KUWAREVYA


wadai fedha zinawarevya mamiss,wataka wapewe elimmu kwanza

Na Moses Ng’wat,
Mbeya.

WAKATI mrembo atakayetwaa taji la miss Mbeya mwaka 2010 akitarajia kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja,wadau wa tasnia hiyo wametaka warembo wapewe elimu ya ujasiliamali ili waweze kuwekeza katika miradi,badala ya kutumia fedha hizo kutafuta umaarufu unaowadi na kujikuta kwenye mambo yanayowaletea kashfa.

Shindano hilo litaksalofanyika kesho mei 29 katika ukumbi wa Mkapa jijini hapa
Jumla ya warembo 12 watapanda jukwaani kuwania umalikia huo wa mkoa,huku wakisindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya Dimond Musika ya jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa,Mratibu wa shindano hilo la mkoa wa Mbeya, Fanuel Ndonde,alisema washiriki hao 12 wamepatikana baada ya mchakato kufanyika katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

Aliwataja warembo hao kuwa ni Jeinas Elias, Ntuli Coster,Ide Joghn, ZainabuMatagi,Laila Bashiru,Margareth Luca,Scola Haule,Zainab Shaban,Irene Gerald,Happness James,Shadia Mohammed na Grace Nashon.

Hata hivyo alisema kuwa tayari warembo hao wamlishaanza kambi tangu mei 24,chini ya walimu wao Sharifa Ally na Zaifa Ismail ambao walikuwa warembo wa mkoa kwa nyakati tofauti.

Alianisha kuwa zawadi kwa mshindi wa kwanza ni fedha tasilimu sh,milioni moja, mshindi wa pili shilingi 600,000, watatu shilingi 400,000, wa nne shilingi 300,000,watano shilingi 200,000 na warembo watakabaki watapatiwa kifuta jasho cha shilingi laki moja kila mmoja wao.
Aidha, alisema shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom,Tbl-kupitia Redds,Furniture Center Uhindini,ACL Ltd/ACESS Computer,UCC, Man Company ,PSI kupitia Salama Kondom,My Choice na Bomba fm.
Wadau hao walisema kuwa baadhi ya warembo wanaoshinda mataji na kupata zawadi ya fedha nyingi hujikuta wakishindwa kuwekeza katika miradi kwa ajili ya maisha yao ya baadae kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya ujasiliamali.
Walisema imefika wakati pia kwa waandaji na waratibu wa mashindano ya urembo kuanzia ngazi za mikoa kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya ujasiliamali ili kuwajengea uwezo warembo katika maisha ya kawaida baada ya kumaliza wa kutumikia mataji wanayoyapata.

Mmoja wa wadhamini hao ,Sadock Jonas ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Furniture Centre,alisema wameamua kutoa udhamini huo baada ya kubaini kuwa urembo ni taasisi ya kijamii hivyo inahitaji mchango ili iweze kuifikia jamii.

No comments:

Post a Comment