Tuesday, August 31, 2010
Monday, August 30, 2010
VODA COM YAFUTULISHA TANGA
precision-air-yazindua-ndege-mpya
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 iliyopewa jina la "Bukuoba" yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk
Meneja wa Uhusiano wa Kampuni ya SCANAD Barnabas Lugisha akiwa na mmoja wa waalikwa katika ndege hiyo mpya ilifanya safari kati ya Zanzibar na Dar es salaam leo kwa ajili ya uzinduzi rasmi. picha na http://fullshangwe.blogspot
C.U.F WALIPOZINDUA KAMPENI ZAO HIVI KARIBUNI
BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WANAFUNZI WALEMAVU
MKURUGENZI WA UKUZAJI RASILIMALI WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA BW. SEIFF MOHAMED (KUSHOTO) AKIMKABIDHI BAISIKELI KWA AJILI YA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA VIUNGO MWALIMU MARIAM KHALFANI (KULIA) KUTOKA SHULE YA MSINGI KILINDONI WILAYANI MAFYA, ANAYESHUHUSDIA NI MKURUGENZI WA MASOKO WA BENKI YA NBC LIMITED BW WILLIAM KALAGHE AMBAO NDIO WAMETOA MSAADA HUO WA SHILINGI MILIONI NANE.
MKURUGENZI WA UKUZAJI RASILIMALI KATIKA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA BW. SEIF MOHAMED (KUSHOTO) AKIPOKEA KUTOKA MKURUGENZI WA MASOKO WA BENKI YA NBC LIMITED BW WILLIAM KALAGHE (KULIA) KAMUSI MAALUM KWA AJILI YA WANAFUNZI WENYE MATATIZO YA USIKIVU KWA AJILI YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KILINDONI ILIYOPO WILAYANI MAFIA, NBC IMETOA VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI NANE KWA AJILI YA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM KATIKA SHULE HIYO, ANAYESHUHUDIA NI MWAKILISHI KUTOKA SHULE HIYO, MWALIMU MARIAM KHALFANI.
MMBWANA MATUMLA APIGWA KWA POINT NA KUPOTEZA UBINGWA WA WBC
Sunday, August 29, 2010
Miss Tanzania 2009 Apongezwa na REDD'S katikua siku yake ya kuzaliwa
Meneja wa Kinywaji cha Redds Primaim Cold, Kabula Nshimo (kulia) akimkabidhi Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald keki ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa katika ukumbi wa Maasai Club mjini Arusha.
Miss Tanzania anaemaliza muda wake akikata keki ya sikukuu yake ya kuzaliwa huku akiwa amezunguwa na baadhi ya warembo wanaotarajia kuwania taji hilo mwaka huu.
Meneja wa kinywaji cha Redds Primaim Cold, Kabula Nshimo akimlisha keki Miss Tanzania anaemaliza muda wake katika sherehe ya kuzaliwa kwa mrembo huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Maasai club mjini Arusha.
Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald akiwalisha keki baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 katika hafla iliyoandalia na Kinywaji cha Redds na kuanyika katika ukumbi wa Maasai Club mjini Arusha.
MICHEZO UCHANGAMSHA AKILI KWA WATU WOTE
MISS TANZANIA WATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI TANGA
Warembo wa Vodacaom Miss Tanzania 2010 wakipita katika mapango ya Amboni mkoani Tanga jana kujionea maajabu mbalimbali ya maopango hayo wakati wa ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Kanda ya Kaskazini ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010, wakisikiliza maelezo ya historia ya Mapango ya Amboni Mkoani Tanga jana wakati warembo hao walipotembelea eneo hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipiga picha na watoto waliotembelea mapango ya Amboni mjini Tanga jana ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
ZITO KABWE AZINDUA KAMPENI ZA KUGOMBEA UBUNGE KIGOMA
Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kaskazini Zitto kabwe akihutubia mkutano wa hadhra ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampeni zake za kuwania tena nafasi hiyo zilizofanyika katika kijiji cha Mkongoro
Mgombea ubunge jimbo la Kigoma kaskazini Zitto kabwe akivalishwa vazi la jadi la kabila la waha na kutawazwa kuwa mwami (Mtemi) wakati wa uzinduzi wa kampeni zake za kuwania tena nafasi hiyo zilizofanyika katika kijiji cha mkongoro.
WANA CCM SUMBAWANGA WAMKUBALI KIKWETE
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha CCM,Mh Jakaya Kikwete akishuka kwenye Helkopta mara baada ya kuwasili Sumbawanga mjini tayari kwa mkutano uliofanyika jana kwenye uwanja wa Mandele mjini humo.
Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Mh Jakaya Kikwete amefanya mkutano wa kampeni jana na kuhutubia katika uwanja wa Mandele mjini Sumbawanga,amb wakazi wa Sumbawanga walijitokeza kwa wingi kutoka vitongoji mbalimbali vya mji huo. Pichani Mh Jakaya Kikwete akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CCM Bw. Hayeshi ambaye kama atashinda kuomngoza jimbo hilo atakuwa anachukua nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga mjini Mzee Paul Kimiti aliyeng'atuka madarakani mara baada ya kulitumikia jimbo hilo kwa muda mrefu.
mama salma kikwete ziarani mkoani dodoma
Saturday, August 28, 2010
DKT WILLIBROD SLAA AZINDUA KAMPENI LEO
Mwenyeki wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe akimkabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama hicho Mh Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.
Wanachi waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama cha CHADEMA leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar
Wasanii wa Bongofleva Dani Msimamo pamoja na Mkoloni wakiimba jukwaani.
Na Waandishi Wetu
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ameeleza vipaumbele vyake katika muda mfupi, kati na mrefu akianza na mambo makuu matatu endapo atashinda nafasi hiyo.
Dkt. Slaa alieleza hayo Dar es Salaam jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili juu ya mipango yake na jinsi atakavyoitekeleza, endapo atapata ridhaa ya Watanzania kuwa kuongoza serikali ya awamu ya tano.
Mambo hayo ni mabadiliko ya katiba, kurejesha taifa katika misingi ya maadili na uzalendo iliyopotea na uwajibikaji serikalini, ambayo yatatekelezwa ndani ya siku 100.
"Tutakapozindua kampeni zetu tarehe 28 tutazindua na ilani yetu pamoja na action plan (mpango wa utekelezaji). Huu ni uchaguzi utakaotupeleka kwenye mabadiliko makubwa," alisema.
Kwa mujibu wa Dkt. Slaa mpango huo utaonesha jinsi ya kufanya mabadiliko hayo, ili kulirejesha Taifa katika mstari kutokana na kupoteza uadilifu na kuendesha nchi kwa misingi ya kubaguana.
Alitolea mfano wimbo maarufu wa CCM uanaohubiri 'kuwaleta wapinzani, kuchanachana na kuwatupa' kuwa unaimbwa hata mbele ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho lakini hawasemi lolote wakati unahubiri dhana ya mauaji.
Akizungumzia utendaji wa serikali, mgombea huyo alisema kwa sasa serikalini hakuna uwajibikaji wala maamuzi na kero za wananchi zinatatuliwa kisiasa.
Dkt. Slaa alitumia muda mrefu kuzungumzia mabadiliko ya katiba, huku akiainisha vipengele vyenye matatizo kwenye katiba ya sasa, hasa madaraka makubwa aliyopewa rais, yanayompa nafasi ya kuteua watu wengi, ingawa si rahisi kwake kuwafahamu wote.
Alisema atakapoingia ikulu ataunda serikali ndogo yenye ufanisi ya mawaziri wasiozidi 20 ili kupunguza matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima.
Kwa mujibu wa mgombea huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Serikali ya sasa yenye mawaziri 47 ni mzigo kwa walipa kodi, katika mishahara, marupurupu, magari na huduma nyingine.
Alitoa mfano wa Uingereza yenye watu zaidi ya milioni 70, ina mawaziri wasiozidi 20.
Akizungumzia baadhi ya gharama zinazoendesha serikali, alitoa mfano wa magari (mashangingi) ambayo yanauzwa sh. milioni 200 kila moja, akisema kila waziri anatembea na zahanati nne zinazogharimu sh. milioni 50 kila moja.
"Hiyo anasa hatuiwezi, lazima tuachana nazo...Mtu asitarajie akienda serikali ya CHADEMA anakwenda kula. Hili tutaanza nalo kwa katiba ya sasa na baadaye kuliingiza katika katiba tutakayounda, ili idadi ya mawaziri wanaotakiwa ijulikane, asijekutokea rais mwingine akaweka anaowataka kwa kuzingatia uswaiba," alisisitiza.
Mgombea huyo alitoa mfano wa Wilaya ya Karatu ambako chama chake kilikuwa kinaongoza serikali na CCM kuwa wapinzani, kuwa waliweka watendaji ndani ya miezi mitatu walifungwa karibu wote kwa ulaji.
Mambo mengine ambayo Dkt. Slaa anatarajia kuweka mfumo wa utawala utakaopunguza matumizi na kuongeza uwajibuikaji, kama kuondoa nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa na kazi zao kurejeshwa kwa wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye katika majimbo, kuongeza uwajibikaji kwa mawaziri kuthibitishwa na bunge, mawaziri kutokuwa wabunge na rais kushinda kwa zaidi ya nusu ya kura.
Pia CHADEMA kinakusudia kuruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani, kuweka mipaka ya kiutendaji katika mihimili mitatu ya serikali, bunge na mahakama, kuainisha shughuli za usalama wa taifa na kuunda tume huru ya uchaguzi.
Vile vile Dkt. Slaa alisema wanakusudia kuondoa dhana potofu kuwa kila kitu kuhusu jeshi ni siri, bali lijulikane kuwa ni huduma ya umma, bali siri ni mbinu, mikakati na vyombo vyake, lakini si masuala kama ya kashfa ya Meremeta, iliyofishwa kwa sababu ya kuhusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Alisema pia wanakusudia kuwa na jeshi dogo lenye vifaa vya kisasa na lenye ufanisi. Pia watafufua kikosi cha nyumbu ili jeshi litumike kutengeneza magari na vifaa vingine.
Akidokeza juu ya kampeni yake, alisema asingeweza kuweka wazi mikakati, lakini wanayo mambo mengi ya kuzungumza, zikiwamo nyaraka mbalimbali za ufisadi na jinsi serikali inavyotumia fedha za walipakodi kuisaidia CCM.
"Uchafu ndani ya serikali uko kila sehemu, tunazo documents (nyaraka), kwenye serikali za mitaa huko ndo usiseme ufisadi wao ninaujua kila sehemu. Kwa ufupi serikali nzima imeoza na haina uwezo wa kujisafisha," alisema.
Kuhusu ajira, Dkr. Slaa alisema serikali yake itahakikisha kila bajeti inayopangwa inalenga kuongeza kiwango fulani cha ajira badala ya kusubiri wawekezaji ndio walete ajira.
Katika kipango ya muda wa kati ndani ya miaka mitatu, Dkt. Slaa alisema kilimo cha zalishaji wa chakula ama kwa kutumia uwezo wa serikali au kwa kutangaza tenda za kimataifa ili kuondoa aibu ya kila mwaka ya kuomba chakula kwa wahisani.
"Mfano yale mabilioni ya JK yalifanya nini, Kina Kapuya (Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Juma) wanatoa takwimu kuwa watu 44,000 wamenufaika. Watu 44 elfu ni kitu gani kati ya milioni 40? fedha kama hizo zingeweza kutumika kuinua kilimo cha umwagiliaji na taifa likajitegemea kwa chakula," alisema.
Alitumia nafasi hiyo kuziponda trekta ndogo (powertiller) kuwa zimenunuliwa bila utafiti katika baadhi ya maeneo, na matokeo yake zimeshindwa kulima kwa kuwa zinatumia nguvu ya binadamu.
Vile vile Dkt. Slaa alisema ni mipango yake mingine miji na kuweka miundombinu ya umma itakayopunguza msongamano wa magari mijini.
Alisema kwa sasa ujenzi unaondelea ni wa majumba makubwa lakini hakuna miundombinu ambayo muda wake muafaka ni sasa, kwa huko baadaye itakuwa si rahisi kulipa fidia.
Kwa upande wa elimu alisema serikali lazima igharamie masomo hadi kidato cha sita badala ya kufuta tu mchango wa UPE ikasema kuwa imegharamia elimu.
Akizungumzia maisha binafsi, Dkt. Slaa alikiri kuwa aliwahi kuwa padri na vyeo alivyowahi kushika ndani ya kanisa Katoliki, kama Makamu wa Askofu, Mkurugenzi wa Maendeleo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu.
Alitumia nafasi hiyo kumtambulisha mke wa sasa, Josephine, na kuweka bayana kuwa kuanzia mwaka jana alitengana na Rose Kamili ambaye katika maisha yao, bila kufunga ndoa kikanisa, walipata watoto wawili
KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD KUFANYA IBADA MAALUMU KESHO
Mchungaji wa kanisa la Mikocheni Assemblies of God,Getrude Rwakatare akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapi pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo kuhusu maandalizi ya ibada maalumu ya kuombea Uchaguzi Mkuu itakayofanyika kesho katika kanisa hilo. Uchaguzi Mkuu wa Urais,Wabunge pamoja na Madiwani utafanyika Oktoba 31. Kulia ni Mchungaji wa Msaidizi, Dk. Stephen Mutyetumo .
(Picha na Francis Dande)
WASANII WAPOZWA KISANII
MWENYEKITI WA SHIWATA KASSIM TALIB AKIWAONYESHA WANACHAMA MOJA YA VIELELEZO WAKATI WA MKUTANO LEO.
BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO ULIOFANYIKA KWENYE UKIMBI WA AFRICENTRE.
MWENYEKITI wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA), amewataka wachamama wa shirikisho hilo kutumia vikao halali badala ya kusikiliza habari za nje za vikao ambazo msingi wake ni kuwavuruga.
Akizungumza na wanachama jijini Der es Salaam jana, Mwenyekiti wa SHIWATA, Kassim Taalib, alisema anaamini kuwa habari zilizotangazwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari, ziliwafanya wanachama wachache waamini kuwa ni kweli, hivyo kuondoa imani kwa viongozi wao.
“Nasisitiza kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, Shiwata ipo na wala hakuna kiongozi yeyote mwenye nia ya kufanya utapeli na wanaofikiria hivyo wamefilisika kimawazo,” alisema Taalib.
Aidha, alisema shirikisho hilo ni la wanachama, lenye lengo la kutetea haki za wasanii na kubuni miradi mbalimbali, ambayo itawaletea mapinduzi ya kweli ya kiuchumi.
Taalib alisema anatambua mtafaruku huo ulisababishwa na baadhi ya wanachama ambao walijiunga na Shirikisho hilo kwa kufuata mkumbo, bila kujua nia halisi.
Aidha aliwahakikishia wanachama kuwa hawajadhulumiwa, maeneo yao yapo na kwa kudhihirisha hilo, hivi karibuni yataanza kusafishwa na ‘greda’ lililokodishwa kutoka Mkoa wa Pwani.
Taalib alisema, mara baada ya kumalizika kufanyiwa usafi, Shiwata itawaalika viongozi wa kitaifa katika sherehe za uzinduzi.
RAIS KARUME AFUNGUA NYUMBA ZA WATOTO YATIMA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Nyumba mpya ya watoto Yatima iliyopo Mazizini nje ya Mji wa Zanzibar,awali nyumba hiyo ya watoto yatima ilikuwepo Forodhani MjiMkongwe wa Zanzibar,(kulia)Mke wa Rais Mama Shadya Karume,mwenyekiti wa Jumuiya inayoshuhulikia mazingira na maendeleo ya vijana,ZAYEDESA.
TIMU YA TAIFA YA NGUMI YATIA AIBU MABINGWA WA MABINGWA
Friday, August 27, 2010
CHANETA YAPATA MILION MBILI
Kaimu katibu mkuu wa CHANETA ROSE MKISI akipokea hundi ya shilingi milioni mbili kutoka LAPF
CHAMA cha NETIBOLI (CHANETA) kimepatiwa msaada wa fedha taslimu MILIONI MBILI na shirika la Pensheni LAPF kama msaada kwa timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini AFRIKA KUSINI mwezi ujao.
Wakati wa hafla ya kukabidhi hundi hiyo , Afisa masoko wa LAPF , REHEMA MKAMBA amesema msaada huo ni kusaidia timu hiyo kujiandaa na mashindano hayo yatakayoshirikisha mataifa mengi ya Afrika
Naye kaimu katibu mkuu wa CHANETA, ROSE MKISI amesema timu hiyo itaondoka nchini kwenda Afrika kusini SEPTEMBA TANO ambapo ni wachezaji KUMI na MBILI na viongozi WANNE ndio watakaokwenda nchini humo.NA janejohn5.blogspot.com
MISS TANZANIA WATEMBELEA VODA COM ARUSHA
Mkurugenzi wa Vodacom wa Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando (wapili kulia) na Mtaalam wa Habari wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) pamoja na warembo wa Vodacom Miss tanzania 2010 wakiangalia namna teknolojia ya mawasiliano kwa kutumia Video inavyofanya kazi wakati warembo hao walipotembelea ofisi za Vodacom kada ya Kaskazini mjini Arusha leo.
