Friday, October 15, 2010
KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA
This is the Nyerere legacy I hold close to my heart when I see today's Tanzania: Nyerere - A Leader Who Dared! (Nyerere - Kiongozi aliye thubutu).
Whatever may be your view of his legacy, Nyerere was the author of his story; and to the benefit of many across Africa and the world at large, he dared to do it his way. Nyerere challenges leaders of today to dare to be the authors of their story and to dream and act in support of a vision greater than the moment, even when faced with the greatest odds and most compelling adversity…
Pengine bila kiongozi kama Nyerere kusingekuwa na Mandela wala Afrika Kusini ilio huru na ndiyo maana Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza aliyo itembelea Mandela baada ya kutoka jela. Lazima tukubali na kujivunia kuwa na kiongozi shupavu na mwenye muono wa namna hii. Hususani mwaka huu wa Kombe la Dunia, dunia ilipo shuhudia manufaa halisia ya ukombozi wa Taifa kubwa kama Afrika Kusini na kuweza kulileta Kombe hilo ndani ya bara letu. Tulistahili tumpe sifa Mwalimu kwani ndie kiongozi pekee aliye thubutu kusimamia mapambano dhidi ya Mabeberu bila kikomo. Si Mmarekani, si Mchina, si Mholanzi bali ni Taifa changa la Tanzania lililo kuwa mstari wa mbele likiongozwa na Mwalimu J K Nyerere - Kiongozi aliye thubutu.
Pengine bila kiongzi kama Nyerere tusingekuwa na taifa lenye mshikamano na lenye kuchukia utengano kama ilivyo sasa Tanzania. Siwezi fikiri ni wangapi walio na ujasiri wa kupangua mifumo ya utawala wa kikabila na wa kikoloni ili waweza kusimamia mwono wao wa Taifa moja linalo takiwa. Nyerere alidhubutu kufanya hivi. Hakutumia muda wake mwingi kulalamika na kushangaa mapungufu. Bali alithubutu kupangua na kupanga upya mambo jinsi alivyo ona yeye inafaa bila kujali maneno na minong'ono ya wanafiki wachache na wasio jali maslai ya wengi au kuwa na muono wa mbali. Hii ndio ilikua tabia yake mzee wetu Mwalimu J K Nyerere - kiongozi aliye thubutu.
Kama Baba wa Taifa alithubutu kufanya makubwa kama haya mbele ya upinzani mzito na vitisho ndani na nje ya nchi, je wewe Mwana wa Taifa unathubutu katika lipi?
C V Magavilla
www.magavilla.com
No comments:
Post a Comment