Friday, September 17, 2010

TIMU ZA ILALA,KINONDONI NA ARUSHA ZAJIAKIKISHIA KUINGIA ROBO FAINAL



Waandishi wa habari wa michezo,kutoka kushoto ni Alex Lwambano wa Radio Claus,Jane John wa TBC na Rajabu Mhamila super D wa Majira wakiwajibika Kaunter.





Na Mwandishi wetu, Arusha.
WAKATI mkoa maalum wa kimichezo wa Temeke ukianza vibaya fainali za mashindano ya taifa ya pool yanayojulikana kama 'Safari Lager National Pool Championship 2010, mabingwa watetezi mkoa wa Ilala na Kinondoni zenyewe zimeanza vema fainali hizo.
Fainali hizo ambazo zinafanyikia kwenye ukumbi wa Matongee Club, zinashirikisha jumla ya mikoa 14 ya Tanzania Bara ikiwa na pamoja na mchezaji mmoja mmoja wanaume na wanawake kutoka katika mikoa hiyo.
Temeke ilianza vibaya fainali hizo zinazodhaminiwa na bia ya Safari Lager baada ya kupata kipigo cha magoli 14-11 kutoka mkoa wa Mwanza, mabingwa watetezi, Ilala yenyewe ilianza vema kutetea ubingwa wake baada ya kuichapa Iringa magoli 15-10.
Mkoa maalum wa kimichezo wa Kinondoni nao ulianza vema fainali hizo baada ya kuikandamiza Marogoro magoli 17-8, huku wenyeji wa mashindano hayo, Arusha ikijihakikishia kucheza robo fainali kufuatia kushinda michezo yake miwili dhidi ya Manyara na Mbeya kwa kuibuka na ushindi wa magoli 16-9 kwa kila mchezo.
Wageni wa mashindano hayo mikoa ya Kagera na Shinyanga ambayo imeanza kushirikia mashindano hayo kwa mara kwanza mwaka huu, ikianza vibaya mashindano hayo.
Mkoa wa Kagera ulibanjuliwa magoli 17-8 na Tanga na Shinyanga ikilala kwa magoli magoli 18-7 kutoka mkoa wa Morogoro, nao mkoa wa Dodoma ulijiweka katika mazingira mazuri ya kucheza robo fainali baada ya kushinda michezo yake miwili dhidi ya Tanga na Iringa ambapo iliifunga Iringa magoli 13-12 na ikaichapa Tanga 18-7, katika mchezo mwingine Mbeya iliichapa Kilimanjaro magoli 16-9.
Mashindano hayo yanatarajia kumalizika kesho kwa bingwa kuondoka na fedha taslim Sh.3,500,000 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo bia ya Safari Lager.
Mashindano hayo yatafungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdory Shirima ambaye ndiye atakayekuwa mgeni rasmi kwa kilele cha fainali hizo.
BURUDAN ZISIZO NA KIKOMO ZIMEAMIA MATONGEE KATIKA MASHINDANO YA POOL TAIFA

No comments:

Post a Comment