Saturday, August 28, 2010

WASANII WAPOZWA KISANII



MWENYEKITI WA SHIWATA KASSIM TALIB AKIWAONYESHA WANACHAMA MOJA YA VIELELEZO WAKATI WA MKUTANO LEO.

BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO ULIOFANYIKA KWENYE UKIMBI WA AFRICENTRE.

MWENYEKITI wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA), amewataka wachamama wa shirikisho hilo kutumia vikao halali badala ya kusikiliza habari za nje za vikao ambazo msingi wake ni kuwavuruga.
Akizungumza na wanachama jijini Der es Salaam jana, Mwenyekiti wa SHIWATA, Kassim Taalib, alisema anaamini kuwa habari zilizotangazwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari, ziliwafanya wanachama wachache waamini kuwa ni kweli, hivyo kuondoa imani kwa viongozi wao.
“Nasisitiza kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, Shiwata ipo na wala hakuna kiongozi yeyote mwenye nia ya kufanya utapeli na wanaofikiria hivyo wamefilisika kimawazo,” alisema Taalib.
Aidha, alisema shirikisho hilo ni la wanachama, lenye lengo la kutetea haki za wasanii na kubuni miradi mbalimbali, ambayo itawaletea mapinduzi ya kweli ya kiuchumi.
Taalib alisema anatambua mtafaruku huo ulisababishwa na baadhi ya wanachama ambao walijiunga na Shirikisho hilo kwa kufuata mkumbo, bila kujua nia halisi.
Aidha aliwahakikishia wanachama kuwa hawajadhulumiwa, maeneo yao yapo na kwa kudhihirisha hilo, hivi karibuni yataanza kusafishwa na ‘greda’ lililokodishwa kutoka Mkoa wa Pwani.
Taalib alisema, mara baada ya kumalizika kufanyiwa usafi, Shiwata itawaalika viongozi wa kitaifa katika sherehe za uzinduzi.

2 comments:

  1. Mara nyingi Binaadam wenye ngozi nyeusi akijaribu kufnya jambo jema ambalo wakati mwingine ni la manufaa, hukatishwa tamaa na wachache ambao hawana nia ya maendeleo, sasa inatakiwa tupate taarifa rasmi kutoka kwa mhusika ambaye anataka kutufanyia jambo kuliko ikuwa 'Mavuvuzela' kwamba mara 'usanii' mara tumedanganywa wakati hatutoi ushahidi stahili kama kwamba risiti ni feki ama taratibu labda hazijafika kunakohusika.
    Tuwe makini kwa sababu sisi ndio mwelekeo unaotakiwa kufuatwa na jamii kuliko kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba ni usanii wakati hakuna ushahidi unaoashiria kutapeliwa.
    Hata vitabu vya mungu vinaeleza kwamba kuna pepo na Moto lakini wengi wetu tunadhani kwamba pepo hakuna, tubadilike na tuelewe kwamba pepo ipo. tuache uvuvuzela na kuwaelewesha wasiojua kama tunajua lakini kama hatujui, tunyamaze

    ReplyDelete
  2. Tuwasaidie wananchi kwamba ni mwelekeo upi waelekee kuliko kuwashawishi kwamba wametapeliwa, hali hiyo inafanana na usaliti ambao hautakiwi, sisi ni waandishi wa habari, kazi yetu kubwa ni kufikisha ujumbe stahili kwa jamii ambayo inatutegemea, sasa tukiwapa taarifa nusunusu hatuwasaidii, tuonyeshe ushahidi wa hili ili tuwasidie, lakini kama na sisi waandishi wa habari hatuelewi. tutawachanganya wanaotutegemea, tuache ubabaishaji huo. tufanye kazi

    ReplyDelete