Tuesday, June 22, 2010

ZANTEL YAIMIZA WATEJA KUSAJIRI NAMBA ZAO


Dar es Salaam

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel imetoa wito kwa wateja wake kwenda kusajili namba zao z simu mapema kabla ya siku ya mwisho Juni 30 mwaka huu iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Taarifa ilitolewa kwa vyombo vya habari na Zantel ilieleza Meneja uhusino wa Zantel Bi.Sharon Costa alisema miezi 4 iliyopita Zantel iliandaa promosheni nyingi kwa lengo la kupunguza gharama za matumizi ya simu hali iliyochangia wateja kununua namba kwa wingi .

"Ongezeko hili la wateja wapya liliongeza haja ya kuhamasisha wateja wapya kusajili namba zao kwa kutumia mbinu mpya," alisema

Naye Mkurugenzi wa Mauzo wa Zantel Bw. John Mbaga alisema mkakati mzima wa mauzo ulizingatia usajili wa namba mpya kila wanapouza line za simu.

“Sisi kama Zantel tulilipa kipaumbele Swala la usajili wa namba za simu kuhakikisha hatupotezi mteja yeyote ambaye amejiunga na mtandao wetu,” alisema

Alisema ili kurahisisha usajili na kuhamasisha wengi wajitokeze kusajili namba zao kwani kampuni ya Zantel imeunganisha suala hilo na matumizi ya huduma zake za kibenki za ZPesa ambapo wateja wote watakaojisajili na huduma ya ZPesa namba zao zitasajiliwa papo hapo.

Pia wanaweza kupata bonasi ambayo wanaweza kupata fedha taslim au muda wa maongezi kwa wakala wote wa ZPesa nchini.

“Tumeingiza mbinu tofauti kwenye shughuli zima la usajili wa namba za simu kuhakikisha tunawafikia wateja wetu wote popote pale walipo nchini haswa wale walio vijijini.

Alisema wameungana na Shirika la Posta nchini na kuweka fomu zao za usajili kwenye masanduku yote ya posta nchini ambapo wateja watakaochukuwa barua wanaweza kujaza fomu na kuitumbukiza kwenye sanduku la kutuma barua.mbali na hivyo tumetoa matangazo ya kusajili laini zao kupitia magazeti mbalimbali Nchini

No comments:

Post a Comment