Thursday, June 17, 2010

Benitez apendekeza Danglish kumrithi Liverpool

ROME, Italia

KOCHA Rafa Benitez anaamini kuwa mtu anayefaa kuchukua nafasi yake katika timu ya Liverpool ni nyota wa Anfield, Kenny Dalglish.

Benitez ametoa baraka kwa King Kenny, baada ya yeye kutangazwa rasmi kuwa mrithi wa Jose Mourinho katika timu ya Inter Milan.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 50, alisisitiza: "Ninafikiri Liverpool inatakiwa kumwangalia, Kenny Dalglish.

"Ni mtu anayefaa kwa kazi ile. Wamiliki wanafaa kuwasikiliza mashabiki kwa kuwa hawana furaha.

Benitez ambaye amekuwa akilipwa mshahara pungufu kwa pauni milioni 10 kwa mwaka dhidi ya ule aliokuwa akipata, Mourinho amsesaini mkataba wa miaka miwili Inter, pia ameeleza kwa mara ya kwanza kuhusu kuondoka kwake Anfield.

Alisema: "Ilikuwa ni wakati mgumu sana kwangu kuondoka Liverpool. Nilikuwa pale kwa miaka sita na mtoto wangu ana miaka saba amekulia pale. Ni Klabu kubwa lakini hali imebadilika.

"Inter ni nafasi nzuri kwangu. Ndiyo, ilikuwa ni ngumu kutondoka Liverpool nilisikitika kuondoka.

"Kabla ya kuondoka nilizungumza na asilimia
95 ya wachezaji wa Liverpool. Wengi walisema asante kwa kila kitu.

"Nilizungumza na Steven Gerrard, katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake alifurahi. Alinitakia kila la Kheri na sasa ameweka mtazamo wake katika fainali za Kombe la Dunia.

"Mahusiano yangu na wachezaji yalikuwa mazuri, pamoja na mashabiki ilikuwa ya kusisimua. Ilikuwa siku ya kusikitisha wakati nilipoondoka, lakini ilikuwa ni lazima kufanya hivyo."

Benitez, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari alimsifu Mourinho aliyehamia Real Madrid, baada ya kuipatia ubingwa wa Ulaya Inter Milan mwezi uliopita. Kocha huyo wa Kireno alikuwa na mahusano mabaya na vyombo vya habari vya Italia.

Lakini Benitez alisisitiza: "Amefanya kazi nzuri hapa. Mimi si mpinzani wa Mourinho.

"Ninapenda kushinda, ninapenda kucheza soka nzuri kwa hiyo sifikiri kama kuna kitu tunatofautiana.

"Sitabadilisha kila kitu kwa sababu ni kwamba haitakwua vizuri. Sijazungumza na Mourinho kwa kuwa nimekuwa bize hapa na yeye pia.

"Pengine nitazungumza naye baadaye wakati kazi zikipungua."

Benitez hakutaka kuzungumzia kuhusu kuleta damu mpya katika timu hiyo kwa sasa na kuongeza kuwa atafanya jambo hilo kwa kushirikiana na Klabu."

Kocha huyo anawapenda wachezaji wa timu yake ya zamani kama, Fernando Torres ambaye alimsifu kwa kupata mafanikio kwa kuwa ni mchezaji anayejituma

Benitez alikubali kujiunga na Inter, mwezi huu baada ya kuombwa wakati akiwa katika kisiwa cha Italia, Sardinia kwenye mapumziko.

No comments:

Post a Comment