Wednesday, August 4, 2010

KAMPUNI YA ZAIN NA PSI TANZANIA ZAZAMINI BONANZA LA NANE NANE MOROGORO




Mkurugenzi wa Masoko wa PSI Tanzania,John Wanyancha (kushoto) akimkabidhi Jezi, Mkurugenzi wa Popular Sports Entertainment, Osman Kazi, Dar es salaam jana kwa ajili ya mashindano ya nanenane yanayoamasisha Kilimo Kwanza mkoani MorogogoTAASISI ya Popular Sports Entertainment ya imeandaa masindano ya kusapoti kauli mbiu ya kilimo kwanza kupitia michezo itakayofanyika Agosti 6-7 katika viwanja vya Seminari ya Morogoro.

Akizungumza Dar es Salaam leo,Mkurugenzi wa Popular Sports Entertainment, Osman Kazi,alisema mashindano hayo yatashirikisha timu 12 kutoka katika vijiji mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam na zingine kutoka katika mkoa wa Morogoro na kuongeza kuwa wameamua kuyapeleka nje ya jiji hilo mwaka huu ili kutimiza lengo lao.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kushirikisha michezo kwa wakulima na kuwapa hamasa katika mpango wa kilimo Kwanza ili kuweza kutimiza lengo la kauli mbiu hiyo mhimu hapa nchini.

Othmani alizitaja baadhi ya timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo ni PSI Tanzania, Zain Tanzania, na Farm base ambazo ni timu za kampuni zilizojitokeza kudhamini mashindano hayo, huku zingine zikiwa ni TASWA Fc, Kingolowila, sangasanga, pamoja na Full Way.

Alisema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa endelevu atapata kombe pamoja na pesa taslimu Sh. 200,000, mshindi wa pili atajipatia Sh. 100,000, na wa tatu ataambulia Sh. 500,000 huku timu nane za mwanzo zikijipatia jezi seti moja kutoka kwa wadhamini na zawadi mbalimbali.


Meneja Miradi na Mauzo wa Kampuni ya Zain, Onesphory Mtuy (kulia) akimkabidhi kombe, Mkurugenzi wa Popular Sports Entertainment, Osman Kazi, Dar es salaam leo kwa ajili ya mashindano ya nanenane yanayoamasisha Kilimo Kwanza mkoani Morogogo.

No comments:

Post a Comment