HAPPY BIRTHDAY MISS TANZANIA 2009 MIRIAM GERALD
Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald akimkabidhi msaada wa vyakula na fedha Katibu Mkuu wa Kituo cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi cha Tumaini Kilichopo Arusha, Richard Laizer ikiwa ni maadhimisho yake ya siku ya kuzaliwa aliyofanyika jana. Kwaniaba ya watoto wanaosoma katika kituo hicho ni mtoto Sweetmercy Emmanuel aliyepokea kwaniaba ya wenzake.
TANZANIA YAINGIA MKATABA NA USA KUBOLESHA MIUNDOMBINU YA UMEME
Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Changamoto za Milenia Tanzania. MCA-T Bw. Bernard Mchomvu (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni SYMBION kutoka Marekani Bw. Paul Hinks, wakitiliana saini mkataba wa uboleshwaji wa miundombinu ya Umeme kwa mikoa sita nchini wanaoshuudia nyuma ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Bw. John Haule na Balozi wa Marekani Nchini Bw.Alfonso Lenhardt
MILLENNIUM CHALLENGE ACCOUNT – TANZANIA
MCA-T signs second major energy works contract with a USA-French Firm-M/s SYMBION - AREVA Joint Venture
The Millennium Challenge Account–Tanzania (MCA-T), the Accountable Entity responsible for the management of the implementation of projects funded by the Government of United States of America through Millennium Challenge Corporation, awarded a $45 million contract on 27th August 2010 to a joint venture between Symbion Power and Areva. The contractors will design, manufacture and install 24 power substations in 6 Mainland regions and Zanzibar. .
MCA-T Chief Executive Officer, Mr. Bernard Mchomvu, congratulated the joint venture firms for winning the tender through competitive bidding procedures and urged them to perform an excellent job to the satisfaction of both the financiers and the people of Tanzania.
“We are very confident that you will deliver a high quality work, timely and as per the allocated budget. Do a job that you can look back with pride and satisfaction.”
Speaking on behalf of the joint venture partners, after contract signing, Mr. Paul Hinks, the Symbion Power Chief Executive Officer said,
“We are delighted to be awarded this contract to work with MCA-T to increase capacity of power supply to consumers which will eventually enhance social economic development for the people of Tanzania. We assure you that we will work hard with the view to complete the job on time covering all the 24 sites.”
Other components in the Energy sector include the laying of a second submarine power cable linking the Mainland to Zanzibar, approximately 40 km long (132kV), 100MW from Ras Kiromoni to Ras Fumba. The Contractor, VISCAS Corporation of Japan signed the works contract in April and has commenced design works prior to the fabrication of the cable. Another component is the Distribution Network Rehabilitation and Extension in Six Regions which will involve construction of a total of 78 networks made up of some 252 kms and 1,247 kms of 11kV and 33kV respectively. The package will supply power to villages and urban areas in six Mainland regions namely Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya, Morogoro and Tanga.
In conclusion, Mr. Mchomvu said “on behalf of the Tanzania Government, I would like to express our much gratitude to the American people and in particular MCC for extending its valuable financial support and technical assistance to Tanzania. This has enabled us to sign what we have signed today. We have realistic expectations for an improved performance in the energy sector, both for the well-being of the people and a sustainable economic development of the country at large.
Photo of the event to be inserted here
####
Millennium Challenge Account-Tanzania (MCA-T) is an autonomous and independent Government Entity established to implement a $698 million grant that will reduce poverty by improving infrastructure and thereby promoting economic growth. MCA-T is supported by Millennium Challenge Corporation (MCC), a United States government agency designed to work with developing countries. For mor
TASWA WAJIPANGA KUMPA TUZO KIKWETE
mwenyekiti wa TASWA JUMA PINTO katikati katibu mkuu AMIRI MHANDO kushoto wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TFF leo.
Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA kimeamua kumtunukia tuzo rais JAKAYA MRISHO KIKWETE kutokana na kusaidia maendeleo ya michezo mbalimbali hapa nchini
Pinto amesema taswa wameona mchango wa Rais KIKWETE katika michezo kwa kuleta makocha mbalimbali.
Amesema tuzo hiyo itatolewa siku yoyote kuanzia sasa mara baada ya kupata majibu kutoka ofisi za IKULU kumpelekea tuzo hiyo