Tuesday, June 1, 2010
WASHINDI WA JIVUNIE SMS WAPATIKANA ZAIN
Meneja mahusiano wa kampuni ya Zain Muganyizi Mutta kushoto Mratibu wa promosheni wa kampuni hiyo Ally Leseko na msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini Bakari Maggid wakiangalia komputa kwa ajili ya kutafuta washindi wa promosheni ya jivunie SMS
Na Addolph Bruno
WASHINDI wawili wameshinda tiketi ya kwenda kuangalia kombe la dunia kombe la dunia kupitia promosheni ya Shinda tiketi ya kombe la dunia na Zain iliyokuwa inayoendeshwa na kampuni hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Masoko wa Zain Nyamizi Mutta mbele ya msimamizi kutoka katika Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bakari Maghi aliwataja washindi hao kuwa ni Joseph Semari ambaye ni Ofisa masoko mkazi wa kampuni ya Bonite Bottlers, mkazi wa Mikocheni Dar es Salaam na Bokeloo Athumani Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kwaludege iliyopo Tanga.
Mutta alisema washindi hao watapata fursa ya kuondoka na mtu mmoja atakayemchagua akiwa ndugu yake au rafiki yake wa karibu na kampuni hiyo itasimamia kwa karibu safari yao.
Alisema washindi hao watakwenda kuangalia fainali hizo zitakazoanza Juni 11 mwaka huu hadi mpaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo atakapopatikana na kupata huduma zinazostaili zote kutoka kwa kampuni hiyo.
Alisema katika promosheni hiyo iliyoanza Mei 17 mwaka huu na kuendelea kwa muda wa siku 84 jumla ya washindi 12 watapata fursa ya kwenda kutizama michuano hiyo mikubwa Duniani ambayo kwa mara ya kwanza inafanyika Afrika tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930 nchini Uluguay.
Mbali na hilo Ofisa huyo aliwataja Oselo Girina na Justine Rugulu kuwa ni washindi wawili walioshinda pesa taslimu Shilingi 500,000 kupitia promosheni ya shinda pesa inayoendeshwa kila siku na kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment