Marquee
tangazo
Tuesday, June 22, 2010
MPIRA WA JABULANI ULIVYOWEKA HISTORIA KATIKA KOMBE LA DUNIA A.KUSINI
Mtangazaji wa TBC PHILIP CYPRIAN akiwa nchini AFRIKA KUSINI
Na Alice Ngubwene
Kama ilivyo kawaida ya kombe la Dunia huchezwa kila baada ya miaka minne. Mwaka huu kampuni ya ADIDAS maarufu kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo duniani. Katika kombe la Dunia la mwaka huu 2010 mpira maalum unaotumika katika mashinda haya umepewa jiona la Jabulani.
Jabulani maana yake ni Sherehekea/Shangilia kwa lugha ya Zulu ,ni lugha mojawapo kati 11 ya Afrika kusini. Mpira huo umetengenezwa na rangi 11 kwa ajili ya heshima ya lugha 11 za makabila 11 ya afrika kusini na pia ni alama ya wachezaji 11 wa timu ya mpira wa miguu.
Rangi 11 pia zinatoa heshima kwa FIFA inayotimiza mashindano 11 tangu kombe la dunia lianze.
Mpira wa soka kawaida unaundwa na vipande 32 vya ngozi , lakini mpira uliotumika katika kombe la dunia mwaka 2006 ujerumani ulitengenezwa kwa vipande 14 na jabulani imetengenezwa kwa utaalamu wa teknolojia ya juu zaidi ukiwa na vipande 8 tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment