Sunday, August 8, 2010

FAINALI ZA MASHIDANO YA NGOMA ZA ASILI ZA BALIMI ZAMALIZIKA JIJINI MWANZA


NGOMA TAMU KUITAZAMA



NGOMA ZILIENDELEA KULINDIMA



Mashidano ya ngoma za asili katika kanda ya ziwa yanayodhaminiwa na bia ya BALIMI EXTRA LAGER jana yamefikia tamati katika uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza na Kundi la ngoma toka Kagera - KAKAU GROUP wameibuka na ushindi wa kwanza. Kundi la Kakau ndilo lililokuwa likishikilia nafasi hiyo baada ya kuongoza katika mashidano ya mwaka jana.

Mashindano ya ngoma za asili kwa kanda ya ziwa 2010, yalianza tarehe 17 Julai 2010 na kushirikisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Tabora katika ngazi ya mikoa na vikundi viwili vilyoshika nafasi za juu kila mkoa viliingia katika fainali kuu ya kanda iliyofanyika August 7 jijini Mwanza.

Lengo la mashindano haya yanayodhaminiwa na TBL kupitia bia ya BALIMI EXTRA LAGER ni kuenzi na kudumisha mila desturi za makabila ya kanda ya Ziwa, na pia kuongeza mshikamano wa makabila haya kupitia utamaduni wao.

No comments:

Post a Comment