Marquee
tangazo
Friday, October 1, 2010
Mgombea urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kama akichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar,
Mgombea urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kama akichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar, ataangalia upya viwango vya kodi ikiwa ni pamoja na kuvipunguza viwango vya ulipaji kodi ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi.
Alisema utozaji kodi kwa kiwango kidogo kutawavutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza Zanzibar na kwamba uwekezaji huo pia utawanufaisha Wazanzibari wote tufauti na ilivyo hivi sasa ambapo wengine wamekuwa wakikwepa kuilipa.
Ahadi hiyo ameitoa jana alipokuwa akizungumza na wajasiriamali kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sunni Madrassa Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema wafanyabiashara wadogo wadogo wanapaswa kusaidiwa na kuongezewa ujuzi ili waweze kuingia katika ushindani wa biashara ambapo Tanzania imeridhia kuingia kwenye soko la pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Nchi yoyote inayoendelea duniani, haiwakomoi wananchi wake katika kodi na badala yake inawawekea viwango vya chini, ili wazidi kuongezeka na mimi nitapunguza viwango vya ulipaji wa kodi kama mkinichagua kuingia ikulu,’’ alisema.Maalim Seif, aliongeza kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF haitaruhusu wawekezaji matapeli wenye lengo la kunufaika kupitia migongo ya wananchi, bali itaruhusu wawekezaji ambao watainufaisha Zanibar na wananchi wake.Alisema hawezi kuruhusu mtu kunufaika kwa gharama za Wazanzibari, lazima wawekezaji wenye tabia kama hiyo watawajibishwa kwani kuwaadhibu wananchi kwa kuwatetea wageni ni kosa na ni kuwadharau wananchi wazalendo.
Mimi siamini kuwa kodi kubwa au utitiri ndio msingi wa maendeleo ya nchi, pia siamini kuwakamua wafanyabiashara wadogo wadogo ndiko kujenga nchi, naamini wafanyabiashara hawa wanatakiwa kusaidiwa ili wajiendeleze katika biashara zao,” alisema.
Aliongeza kuwa akiingia madarakani atahakikisha mafunzo kwa wajasiriamali yanatolewa kwa kiwango cha juu ili kuwajenga uwezo wa kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi kwa lengo la kukuza kipato chao.
Alisema wafanyabiashara wengi hususan wadogo wadogo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa utundu, lakini wakipatiwa mafunzo watapiga hatua kubwa zaidi na taifa linanufaika.
http://www.kingkif.blogspot.com/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment