Thursday, July 1, 2010
RAIS WA NIGERIA ASIMAMISHA TIMU YA TAIFA KUTO SHIRIKI MICHEZO YOYOTE YA SOKA KIMATAIFA
Na alice ngubwene
Ndugu mpenzi au mshabiki wa soka popote ulimwenguni , nimesikitishwa sana na kauli ya Rais wa nigeria kuifungia timu yake ya taifa kutocheza mechi za kimataifa kwa muda wa miaka miwili. Katika utaratibu huu napata maswali mengi ambayo yananifanya niulize ni jinsi gani ushiriki wa Serikali katika swala zima la michezo popote duniani, na napata wasiwasi kuwa tunakokwenda kama FIFA haitajizatiti katika kanuni zake basi kila nchi itakuwa inajichukulia maamuzi yake , maana unaweza kusikia hata mpira miguu ukafungiwa bila sababu za msingi!
Katika kauli iliyotolewa juzi na Rais wa nigeria Goodluck Jonathan , inabidi nipate wasiwasi huyu Mshauri wa Rais katika maswala ya michezo ana ufahamu gani haswa katika nyanja hizi, Wakati michezo na haswa soka ni mchezo ambao unatumika duniani kote kama kivutio katika kuleta amani na mshikamano duniani kote, hata nchi zenye vita inapofika swala la michezo watu huweka silaha chini na kufurahia burudani.
Kauli hii naifananisha na ya mtu ambaye hana ufahamu kabisa katika maswala michezo hasa soka na michwezo mingineyo kuwa michezo ni burudani , kama ameshauriwa na mgonjwa labda wa kili hivi yaani sipati picha kabisa. ukifuatilia kwa makini nchi ya Nigeria imekuwa na wachezaji maarufu tanug miaka ya 90 na ulimwengu mzima umekuwa ukitambua mchango wao katika soka. Mchakato wao na chama chao cha soka kimekuwa kiligubikwa na mambo mengi katika uteuzi wa kocha mpya baadaya kumfukuza kocha wao aliyewapeleka katika kombe la mataifa ya afrika Bw. shaibu Amodu na kukaa muda mrefu bila kocha huku cha mpira wa miguu cha nigeria NFF kikiangaika kupata kocha mwingine kwa ajili ya kuongozana timu yao katika mashinda ya WOZA 2010.
kila mtu anatambua ni muda gani Bw Lagerbacks amepokea timu hiyo ya nigeria, inasikitisha sana maana tunasahau kuwa hata uteuzi wake aliofanya katika kikosi hicho uligubikwa na presha kutoka chama chao cha mpira wa miguu NFF. sasa iweje nigeria ifanye maamuzi magumu kama haya ambayo hayaleti kuimarisha bali kubomoa kabisa, kwanini asiunde kamati ambayo itachunguza kwa nini timu imeshindwa kuendelea katika hatua ya pili katika mashindano hayo na baada ya kujua mapungufu hayo yakatafutiwa tiba yake. Mfano hata kuwahusisha wanasoka wa zamani ambao walipata mafanikio ndani na nje ya nchi zao katika ufanya mabadiliko na mapinduzi ndani ya vyama vyao vya mpira.
Katika mashindano lazima tukubali kuwa kuna kushinda na kushindwa , nigeria kama timu za nchi nyingine mfano ureno,ufaransa, uingereza, mexico, italy na nyinginezo nyingi tena bora sana zimeshindwa kufuzu nakuendelea na mashindano hayo. FIFA imeweka wazi kabisa kanuni zake ambazo zinaeleza wazi namna serikali kutokuingilia mambo michezo
.
Nafikiri kukiwa na misingi ya utawala bora katika nchi yeyote ndani ya vyama vya mpira, hiyo tu inatosha kuweka mikakati bora ya kusaidia timu za mpira pamoja michezo mingine kufanya vizuri kitaifa na kimataifa. na Kuzuia sio jawabu litakalosaidia aina yoyote ya mchezo kuunda timu bora hapo siku za usoni , bali ni sawa na kubomoa hata kilo ulichonacho kitaharibika. ni sawa kusimamisha wanafunzi wa shule ambao siku za usoni utegemee watatoa matokeo bora ya mtihani!!
kwa maoni zaidi wasiliana na 0733 660669
No comments:
Post a Comment