Wednesday, June 9, 2010
KUNDI LA WANAUMEHALISI LAVUNJIKA LAANZA WANAUME
KUNDI JIPYA LA WANAUME LIKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
KUNDI la Wanaume halisi lilotamba apo awali sasa limevunjika na kuundwa kwa kundi jipya la Wanaume.
Kundi hilo la Wanaume linaundwa na wasanii sita ambapo ambao awali walikuwa miongoni mwa wasanii 11 waliunda kundi la Wanaume Halisi lililokuwa likiongozwa na mwanamuziki Juma Kassim 'Juma Nature'.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa kundi hilo la Wanaume Hassan Umande alisema, kwa sasa kundi hilo limekuja na mikakati mipya ambapo kundi linaongozwa na misingi ya katiba ambapo kila msanii anayeunda kundi hilo ameweza kupewa katiba hiyo na kuipitia na ndipo wakaingia mkataba chini ya mwanasheria.
"Kundi hili litaongozwa na msingi wa katiba hivyo msanii yeyote atakayekiuka misingi hiyo sheria itambana na kupewa adhabu na uongozi," alisema Umande.
Alisema, wameamua kulipa kundi hilo jina la Wanaume likiwa na maana mwanaume yeyote kutoka maeneo yeyote ya hapa Dar es Salaam na hata nje anaruhusiwa kujiunga na kundi hilo tofauti ya ilivyokuwa awali kwa kundi la TMK Wanaume ambalo lilikuwa likiangalia wanaume wa eneo moja la Temeke
Alisema, kwa sasa wapo katika maandalizi ya albamu yao ya kwanza ya kundi hilo ambapo hadi sasa wameishafanikiwa kurekodi nyimbo nne chini ya TMK Production ambazo ni Poa tu, Mukide, Mapenzi kitugani na Kisimati ambapo baadhi ya nyimbo hizo zitaanza kusikika kesho kutwa katika vituo mbalimbali vya redio.
Aliwataja wasanii hao kuwa ni Richard Shauri 'Rich One', Karim Kazumari 'Kaka Man', Abdul Ally 'Mzimu', David Mpangile 'Daz P', Athuman Yahaya ' A Man' na Juma Mbelwa 'Juma Jazz'.
No comments:
Post a Comment