Wednesday, August 25, 2010

TIMU YA TAIFA YA POOL YAINGIA KAMBINI KWA UDHAMINI WA BIA YA SAFARI




MCHEZAJI WA TIMU YA tAIFA gODFREY mUHANDO AKIPIGA MPIRA WAKATI WA MAZOEZI
TIMU ya Taifa ya mchezo wa Pool imeanza kambi kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Ufaransa Novemba 8 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Tanzania (TAPA), Amos Kafwinga alisema kambi hiyo itajumuisha wachezaji 8 chini ya Kocha wao Mkuu Denis Lungu kutoka Zambia.

Kafwinga alisema wachezaji hao watakuwa wanafanya mazoezi mara mbili kwa wiki katika baa ya Blackpoint iliyopo Makumbusho, Dar es Salaam.

“Maandalizi yanayofanywa yataisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo ya kuitangaza nchi kupitia mchezo huo unaodhaminiwa na bia ya Safari Lager,” alisema Kafwinga.

Wachezaji wanaounda timu hiyo ni Felix Athanas, Abuu Shabani, Godfrey SWai, Mohamed Idd, Omary Akida, Godfrey Mhando, Aliakber A Akberali na Arjuan Lavinja.

Nae kocha wa mchezo Lungu alipo ulizwa kuusu maendeleo ya kambi hiyo alisema wachezaji wote wapo katika hili nzuri ya mchezo na watahakikisha wanaitangaza vema bendera ya Tanzania kimataifa


Kocha wa Timu ya taifa ya mchezo wa pool. Denis Lungu (katikati) akiwapa maelezo wachezaji wa timu hiyo kwenye kitabu wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika makumbusho Dar es salaam

No comments:

Post a Comment