Saturday, June 12, 2010
BAFANA BAFANA MEXICO ZATOSHANA NGUVU
MAMBO YALIKUWA SI MCHEZOOO
Bafana Bafana, Mexico hakuna mbabe
* Leo Korea Kusini v Ugiriki, Argentina v Nigeria, England v Marekani
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
FAINALI za Kombe la Dunia, zilianza jana kwa wenyeji Afrika Kusini kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mexico, katika mechi ya Kundi A iliyopigwa katika Uwanja wa City Soccer wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 94,700 mjini hapa.
Mshambuliaji Siphiwe Tshabalala aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli la kwanza la michuano hiyo kwa Bafana Bafana katika fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010.
Mchezaji huyo alifunga goli hilo dakika ya 55, lakini matumaini yao ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo, yalikatishwa na Mexico ambayo ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Rafael Marquez, zikiwa zimesalia dakika 11 mpira kuisha.
Mexico ambayo ilitawala kipindi cha kwanza na ilikosa nafasi nyinngi hadi, Tshabalala alipopata pasi nzuri ya Teko Modise na kumfunga kipa wa Mexico, Oscar Perez katika dakika ya 55.
Wakicheza mbele ya mashabiki 90,000, ndani ya uwanja wa wao Soccer City, Bafana bafana hawakuweza kuibuka na ushindi.
Kipindi cha pili Bafana Bafana ikiwa katika jitihada za kuongeza mashambulizi, ilijisahau ambapo kiungo wa Mexico, Marquez aliinasa vizuri pasi ya Andres Guardado na kufunga goli la kusawazisha.
Timu zote zilicheza kwa nguvu kutaka kupata goli la ushindi na Katlego Mphela, angeweza kufunga goli la ushindi dakika 85 wakati alipopiga shuti na mpira kugonga mlingoti wa goli na kurudi uwanjani.
Awali Mexico ilifunga goli dakika ya 38, lililofungwa na Carlos Vela lakini lilikataliwa na mshika kibendera kwa madai kuwa mfungaji akulikuwa ameotea wakati beki mmoja Bafana Bafana alikuwa kwenye mstari wa goli pamoja na kipa ambaye alitoka.
Afrika Kusini inayonolewa na Carlos Perreira, ilijibu shambulizi dakika ya 44 ambapo, Tshabalala aliunganisha mpira wa kona na kipa Perez aliupangua na kuwa kona nyingine.
Mechi hiyo ilitanguliwa na sherehe za ufunguzi wa mashindano zilizoongozwa na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliyefungua rasmi mashindano hayo, Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter aliyetoa iliyeipongeza Afrika Kusini kwa maandalizi mazuri.
Akizungumza kabla ya mashindano hayo Rais Zuma, alito salamu kutoka kwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye hakudhuria ufunguzi huo kutokana na kufiwa na mjukuu wake, Zenani Mandela (13) kilichotokana na ajali ya gari.
Watu wngine maarufu waliokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na Rais wa Mexico, Felipe Calderon na Makamu Rais wa Marekani, Joe Biden.
Katika mfululizo wa mashindano hayo leo kwenye Kundi A, Korea Kusini itapambana na Ugiriki mechi itakayochezwa Uwanja wa Nelson Mandela Bay saa 8:30 na mechi nyingine ya kundi hilo, Argentina itachuana na Nigeria katika Uwanja wa Ellis Park saa 11 jioni.
Mechi nyingine inayotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki itakuwa kati ya England na Marekani ya Kundi C, ambayo itachezwa saa 3:30 usiku kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Afrika Kusini wakishangilia bao lao lililofungwa na Siphiwe Tshabalala katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia iliyochezwa jana katika Uwanja wa Soccer City, ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
No comments:
Post a Comment