Thursday, June 10, 2010
ZANTEL YAZINDUWA BIDHAA MPYA YA THAMANI
maofisa wa Zantel wakizungumza na waandishi wa habari leo
baadhi ya maofisa wa zantel wakiwa katika uzinduzi huo leo
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya Zantel.Ike Kalu, kulia akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni ofisa wa kampuni hiyo Bw.Brian Karokola
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Toleo la Leo
Dar es Salaam, Juni 10, 2010: Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezinduwa kifurushi kipya cha thamani kwa ajili ya wateja wake wenye matumizi makubwa ya huduma za mawasiliano. Kifurushi hiki ni cha kipekee na nafuu kilichotayarishwa hususan kutimiza mahitaji ya mawasiliano ya wateja ambao huhitaji huduma za mawasiliano mara kwa mara. Kifurushi hiki kinafanana na vifurushi vingine duniani. Kifurushi hiki kitawawezesha wateja wa Zantel kudumisha mahusiano na ndugu, jamaa, marafiki na washiriki wengine kokote walipo duniani kupitia mtandao wake uliosambaa nchi nzima.
Kifurushi cha Highlife ni cha kujisajili ambacho kina sifa 3, simu, intaneti pamoja na kutoa tuzo. Kifurushi hiki kinamuwezesha mteja kupiga simu kwa TSH 3 kwa sekunde kwenda mitandao yote nchini pamoja na nchi 25 duniani.
Ikechukwu Kalu, Mkurugenzi Masoko wa Zantel alisema: “Kifurushi cha Highlife ni cha kwanza aina yake Tanzania kinachokupa thamani na kukuwezesha kupiga simu ndani na nje ya nchini muda wowote kwa gharama nafuu nay a ushindani kuliko zote nchini.” Hii ni ahadi ya ukweli kutoka Zantel kwa wateja daima kuzinduwa bidhaa mpya na kuwapa vifurushi vinavyozingatia mwelekeo wa maisha yao.
Wateja wanaweza kujiunga na kifurushi cha Highlife kwa kupiga *190# na watatozwa TSH 1,000 tu gharama ya kujisajili. Mteja askishajiunga na kifurushi cha Highlife ataweza kupiga simu (Zantel kwenda Zantel, Zantel kwenda mitandao mingine, pamoja na simu za kimataifa) kwa gharama moja ya TSH 3 kwa sekunde. Kwenye intaneti, wateja watapata viwango vya GB 2 kwa gharama ya TSH 10,000 kila wiki au kwa TSH 35,000 kila mwezi. Hii pia ni gharama nafuu sokoni kuliko zote.
“Kifurushi cha Highlife pia kina ofa nzuri za intaneti zinazokupa uhuru wa kutumia intaneti kwa muda unaotaka wakati wowote pahali popote na kwa kasi kubwa kuliko zote” aliongezea Bw. Kalu.
Kifurushi hiki pia kinatoa tuzo kwa wateja wetu kwa uaminifu wao kwa kuwazawadia pointi kwa matumizi ya simu. Kwa kila TSH 1,000 mteja wa Highlife anayotumia atajilimbikizia pointi ambazo anaweza kubadilisha kupata Zawadi mbalimbali kama muda wa maongezi, vifurushi vya intaneti, simu za kisasa kama Blackberry na vifaa vya intaneti (modems). Zawadi zingine ni tiketi za kuangalia mechi za Barcelona uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp jijini Barcelona, Uhispania pamoja na safari za kwenda Dubai.
Kila wanapojiunga na kifurushi cha Highlife utajipatia pointi 20 na kila mwaka utapokea pointi 25 kwa kuendelea kutumia huduma hii.
Zantel inaleta mabadiliko ya mawasiliano kupitia kifurushi hiki cha Highlife. Kudhani kuwa Watanzania wanaweza kuongea kwa gharama moja simu za ndani na nje ya nchi ni jambo ambalo halikudhaniwa linawezekana. Hii ni ishara nyingine kutoka mtandao unaokuwezesha Kuongea Zaidi!
-MWISHO-
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Sharon Costa, PR Manager, ZANTEL, sharoncosta@zantel.co.tz
Kuhusu Zantel:
Hadithi na historia ya kampuni ya simu za mikononi ya Zantel inahusu uwekezaji, ubunifu wa bidhaa bora na za kisasa, na yenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja wake. Licha ya hayo, ni hadithi inayohusu ukuwaji na uwezo wa kutoa faida kubwa kwa watumiaji wa simu za mikononi nchini Tanzania. Ikianzishwa mwaka wa 1999, kampuni ya simu ya Zanzibar ina ubia kati ya serikali ya Zanzibar kwa 18%, kampuni ya simu ya Emirati (ETISALAT) kwa 65%, na kampuni ya Meeco International kwa 17%.
No comments:
Post a Comment