Wednesday, September 1, 2010

Zain yatoa futari kwa yatima Mbeya

Baadhi ya watoto katika kituo cha Elimu kwa watoto yatima Kihumbe cha Mbeya wakipata futari ya pamoja iliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania mwishoni hivi juzi
Meneja Huduma za Jamii Kampuni ya Zain Tanzania Bi.Tunu Kavishe, Meneja Biashara wa Zain Mbeya Marwa Patrick na Mkuu wa Kituo cha Elimu kwa watoto yatima Cha Kihumbe cha Mbeya Veronica Mboma wakati wa makabidhiano ya vyakula kwa ajili ya futari wakati wa mwezi wa ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kituoni hapo.




Kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa Build Our Nation, juzi ilitoa futari katika kituo cha Elimu kwa watoto yatima cha Kihumbe cha mkoani Mbeya kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani.

Futari hiyo ambayo ilitolewa na Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe iliambatana na misaada mingine ya vyakula vikiwemo mchele, Unga, Sabuni na Mafuta ya kupikia.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe alisema kuwa Zain wameamua kutoa msaada huo kama sehemu yake ya kujali jamii kupitia mradi wake wa Build Our Nation.

“Siku ya leo, tumeamua kufuturu pamoja na watoto yatima wanaotunzwa na kituo cha watoto yatima ambacho pia kinatoa elimu ili kudhihirisha kuwa Zain iko karibu na jamii wakati wote, alisema Tunu Kavishe, Meneja Huduma za Jamii wa Zain.

Akizungumzia msaada huo, Veronica Mboma Msimamizi kituo hicho alisema kuwa wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Zain kwa ajili ya kuwakumbuka watoto yatima katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani na kuyaomba mashirika mengine kufuata mkondo huo wa kuwajali watoto yatima.

“Kwa niaba wa wafanyakazi wa kituo hiki napenda kuwashukuru Zain kwa moyo wa upendo na tunahamini kuwa tutaendelea kuwa pamoja nanyi hata siku za huko mbeleni, AlisemaVeronica Mboma

Mikoa mingine ambayo kutafanyika hafla za kufuturisha kutoka Zain ni Dar es Salaam, Pemba, Songea, Morogoro, Tabora, Kigoma na Kagera.

Kavishe alisema kuwa zaidi ya miaka mitano, mbali na juhudi za kusaidia jamii kwa namna mbalimbali hapa nchini, hususan katika sekta ya elimu, kampuni ya simu ya Zain imejiwekea utaratibu wa kuwa inafuturisha wadau mbalimbali katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment