Wednesday, September 22, 2010

ZAIN YAPUNGUZA GARAMA ZA UPIGAJI SIMU KWA 50%


Kampuni ya simu za mkononi ya Zain, inayoongoza kwa viwango nafuu na huduma ubora nchini, imetangaza punguzo la gharama za simu kwa wateja wake kwenda mitandao mingine kwa asilimia hamsini.

Kuanzia sasa, wateja wa Zain wataweza kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama ndogo ya sh 3 kwa sekunde siku nzima.

Punguzo hili ni muendelezo wa mkakati wa Zain wa kutoza viwango nafuu baada ya kuanzisha sh 1 ya kweli isiyo na upinzani nchini miezi michache iliyopita.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na punguzo hili jijini Dar-es-salaam leo, Sam Elangalloor, Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania amesema, “Tunajivunia zaidi kwa kuwa mtandao nafuu hapa nchini kuliko mtandao mwingine wowote na katika kuthibitisha hilo, leo tena tumeweza kushusha gharama mpaka nusu ya gharama za mwanzo. Tunaamini kila mtanzania ana haki ya kuwasiliana na kwa kuzingatia hilo kuanzia Ijumaa ya tarehe 17 mwezi wa tisa,2010 zaidi ya wateja wetu milioni 5 watafurahia punguzo hili la asilimia 50.

Zaidi ya hayo, wateja wa Zain wataweza kupata sms 4 za bure kwenda mitandao mingine yeyote.

“Tunaamini unafuu wa gharama hizi,upatikanaji wa huduma nzuri ndicho wateja wetu wanachokitegemea kutoka kwetu kama watoa huduma na tumenuia kufanya hivyo. Wateja wetu hivi sasa wataweza kuongea na ndugu zao, marafiki na kufanya biashara kwa uhakika zaidi katika mtandao wetu ulionea zaidi.

Kwa punguzo hili la viwango vya simu za mkononi, Elangalloor alisema kwamba punguzo hili kubwa limekuja sambamba na dhamira ya kampuni ya Zain katika kuhakikisha gharama za simu ni nafuu kwa kila mtu nchini.

“Wateja wote wa malipo ya kabla na baada watanufaika na punguzo hili. Pia mtakumbuka ya kwamba ni hivi karibuni tu pia tulitoa punguzo za gharama za intanet na za modem hivyo kuwezesha watu wengi zaidi kuwasiliana bila upinzani”, aliongeza Elangalloor.

Akiongeza, Cheikh Sarr, Mkurugenzi wa Masoko, alisema kwamba “mbali na kujidhatiti katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu wote, katika kupiga simu na kutumia mtandao utagundua ya kwamba viwango vyetu ni vya ushindani mkubwa, tumeenea katika maeneo mengi zaidi na katika kasi ya hali ya juu,hali ambayo inatoa uzoefu wa tofauti wa matumizi ya simu za mkononi hivyo kuchangia matokeo chanya katika uchumi kwa ujumla wake.

For More Enquires Contact

Muganyizi Mutta

Zain Tanzania Public Relations Manager

0786 670 711

No comments:

Post a Comment